Ufugaji wa Kuku wa Kienyeji na Masoko yake

Mkuu ulishawafuga hawa wa kienyeji?
Baadhi ya wafugaji huwa wanawafagilia sana, ila nikipiga hesabu ya chakula/muda wanaokaa nahisi ni hasara kibiashara.
Vipi kuhusu chotara?

kuku wa kienyeji hawana faida nzuri,jaribu kuku wa nyama au mayai
 
kuna uzi mmoja wa jamaa mmoja anaitwa kubota kama sikosei unaitwa zijue mbinu zangu ufugaji wa kuku wa kienyeji. kuna kila kitu mule. sidhani kama ukiusoma ule uzi utakuwa na swali. best wishes
 
Ndo mara yangu ya kwanza kusoma uzi huu ila kwa hapo red naomba nijibu; mimi binafsi tangu nimeanza kufuga vifaranga nawapatia chakula cha kutengeneza mwenyewe na wanakua japo sio wote. Nikiwaachia kutembea wanashambuliwa na maadui.
 
naombeni ushauri nini kuku wangu ametaga siku 5 mfululizo siku ya 6 na ya 7 hakutaga akaja kutaga siku ya 9 kwahyo ndan ya siku 9 kataga mayai 6 na mpk leo siku ya 15 hajataga wala kuyaatamia,je hii inatokana na nini?

chakula anachopewa hakina virutubisho vya kutosha; na hasahasa angalia anaweza akawa anakosa calcium kwa ajili ya kutengeneza shell la yai; mpatie unga wa konokono.
 
Haya ni moja kati ya mazuri ya mapinduzi ya teknolojia, natamani wadogo zangu wa sekondari na vyuo vikuu wangekuwa wanatumia mitandao ya kijamii positively kama uzi huu na mingine kama hii. Bravo jf, bravo wadau wote.

nipo mkuu... nafuatilia kwa makini sana na naamin siko peke yangu...
 
woooote mmetoka kwenye hoja ya mtoa mada mmengangania email ya mvua. dah!woote mmekuwa mabroila?
 
Ifikapo mwezi Jan 2013 nitaweka hesabu za wazi na mchanganuo mzima wa ufugaji wa kuku wa kienyeji unavyolipa + changamoto zilizopo.

Mkuu Tutor B japokuwa uliandika 2013 nadhani ulikuwa na maana ya 2014. Nakukumbusha tu kwa upole, Jan 2014 ndio hii. Nitashukuru kupata mchanganuo ili niongeze darasa.
Asante kwa mwanzisha mada na wote waliochangia uzi huu kwa kutuelimisha.
 
Last edited by a moderator:

ahsante,,nimeikopy hakika naenda ku-print nakuifanyia kazi.
 

Ushauri mzuri, shukrani.
 
Habari za saa hizi wapendwa, nahitaji kujuwa jinsi ya kufuga kuku wa kienyeji na kuwafanya watage mayai kila siku
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…