Ningependa kuuliza juu ya chakula, je, hawa nao wanalishwa chakula sawa na kile cha kuku wa kizungu?
Ili kuku wawe na afya nzuri, ukuaji nzuri na kutoa mazao mengi na bora wanahitaji vyakula aina ya Wanga, protini, madini, vitamin na maji.
KUMBUKA
-Ukosefu wa vitamini A hujitokeza baada ya kiangazi kirefu
-Macho ya kuku huharibika
-Ugonjwa unakuwa mgumu kutibika dalili za wazi zikionekana
-Husababisha vifo hasa kwa kuku wanaokua.
-WAPE MAJANI MABICHI WAKATI WA KIANGAZI
-VITAMINI ZA KUKU ZA MADUKANI HUFAA KWA KINGA YA KUKU WENGI
MCHANGANYIKO WA VYAKULA WENYE ASILI ZIFUATAZO UNAFAA KWA KULISHA KUKU.
1.Mizizi - Mihogo, viazi vitamu, mbatata, magimbi n.k
2.Nafaka- Mahindi, mtama, mpunga, ulezi, pumba za nafaka n.k
3.Mboga- Jamii mbali mbali ya majani kama vile kunde,mboga za majani, nyanya, kisamvu n.k
4.Matunda- mapapai, maembe n.k
5.Mbegu za mafuta- karanga , ufuta, mashudu ya pamba, alizeti, machicha ya nazi n.k
6.Wadudu mbalimbali.
7.Maji
Vyakula nilivyotaja hapo juu hupatikana kwa wingi zaidi wakati wa mvua na mavuno, mara baada ya kipindi hicho kunakuwepo na upungufu mkubwa sana ambao unachangia ukuaji taratibu na utagaji hafifu.
Utafiti unaonyesha kuwa kiasi cha chakula wanachojitafutia wenyewe huwa hakiwatoshi. Inakadiriwa kuwa wakati wa mavuno kuku anaweza kuku anaweza kujitafutia asilimia 50 - 70 ya chakula na wakati wa kiangazi asilimia 30- 50 tu ya mahitaji yake ya chakula. Kwa kawaida kuku wa kienyeji hutumia zaidi ya 90% ya masaa ya siku katika umbali wa mita 110 hadi 175 ili kujitafutia chakula, kuku aliyepevuka anayefugwa huria anahitaji gramu 80 za chakula cha ziada kwa siku.
Hivyo ili kuku waweze kuzalisha wafikie uwezo wao ni muhimu wapewe chakula cha ziada. Chakula cha ziada mara nyingi hutokana na vyakula vinavyopatikana kwa urahisi katika mazingira aliyopo mfugaji. Nakuomba ufuatilie zaidi kwa mtaalamu wa mifugo aliye karibu nawe ili upate mbinu zaidi za namna ya kuandaa chakula cha kuku.
Kuhusu kuku wa kisasa sina uzoefu nao.