Naimani1234
Member
- Jul 19, 2013
- 52
- 6
Kubota vipi. Achia namba ya simu tupandiane hewani. Wajua... ukiliona jua jua giza laja. Funguka...
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ndo nature yao. Ila jaribu kuwapa chakula cha kuku wa nyama shida ni kwamba wanaweza wasitageJamani hawa kuku wa kienyeji wanakuwa taratibu sana
Ndg Zangu nina Kuku wangu yeye anataga mayai hadi 30 hivyo sasa nimengojea ahatamie lakini bado anaendelea kutaga hivyo nimeamua mayai kuwapa kuku wengine hivyo hii mbegu ni nzuri kweli? Ila ni kuku wakubwa sana na mayai yao ni makubwa pia.
Ndg Zangu nina Kuku wangu yeye anataga mayai hadi 30 hivyo sasa nimengojea ahatamie lakini bado anaendelea kutaga hivyo nimeamua mayai kuwapa kuku wengine hivyo hii mbegu ni nzuri kweli? Ila ni kuku wakubwa sana na mayai yao ni makubwa pia.
Utakua unaonewa wivu na yule jirani yako kwenye ile nyumba yenye dirisha la nondo!Kubota
Mama Joe
guta
Mama timmy
Hebu litazameni hili lililonipata jana baada ya Mi nikiwa Safari niliporudi nikakuta kuku mmoja mtetea amekufa ndani ya banda na hata hakuonyesha dalili yoyote na leo nikajaribu kutafuta watalaam nikakuta leo ni siku ya mapumziko na nipo nikachukua maamuzi ya kuzika.
Je? Kwenu haya yanatokeaga? Na hata nimejaribu kumpigia guta RETI na bila ya mafanikio baada ya simu zao kutopokelewa.
NAOMBENI USHAURI WENU WANDUGU!
Asanteni sana!
Una uhakika ni wa Kienyeji? usikute ni Chotara,make kiasili kuku wa kienyeji hawzi acha kuatamia, hiyo haipo so unaweza kuta ni chotara make saa zingine ni vigumu kutofautisha chotara na kieyeji kwa sababu hta mayai yao na rangi zao unakuta zinafanana
hicho kitu kimenitokea hata mimi. nafikiri inawezekana coz mimi nina kuku wa kienyeji ni kishingo,ametaga mayai zaidi ya 25 na bado anaendelea. imebidi niyaweke kwa kuku wengine wanaoatamia
Huu uzi ni zaidi ya chuo! umenihamasisha nianze ufugaji wa kuku wa kienyeji! mambo karibu yote naona yamepitiwa na wadau tena kwa vitendo na sio nadharia.kuanzia nilipouona na kufuatilia maelezo ya kwanza ya mkubwa KUBOTA ilinifanya nione kuwa tayari nimepata pa kutokea. nilitumia kama 1.5ml kujenga banda ambalo nimeanza kufuga kuku hawa wa kienyeji. ni matumaini yangu ntafanya vizuri maana nimeshaanza kuatamisha kuku na itabidi niwe mwangalifu pia kwa vifaranga. ila nawashukuru sana wote na naamini Mungu atawabariki sana.
Mkuu Pleo nashukuru kwa mrejesho wako, na maneno yako mazito yaliyosheheni baraka na kutakiana mema. Ninakuhamasisha usichoke kutafuta maarifa popote yapatikanapo ili uweze kufanikisha mambo yako. Hata mimi nawashukuru sana wachangiaji wote hapa kama ulivyoshuhudia michango yao ilivyotulia.Salaam nd. Kubota na wachangiaji wote wa uzi huu. Inabidi nikiri kujiunga JF kuufuata Uzi huu. Nikiwa kwenye utafiti wa kukabiliana na tatizo la magonjwa na chakula cha kuku wa kienyeji, nimejikuta nikidondokea kwenye uzi huu mara kadhaa, natanguliza shukrani kwa fadhila za maelezo/tafiti/changamoto na fulsa mlizopitia kufika mlipo, amini hamtupi hela ila njia ya kuipata kwa wingi.
Mbarikiwe sana, na Mungu atugawie penye manono ya nchi na umande wa mbingu wingi wa nafaka, mvinyo na kuku pawe makao yetu.
Mkuu Naimani1234 ninakubali kutembelewa karibu sana kwetu. Na safari yako ya kwanza uje wakati wa kipindi cha kulima maana hivi sasa tunavuna, ha ha haaa!!Bwana kubota. Unakubali kutembelewa. Wajua kusikia ukichanganya na kuona msmbo huwa bambam.
Mkuu Ibra6 tuko pamoja sana mimi sijakutana na swali tata kiasi cha kuhitaji uvumilivu, maswali yote jukwaa hili la ujasiliamali huwa yametulia na yakistaarabu sana, usisite kuuliza pale utakapokuwa na uhitaji, maana hapa tunarundika maarifa na uzoefu kwa pamoja toka kwa wana JF mbali mbali. Mkuu Ibra6 kuhusu suala la uuzaji kuku uliowahi kuulizia kwamba sijatoa uzoefu wangu juu ya hilo. Niseme kwamba tatizo kubwa kwenye ufugaji wa kuku wa kienyeji ni ukuzaji tu, sijapata hofu kuhusu soko la kuku hawa! Kilichoniacha hoi tu ni pale nilipoanza kuuza kuku ndiyo nilibaini kuwa kumbe watu wanajichana nyama ya kuku kuliko kawaida. Ili uweze kupata bei nzuri yakupasa ulenge misimu yenye mahitaji makubwa. Ukiwa mfugaji stadi ukafahamika huwa kuna order nyingi zinakuja kutegemea na mahali ulipo. Eneo ninalokaa kuna taasisi nyingi na ni karibu na mji wenye ofisi nyingi za serikali. Kunapokuwa na sherehe au semina au mikutano inayoendana na maakuli huwa napokea order zao kubwa. Na hapo huwa napata bei nzuri tu. Kuna watu wengine huja kununua kuku wa mbegu! Na hao ndiyo huwa hawajali bei anachotaka ni hiyo mbegu. Nilipokuwa nimefuga kuku wa Malawi ambao nilikuwa nimekerwa na udhaifu wao, alitokea mkulima tajiri aliwatamani sana na alinunua wote kama mbegu ili akawazalishe hapo nilikamua mushiko mreefu. Tatizo la soko la kuku wa kienyeji si kukosa wanunuzi bali kupata bei ndogo hasa inapotokea wewe mfugaji ndiye mwenye kufuata wanunuzi! Utafiti ulishawahi kufanywa kuangalia mienendo bei ya kuku kwa kuwahoji wafugaji sehemu mbali mbali Tz ilibainika kwamba bei nzuri hupatikana pale mnunuzi anapokuja kununua yeye, na inapokuwa mfugaji ndiye anaetaka kwenda kuuza bei huwa ni kulaliwa tu! Ufumbuzi wa hili ni kuuza wakati wa mahitaji makubwa, ni kufuga kwa malengo,unakuwa umeshapanga mwenyewe ni lini uingize mzigo sokoni ili kupata bei nzuri. Kwa hiyo Mkuu Ibra soko la kuku wa kienyeji ni kubwa. Usichanganye tatizo la soko la kuku wanalolalamikia wafugaji wa broiler, kuku broiler akifikia uzito wa kuuzwa lazima uwauze vinginevyo wakiendelea kukaa wanatafuna chakula na ndiyo wanatafuna faida, hapo ndiyo unakuta wafugaji wahaha! Hali haiko hivyo kwa ufugaji wa kuku wa kienyeji. Wachangiaji wengine wataongezea.Mkuu kubota tunajua we mfugaji practical.sio mfugaji wa thiory.wafugaji wengi ni wa hobby na thiory! Vumilia maswali
Huyu ni wa kienyeji na alishaangua watoto sita supperUna uhakika ni wa Kienyeji? usikute ni Chotara,make kiasili kuku wa kienyeji hawzi acha kuatamia, hiyo haipo so unaweza kuta ni chotara make saa zingine ni vigumu kutofautisha chotara na kieyeji kwa sababu hta mayai yao na rangi zao unakuta zinafanana
Hii mbegu niliitoa Moshi hakika ni nzuri hata kwa ukubwaMkuu Unatisha 30eggs. Mbegu ya kuku ya wapi?