Ufugaji wa Kuku wa Kienyeji na Masoko yake

Kuku wa kienyeji kama unawafuga kwa mtindo wa free range waweza kufuga wengi kulingana na ukubwa wa shamba lako,na hautingia gharama kubwa ya kuwalisha. Na ukitaka kuuza utauza taratibu bila shinikizo lolote
 
Nimehamasika sana,ninashamba kama heka kumi Nataka nifuge kuku hawa wakienyeji ntaanza na kuku majike 50 majogoo 5 ,kwa kufuata maelekezo nloyapata huku,ntatoa marejesho baada ya miezi 6.
Karibu sana mkuu, ningekushauri pia kabla ya kuanza ungefanya study tour angalau kwa mtu mmoja anayefuga tayari ukajionea kwa vitendo..

All in all, all the best
 
Karibu sana mkuu, ningekushauri pia kabla ya kuanza ungefanya study tour angalau kwa mtu mmoja anayefuga tayari ukajionea kwa vitendo..

All in all, all the best

Mwenyewe nataka kuanza kufuga mwisho wa mwaka ila ningependa kutembelea kwa waliofanikiwa
 
Karibu sana mkuu, ningekushauri pia kabla ya kuanza ungefanya study tour angalau kwa mtu mmoja anayefuga tayari ukajionea kwa vitendo..

All in all, all the best

Kiongozi asante kwa ushauri mzuri, hii kitu ninataka niifanye full time mimi mwenyewe ,nimesha watembelea jamaa kama wawili ambao wanafuga hawa kuku wakienyenji na wanafanya vizuri. Lakini mie jinsi ninavyofikiria ntakwenda hatua kadhaa mbele. Licha yakutaka kuwa boss of my own ,nina pendasana kufuga kuku .
 
Mkuu Nakusalimu,japokuwa Uzi huu ni wa Miaka Mingi na Mimi ndiyo kwanza nauona nimevutiwa sana!! Tafadhali naomba na mimi unitumie hiyo database yako!! Natanguliza
Shukrani za Dhati!!

Mkuu kama ulivyotangulia kusema japo uzi wa mda mrefu basi na mimi nitumie iyo database kama amekutumia
Natanguliza shukrani zangu kwako
 
Naitwa Fredrick SEBA, NAKAA BANANA UKONGA,
Najishughulisha na ufugaji wa kuku wa kienyeji pure, machotara na wamalawi nauza mbegu pia i mean vifaranga, kwa yeyote anayehitaji kufuga na elimu pia ya jinsi ya kuwafuga kisasa tuwasiliane kwa simu mamba 0716/63-234 201
Also press order yako ya vifaranga mapema
 
Naomba msaada , nilianza na kuku wa kinyeji 16 vifarangz na mpaka sasa niko nao 14. Ila sasa nimeona kuku 3 ambao nimeona kwenye cobz zao kuna vitu kama vidonda vyeusi, je huu ni ugonjwa gani na niutibu kivipi???
Nitashukulu kwa msaada nitakaopata
 
Naomba msaada , nilianza na kuku wa kinyeji 16 vifarangz na mpaka sasa niko nao 14. Ila sasa nimeona kuku 3 ambao nimeona kwenye cobz zao kuna vitu kama vidonda vyeusi, je huu ni ugonjwa gani na niutibu kivipi???
Nitashukulu kwa msaada nitakaopata

Sio ugonjwa ni viroboto.
Dawa yake chukua mafuta ya taa uwawekee eneo hilo navyo vitapotea mapema iwezeksnavyo.
 
Asante I will do that kesho, nz kuna dr mmoja nilimuulizia akaniambia ninunua dawa niwawekee kwenye maji ila siku amini maoni yake
 
Sio ugonjwa ni viroboto.
Dawa yake chukua mafuta ya taa uwawekee eneo hilo navyo vitapotea mapema iwezeksnavyo.

mbona nmejarbu kwenye kuku wangu havkupotea kwa mara moja na mpk nkaamua nkawanunulie dawa lkn bado cjaona maendeleo yeyote na leo n cku ya4
 
Karibu sana mkuu, ningekushauri pia kabla ya kuanza ungefanya study tour angalau kwa mtu mmoja anayefuga tayari ukajionea kwa vitendo..

All in all, all the best

Naomba ufafanuzi nduguzanguni ,Je kuku akichanjwa ndiu kwa mara ya pili kuna tatizo? Nauliza hili swali kwasababu nimenunua kuku wa mbegu mitetea na majogoo kutoka kwa wakulima wenzangu sasa sina uhakika kama walipewa hii chanjo muhimu ya ndui. Je ni vema niwachanje wote tena?
 
Wadau naombeni tofauti kati ya Broiler starter na Starter Mash kwani nilienda duka la mifugo nikihitaji chakula cha vifaranga wa kienyeji wa siku moja wakanipa mfuko ulioandikwa Broiler Starter nimeutumia sasa vifaranga vyangu vina wiki ya 4 hakuna aliyekufa (vifaranga 63 )ila leo kuna mmoja anatambaa kama anashindwa kusimama halafu ni mzito. Nipeni ushauri.
 
asante mkuu. pia ueleze utunzaji na chakula
Vifaranga hao nimewatotolesha kwa kwakutumia kuku wa kienyeji saba kwa kuwapa mayai 10 kila moja na kupata vifaranga hao 63 walioanguliwa kwa siku moja. Kwa kuwa nipo kijijini hakuna umeme na kutumia taa ya mafuta ni gharama nimewaachia kuku watano wanalea hao vifaranga katika banda lao na baada wiki 8 nategemea kuwaachanisha na hao kuku.Nimewachanja mdondo na ndui,pia nawapatia Vitamini ya dukani inayoitwa PHARMAXINE CHICK PLUS katika maji ya kunywa hasa siki hali ya hewa ni ya baridi, kuhusu chakula nawapa Broilers Starter kwa kiasi cha kikombe cha chai kwa vifaranga kumi asubuhi na mchana nawapa chengachenga ya mahindi nachanganya na wadudu fulani kama siafu walichangayika na dagaa wanaouzwa sokoni kilo Tsh 1200/= kwa kipimo cha kikombe kimoja cha chai cha wadudu hao kwa vikombe 4 vya chenga na nawapa wastani wa kikombe 1 kwa vifaranga 10. nawapati mchicha mara tatu kwa wiki kwani wakati huu wa kiangazi ni shida kupata majani mabichi ya kutosha.
 
naombeni ushauri nini kuku wangu ametaga siku 5 mfululizo siku ya 6 na ya 7 hakutaga akaja kutaga siku ya 9 kwahyo ndan ya siku 9 kataga mayai 6 na mpk leo siku ya 15 hajataga wala kuyaatamia,je hii inatokana na nini?
 
Mm naomba ushauri ,nimenunua kuku wa mayai 26 size ya miezi mitatu cha kushangaza nimewaweka ktk chumba ambacho muna godoro ukutani leo nimeamka wamelitoboatoboa wanakula je hakuna madhara yeyote?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…