Ufugaji wa Kuku wa Kienyeji na Masoko yake

Kubota na co salaams, sisi tupo tunaendelea vizuri tu. Ukipita nymba yenye makelele ukaona kimya ujue tunakula! Sasaivi tunaongelea masoko kule kulikuwa na uzi wa Eliphas. Masoko ya reja reja ni ya kubahatisha. Wateja wangu wote wa kuku wa kisasa wanajibu kama kasuku "nitafute ukiwa na kuku 400 kuendelea....' wakati mie nauza jogoo 10 au 20 kufanya kuwapunguza tu ila nimecheck soko liko poa sana tu. Kingine wengi wanawataka kwa ajili ya kufuga na hivyo wanangangania tetea wasioanza kutaga sasa kwa vile hii ni stock ya kwanza imebidi niwanyime. Kuhusu Chakula cha vifaranga mimi sijaka tama na endapo nitachukua vifaranga karibuni nitajaribu hata ikibidi nihamie mashine nijifunze mbona wengi hawana uchoyo ni sisi tu kukosa mtaji mkubwa wa kusaga chakula kingi na kupenda kununua mfuko kila ukipata kidogokidogo. Niwatakie siku na kazi njema
Mama Timmy, Mama Joe, Asigwa, LiverpoolFC, Guta, n.k, upweke umenizidi, mko wapi wakubwa? Feedback zije wajameni!
 
hahaaaaaaaaa umenikumbusha mbali kweli mimi mbwa wamefugwa nyumbani utotoni sikuwa karibu nao sana. Nilipoanza kufuga mtu alimpa motto wangu kambwa kadogo kiasi kwa kweli sikuwa na mind kanakula nini hasa ingawa dagaa wanakanunulia nilichokuja shtuka kukuta miguu ya kuku nyuma ya banda ilibidi nikarudisha fasta. Kweli inabidi utafute mbwa mzuri sio kila mbwa anafaa.
Asante sana,dog nlpata mdogo akala kuku akazaa watoto nao wakala kuku,nkawachapa usku wanenda kuvnja mabanda ya majiran
 
Wakuu wote (Kubota, Mama-Timmy, Mama-Joe, Asigwa, LiverpoolFC, Guta, n.k, n.k, n.k); Jamani Mwenyezi Mungu awabariki sana sana sana. Wajasiriamali tunaelimika sana.
Mie nilitaka nikasome certificate ya vet ili niweze kufuga kuku wa asili/kienyeji vizuri, lakini kwa kusoma uzi huu, pamoja na nyuzi nyingine hapa JF, basi mie ni mfugaji bora sasa wa Kuku wa asili/kienyeji.
Narudia tena. Mwenyezi Mungu awabariki sana.
 
Wadau nataka kumuanzishia mama mradi wa kuku wa kienyeji. Napataje breed nzuri ya hao kuku?nimeskia hapa watu mnataja mbegu za kiisrael,ndo nawapata wapi hao?
 
Mama Timmy, Mama Joe, Asigwa, LiverpoolFC, Guta, n.k, upweke umenizidi, mko wapi wakubwa? Feedback zije wajameni!
Tupo mkuu hatujapotea tupo sana aisee...nilikuomba unitag kwenye uzi mpaka leo hujanitag mkuu..ndio maana someties inakua kazi kuufuatilia na kutoa mrejesho wa uzi...

Ubarikiwe lakini katika kila ulifanyalo mpaga uduwae...
 
Wadau nataka kumuanzishia mama mradi wa kuku wa kienyeji. Napataje breed nzuri ya hao kuku?nimeskia hapa watu mnataja mbegu za kiisrael,ndo nawapata wapi hao?
Mtafute mkuu mmoja humu anaitwa Chasha atamaliza hiyo maneno yoote....
 
Last edited by a moderator:
Mama Timmy, Mama Joe, Asigwa, LiverpoolFC, Guta, n.k, upweke umenizidi, mko wapi wakubwa? Feedback zije wajameni!
Kubota kaka yangu natumai umzima wa afya!kwa upande wangu namshukuru Mungu kwa afya na hatua nipigazo kila siku ktk maisha yangu.kuku wangu wanaendelea vzr na kwa sasa niko kwenye zoezi la kutotolesha kwa kutumia kuku wachache mara mbili.changamoto ni nyingi sana ila na jaribu kuzigeuza kuwa ni shule kwangu.
 
Safi sana mwanamke hapaswi kukata tamaa Kirahisi.ninaamini safari hii unamaliza mchezo nasi tutajifunza kupitia kwako.nakutakia mafanikio makubwa.
 
Chotara hawaatamii japo niliwahi ona mmoja mmoja wanaatamia..chotara anahitaji mtu mwenye muda wa kuwahudumia vinginevyo utakula hasara kila siku.kwangu mimi chotara ni chuma ulete kwani wana gharama kubwa sana kwenye utunzaji wao.ukianzia chakula,madawa na kikubwa ni muda utakaoutumia kuwahudumia.ila Kama vyote hivi unavimudu basi utapata faida
 
Namshukuru Mungu na ushauri wenu ni kweli tukikazana tutaweza tu, changamoto kubwa ni magonjwa ya ghafla kutokea ila nashukuru yaani kila likija hili unakuta mwingine hapa kesha leta na ufumbuzi umejadiliiwa yaani imenisaidia sana sikuwa na Dr yoyote wa mifugo zaidi ya kupata ushauri hapa, kwa RETI na kwenye phamarcy. Sikutaka kuchukua mkopo nilitaka niende taratibu kwa kujibana tu na kupunguza matumizi yasiyo lazima. Naomba nikutie moyo mama Timmy kuku chotara hawana tofauti na hawa kienyeji kwa kulisha na dawa, mimi nimefuga wale wa kisasa ndio nimehamia kwa hawa, ukuaji wa hawa chotara ni wa haraka wakati hawahitaji gharama kubwa kihivyo maana hawali chakula kingi kama wakisasa wala hawahitaji vitamin isipokuwa wiki chache 2 za mwanzo. Kwavile wanakua haraka tayari wakifika kiezi 5 tu unauza kwa 10000 lakini ukiwaacha hadi miezi 8 jogoo ni wakubwa sana na wanauzwa 15000 -20000. Unakuwa huna pressure ya kukubali bei ndogo maana hawali chakula kingi. Faida ya pili wanataga mapema kuliko wa kienyeji hivyo wanaanza kujilisha wenyewe wakiwa na miezi 6 kuendelea na vilevile waweza kuwatumia mayai yao kutotoa vifaranga aidha kwa kuwatumia tetea wa kienyeji pure au incubator na hivyo kutokuwa na haja ya kununua tena vifaranga wengine. Nitajaribu kuweka mchanganuo wa gharama na faida ingawa nikiangalia sio tofauti na iliyowekwa na RETI hapahapa. Lengo langu ni kuongeza aina nyingine ya kuku chotara ili kuwa na aina tofautitofauti, kuanza kutengeneza chakula changu mwenyewe kupitia formula nilipewa na ex SUA lecture na Dr mifugo sasaivi yuko wizarani yeye na mkewe wameitumia na waliniambia inafaa sana ingawa itabidi nipate ushauri wa mwenye mashine kiwango cha usagaji na uchanganyaji wa chakula nitaleta feedback hapa. Nawashukuru wote kwa michango yenu Mungu azidi kuwafanikisha zaidi ktk malengo yenu.
Safi sana mwanamke hapaswi kukata tamaa Kirahisi.ninaamini safari hii unamaliza mchezo nasi tutajifunza kupitia kwako.nakutakia mafanikio makubwa.
 
Hawa vifaranga WAJE kutaga wanachukuwa siku ngapi?
 
Nashukuru kwa kunitoa woga mama joe.nikiwa tayari kufuga chotara nitakutafuta kwanza ndugu yangu.
 
Naombeni msaada wenu, nina vifaranga vya kuku chotara ambavyo vina umri wa wiki 7.
Tatizo ni kwamba miguu yao inakosa nguvu, wanashndwa kutembea.
Nilimpeleka mmoja kwenye duka la dawa za mifugu, wakamchunguza na kunipatia dawa ya vitamin kwa kuwa walinieleza kuwa miili yao imeshndwa kutengeneza vitamin B plus.
Tatizo bado linaendelea japokuwa nilianza kuwapatiwa vitamin hao vifaranga wote. Nasubiri ushauri wenu wanajamvi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…