Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mm naomba ushauri ,nimenunua kuku wa mayai 26 size ya miezi mitatu cha kushangaza nimewaweka ktk chumba ambacho muna godoro ukutani leo nimeamka wamelitoboatoboa wanakula je hakuna madhara yeyote?
Asante Mkuu kwa mchanganuo huu, Je wewe umeshaanza kufuga au unaelezea nadharia? Katika uwekezaji au biashara yeyote kuna changamoto zake, kwa hiyo usijekuingia katika uwekezaji au biashara kwa mahesabu haya; mambo yakienda tofauti unaweza kukata tamaa. Unaweza kuona ufugaji wa kuku wa kienyeji ni rahisi, lakini siyo rahisi kama wengi wamavyofikiria (kwa uzoefu wangu). Nami nilikuwa na mahesabu kama haya nikanunua kuku zaidi ya 35, lakini zilianza changamoto za magonjwa na walibaki wachache sana. Unaweza kusema tumia dawa. Kwa sasa kuku wa kienyeji nimeweka kwa ajili ya matumizi binafsi lakini kwa biashara niliamua kufuga kuku wa nyama (broiler). Nimetoa comment kutokana na uzoefu niliopata lakini wengine wanaweza kuwa na uzoefu wa tofauti na michango zaidi inaweza kutolewa.
je juna mtu anjua kuhusu kuku aina ya KROIRER? ni high bread ya local chicken and muzungu wametoka kenya,
nimeamua kuanza na kuku 10 tu, na kesho ndo nawapokea na maandalizi yako kwenye gear no 5, na haya yote ni juu ya kusoma saaana huu mtandao wa ujasiriamali ndani ya jamii forum, nimeamua kuyavulia woga maji na kujitumbukiza mzimamzima
its ssaid that FAILURE IS PART OF SUCCESS
Umesema vema mkuu, WaTz tumekuwa watu wa porojo na mabishano ya kisiasa yasiyo hata na tija ktk maisha yetu ya kila siku. Ukienda JUKWAA LA SIASA utakuta ni Chadema na CCM tu! Comments za kizushi hadi inachefua, kisa anatetea chama chake. Huku hata mm naona kwanifaa atiii...Mimi jukwaa la siasa halina faida kwangu.,napenda sana hili jukwaa wa wajasiriamali,bsness &econmy.
I like it,yani mtu unapat vitu vya kukukomboa,afu hili jukwaa watu wapo serious na kazi,halina waropokaji na wazozaji kama kuuule politics forum.
nami najipanga ili niingie kwenye hii biashara kichwa kichwa nimeshachoka kutumwa.Nakushauri ufuge wa kisasa - Layers. wa kienyeji it takes time na faida si kubwa vile unavyodhani - nitafute nikupe ushauri wa bure - meanwhile angalia kazi hii hapa
![]()
Hawa wako 900, wanatoa Tray 24 kila siku kila Tray 5000- Chakula chao ni kilo 125 approx Tshs 55,000/-
Mtaji wa kuanzia unahitaji kuwa na not less than 6m before you start production. Kama unataka mchakato mzima sema nitakutumia database yangu.
karibu mkuu soko lipo, unatoka nao wapi, lini umewachanja Kideri/mdondo? Kuna wadau wamekuwa wakiulizia hata hapa JF sana hawa kuku hivyo sio lazima ummuzie mmoja wote ila tupo tunaotaka 20, 50 nk. Jieleza majogoo wangapi na tetea wangapi na bei ya jumla shilingi na utawafikishia wapi kwa hapa Dar tukutafute, cc faiz jr, wazo languHabari ya majukumu wakuu! Wandugu nilikuwa naomba kujuzwa kuhusu masoko ya kuku wa kienyeji hapa Dar, nahitaji kuwauza kuku kuanzia 100
karibu mkuu soko lipo, unatoka nao wapi, lini umewachanja Kideri/mdondo? Kuna wadau wamekuwa wakiulizia hata hapa JF sana hawa kuku hivyo sio lazima ummuzie mmoja wote ila tupo tunaotaka 20, 50 nk. Jieleza majogoo wangapi na tetea wangapi na bei ya jumla shilingi na utawafikishia wapi kwa hapa Dar tukutafute, cc faizajr, wazo langu
ni kweli watu tunakimbia kuku wanaouzwa masokoni sababu mtu akiona wagonjwa anaamua kuuza. Pia wengi hawapatiwi chanjo ikitokea wamesafirishwa toka mbali wanafika wanaanza kuumwa aidha kudhoofu na hali ya hewa au kuambukizwa njiani. Tunategemea hapa JF itakuwa gulio la wasomi kutokana na darasa zinazotolewa hapa na kupigiwa mfano.'kweli kabisa maelezo yake hayajitoshelezi hata kidogo kwa kweli...'
Habari ya majukumu wakuu! Wandugu nilikuwa naomba kujuzwa kuhusu masoko ya kuku wa kienyeji hapa Dar, nahitaji kuwauza kuku kuanzia 100
Soko ni kubwa sana wewe tu
karibu mkuu soko lipo, unatoka nao wapi, lini umewachanja Kideri/mdondo? Kuna wadau wamekuwa wakiulizia hata hapa JF sana hawa kuku hivyo sio lazima ummuzie mmoja wote ila tupo tunaotaka 20, 50 nk. Jieleza majogoo wangapi na tetea wangapi na bei ya jumla shilingi na utawafikishia wapi kwa hapa Dar tukutafute, cc faiz jr, wazo langu
Huyu mdau analeta masikhara kwenye siriasi issue. Mbona haji kujibu maswali ya wadau.