Mkuu
Kubota na wengineo...
Kuhusu suala la kuwafanya kuku wa kienyeji kuangusha mayai kuna kautafiti kamefanywa na taasisi moja inatoa jarida linaitwa Mkulima Mbunifu (link yao ni
Mkulima Mbunifu), wamegundua vitu vikubwa viwili..
Kwanza kuku wa kienyeji anaweza kuangusha mayai zaidi ya 200 akitunzwa vizuri tofauti na dhana iliyozoeleka ya 50 mpaka 80 kwa mwaka.
Pili kuna mmea ukiwapa wanaangusha mayai balaa ila hauna jina la kitaalamu, na maelezo yao ni haya hapa chini (Nimeshidwa ku attach picha ya hako ka-mmea network iko slow sana ila document iliyo na hiyo picha iko kwenye attachment hapo chini, kama kuna mtu anaweza ku-extract na ku-upload picha afanye hivyo ili watu wote wauone huo mmea)...]
Nimekusoma mkuu, kweli hakuna linaloshindikana duniani. Mmea nimeuona kwenye link uliyotuwekea nimejaribu kukopi and paste imedunda! Ila sijawahi kuuona kabisa. Hata hivyo nitafuatilia huo utafiti kwa karibu maana kama ni hivyo basi inaweza kuwa inalipa sana. Ahsante kushare mambo mapya haya!! Huo mmea itabidi upewe promo kubwa sana na kama ikibidi liwe zao la biashara kabisa maana haya uliyoyawasilisha kuhusu mmea huo siyo mambo madogo !!