Ufugaji wa Kuku wa Kienyeji na Masoko yake

Kubota bado najifunza kuhusu ulinzi, aina ya mbwa: lazima nipate waliofunzwa au ninunue mdogo nimfundishe mwenyewe? Je mbwa yeyote anafaa?
Sorry Mama Joe nilipitiwa kukujibu, nunua mdogo uanze nae haina haraka! Kwa mbegu zetu hapa Tz naona mbwa ni mbwa tu, ingekuwa ni ulaya kuna mbwa wadogo kama paka. Lakini ukianza nae akiwa mdogo ukamtunza na lishe nzuri anakuwa na nguvu na umbo la kutosha tu. Hebu cheki kifaa changu hiki nimeattach hapa, usione hivyo huyu askari ninamheshimu sana !!
 

Attachments

  • CIMG1006.JPG
    539.7 KB · Views: 392
  • CIMG0979.JPG
    871.2 KB · Views: 370
Kubota I salute you! yaani hizi picha za free range zimenitia nguvu hasa, wengi wetu bado tunachukulia kuku kama ufugaji mdogo wa uwani (backyard poultry keepers) ambayo kwa kweli sio uzalishaji mkubwa bali ni matumizi madogo ya nyumbani na pocket money tu. Hizi picha zimenipa nguvu ya uzalishaji mkubwa kwa kuku wa kienyeji, Hongera kwa picha ya mbwa, basi nitafuata ushauri wako maana nilidhani kuna aina maalumu tu ndo inafaa kikubwa nitatafuta wadogo nijaribu kuwafunza mwenyewe.
 
Mkuu Kubota na wengineo...

Kuhusu suala la kuwafanya kuku wa kienyeji kuangusha mayai kuna kautafiti kamefanywa na taasisi moja inatoa jarida linaitwa Mkulima Mbunifu (link yao ni Mkulima Mbunifu), wamegundua vitu vikubwa viwili..

Kwanza kuku wa kienyeji anaweza kuangusha mayai zaidi ya 200 akitunzwa vizuri tofauti na dhana iliyozoeleka ya 50 mpaka 80 kwa mwaka.

Pili kuna mmea ukiwapa wanaangusha mayai balaa ila hauna jina la kitaalamu, na maelezo yao ni haya hapa chini (Nimeshidwa ku attach picha ya hako ka-mmea network iko slow sana ila document iliyo na hiyo picha iko kwenye attachment hapo chini, kama kuna mtu anaweza ku-extract na ku-upload picha afanye hivyo ili watu wote wauone huo mmea)...

" Unaweza kufikiria ni mzaha lakini wafugaji wanafanya haya na kuona Mafanikio kwa k i a s i
Kikubwa s a n a . M i e z I Michache iliyopita t u l i p o – tembelea w a k u - l i m a h u k o Njombe, t u l i kutana na u t a f i t I huu ambao wakulima wamefanya na kujaribu wenyewe na kisha kuona mafanikio.
Utafiti huu unahusisha mmea mdogo sana ambao bado hatujaweza kufahamu jina leke kitaalamu au kwa Kiswahili sahihi, lakini kwa lugha ya Kibena unafahamika kama
Muyeheyehe. Muyeheyehe kwa Kibena ni mmea ambao una vijitawi vidogovidogo
ambavyo ni kama mfagio (dhaifu) ndio maana wakaita muyeheyehe. Unapokomaa unabaki na vijitawi na vijinundu vidogo-vidogo. Mmea huu hustawi sehemu ambayo haina rutuba au iliyolimwa kwa muda mrefu.
Wafugaji wa eneo hili wanaeleza kuwa baada ya kuona hauna jina linalotambulika na ni mmea ambao ulikuwa unadharauliwa sana waliamua kuupa jina hilo. Mmmea huu unasaidia kuku kutaga mayai mengi zaidi ya ilivyokuwa kawaida.

Namna ya kuandaa
Ng`oa mimea hiyo upate ya kutosha. Twanga na kuanika sehemu yenye kivuli hadi ukauke ili kupunguza kupotea kwa virutubisho kwa njia ya hewa. Rudia tena kutwanga ili kupata unga ambao utautunza kwa muda mrefu.

Namna ya kutumia
• Changanya kijiko kimoja kikubwa cha chakula kwenye maji lita 5 ya kunywa kuku.
• Wape kuku kwa muda wa wiki moja mfululizo. Baada ya hapo wape kuku mara mbili kwa wiki, na kuendelea.

Njia nyingine
Chemsha maji kisha chukua majani nusu kilo, weka hiyo dawa kwenye ndoo ya lita kumi na ujaze maji ya moto na kufunika. Acha kwa saa 12-24 inakuwa tayari. Changanya maji kwa uwiano wa 1:2 Dawa lita moja maji ya kawaida lita 2 utachanganya kulingana na idadi ya kuku wako na kiasi cha maji wanachohitaji kwa siku.
Wape maji hayo kama ilivyo kwenye matumizi ya unga. Wakati mwingine ili dawa hii ifanye kazi vizuri zaidi unaweza kuchanganya na unga wa majani ya lusina, calliandra, alfa alfa na chokaa, mchanganyiko huu ni kwa uwiano wa muyeheyehe lita 1 kwa robo tatu lita ya mchanganyiko wa lusina ,calliandra alfa alfa na chokaa.
Pia dawa hii inasaidia kuwakinga kuku dhidi ya magonjwa ya kideri. Kwa kutizama picha, hiyo unaweza kuutambua mmea huu kutoka katika eneo lako na ukajaribu kuutumia. Ni vizuriwakulima/wafugaji wa kujaribu njia za asili na rahisi huku wakiwashirikisha watafiti na wataalamu ili waweze kuwa na mafanikio zaidi.
"
 

Attachments

Last edited by a moderator:
Kaka mkuu Kubota, naomba unipatie websites tofauti tofauti za uchinani na sehemu nyingine ulizo na ujuzi nazo juu ya bei za Incubators. Pamoja.
 

Kaka mkuu, hali yako kwanza? Mi swali langu lita diverge kidogo, ni kuwa ningependa kujua njia tofauti tofauti juu ya kuliface tatizo kubwa la kuku wa kienyeji, la ugonjwa ambao husababisha vifo vyao kwa wingi, je kuna njia gani mbadala huwa zinatumika? Asante.
 

Kweli nchi hii ni nzuri sana! Picha hizo kama za Mbeya Mbeya au Iringa Iringa au ni wapi!?Zinatia moyo! Hongera sana.
 
Asante kaka mkuu, nimeiona na ipo mingi sana ila mi pia jina kusema ukweli silifahamu ile huu mmea upo na tunashkuru sana kwa elimu uliyotupatia...:yo:
 
 
 
Asante kaka mkuu, nimeiona na ipo mingi sana ila mi pia jina kusema ukweli silifahamu ile huu mmea upo na tunashkuru sana kwa elimu uliyotupatia...:yo:
Haina neno mkuu..hapa ndio JF, heshima kwa mkuu KUBOTA kwa kumwaga nondo zake hapa....amenisaidia sana....
 
Asante Sana Kubota.
Umefanaya kazi nzuri sana kufungua ubongo wangu. Naomba endelea kutoa Elimu hii ya mbinu/utaalamu wa kufuga kuku wa kienyaji kisha kazi kwngu.
 
Hebu tujaribu kuelewa amejaribu kutupa mwanga tena n mim nilikuw gizani.Asante
 
 
Naaaam!

Kubota
Mama timmy
asigwa
Mama Joe
Chansa
bacha
Kunta Kinte

Na wadau wenzangu wote wa jukwaa lengwa la ujasiria,Ninapenda niwasalimu wote katika Jina lake Bwana wetu Yesu Kirsto!

Awali ya yote kabisa nataka mniwie radhi kwani tangu katikati ama mwanzoni mwa mwezi wa tatu sikuwa on line kbs kwa sababu iliyokuwa nje ya uwezo wangu!
Ila hakika namshukuru Mwenyenzi MUNGU mwenye mamlaka kwa wote kwani nimerudi tena na sifa daima ninamrudishia!
Hakika tuliachana nikiwa na vinyoa wapatao 60 bila ya kukosea waliototolewa tarehe 25.02.2013 na hakika hajafa hata mmoja kwa ugonjwa ila wawili kati ya hao kwa bahati mbaya wamedondoka toka chumba chao na kuingia kwa kuku wakubwa na wakauawa kuku wakubwa na tundu lile nilikuwa dhibiti na sasa kila kitu ni murua kabisa na mjue ya kwamba vinyoa hivyo wako na kuku wawili tu!

Sina mengi ila kwa kuwa nimerudi rasmi hakika nitakuwa on line full time! Na mjue ya kwamba chakula cha hawa vinyoa muda wote ni starter tu ile chickmarsh sijapata wa sijahangaika nayo baada ya kuona mwenendo wao si mbaya!
Muwe na wakati mzuri ila hakika mjue kwa sasa nipo on line!

Asanteni na mubaki na Amani yake Bwana!
 
Last edited by a moderator:
Hongera sana mkuu kwa kuleta mrejesho.... Najua hao vinyoya wakikua wakaungana na mama zao karibia wataleta jeshi kubwa sana la kuku... Hongera sana kwa kuuthubutu....
 
Last edited by a moderator:
Habari wadau wote wa ufugaji kuku , mlipotea sana ili tunashukuru Mungu kila mmoja anarudi na jipya jema la kushare, asante kwa feedback za LiverpoolFC na vinyowa wengi, nashukuru sana Asigwa kutushirikisha mmea wa ajabu! Kubota tunashukuru kwa kushare uzoefu wako ktk kufuga kuku wa kienyeji, kifupi mimi nilishalemaa na wa kisasa nilihitaji sana ujuzi jinsi ya kufuga hawa wa kienyeji na nashukuru nimepata ujuzi na maarifa mengi. Nimepunguza na kuacha matumizi ya madawa ya kemikali na kuegemea zaidi kwenye organics au ya kienyeji kama walivyfundisha hapa. Kupitia JF pia nilihamasika kuanzisha kibustani hata sehemu ndogo za maua na pilipili mbuzi, hoho, mbogamboga, mipapai na mitopetope imekubali vizuri na hivyo kuchangia kama chakula na dawa kwa kuku. Ninaongezea milonge ingawa nafasi ni finyu kiasi nahitaji kutanuka sasa. Ukifuata mafunzo kupitia thread hii yaani kuna kunufaika kwingi. Mimi nilianza na chotara 246 tarehe 5/2/2013 na hadi sasa wamepona 240. Sita kwa kweli walikuwa dhaifu na walikufa wiki ya kwanza na ya pili. Nawawekea picha zao wakiwa vifaranga hadi sasa nimewagawa makundi mawili. Asante wote kwa moyo wenu wa kujitoa kujibu nilipokwama, Reti kwa vifaranga na Kubota kwa mchango wako mkubwa. Mbarikiwe
 

Attachments

  • Chicks2.jpg
    41.1 KB · Views: 441
  • Chicks1.jpg
    33.9 KB · Views: 395
  • group A.jpg
    52.1 KB · Views: 428
  • group B.jpg
    62.5 KB · Views: 450
Hongera sana Mama Joe. Hao uliowagawa sthemu mbili mbona kama wamebanana au ni picha tu? Kwa kweli wamependeza na ina tia moyo, umekuwa unawalisha nini hadi sasa? Nauliza kwani niko njiani kuanza na hao chotara. Nadhani hujatambua una vijogoo wangapi na majike wangapi kwa umri huo wa miezi miwili na sjku kumi!?
Kaza buti tuko pamoja humu kwenye JF. Asanteni wadau wote.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…