Ufugaji wa Kuku wa Kienyeji na Masoko yake

Wenye uvimbe kama sio vidonda wapake mafuta ya kula, ila wengine huwaosha na kuwapaka iodine. Kila la heri
Nilishawatenga na kanga muda mrefu maana mayai yalikuwa hayakai Mama Joe. Nitajaribu kwenda famasi nikapate ushauri pia. Hawa wengine wako safi kabisa. Asante sana .
 
Jamani asanteni sana sana kwa uzi huu, nimejifunza mengi sana, nimesoma uzi huu kwa muda wa siku 3 mfululizo jana nilikaa mpk kichwa kikaniuma, nimejifunza mengi sana juu ya ufugaji wa kuku, nami ni mfugaji humu ndani ndiko kulinihamasisha bila kutafakari marambilimbili nikaamua kufuga, na kwwakweli nawapenda sana kuku.
Mungu awabariki wote kwa michango yenu yenye manufaa, big up san a@Kubota muanzisha thread, hujui tu ni kwa kiasi gani umeinsipire watu wengi kuwa wafugaji na kwanamna hiyo umeokoa au umepandisha maisha ya watu wengi sana, Mungu akubariki kiasi cha kuiminwa na kusukwasukwa!
Niwashukuru pia Mama Joe, Mama Timmy, Chasha, asigwa, Liverpool fc na wengineo wote kwa michango yao bora.
JF is the right place to be! Sijajutua na wala sitajuta.

By ze way Kubota hivi tanuri moja la mkaa linatoa magunia mangapi ya mkaa? Nina shamba langu bagamoyo nataka kusafisha nikaona miti ile nichome mkaa.
 
Last edited by a moderator:
Gazeti,ainisha matumizi ya ya taba asilia ktk kutibu magonjwa ya kuku. eg. Mronge unatibu nini ktk kuku na jinsi ya kuandaa tiba na dose yake ikoje,kwani itampunguzia mfugaji gharama za madawa
 

Nimeumwa na kichwa ghafla....umaskini ni kujitakia tu...heko sana mkuu....
 
Gazeti,ainisha matumizi ya ya taba asilia ktk kutibu magonjwa ya kuku. eg. Mronge unatibu nini ktk kuku na jinsi ya kuandaa tiba na dose yake ikoje,kwani itampunguzia mfugaji gharama za madawa

Gazeti. tunaomba mwongozo wa kuzitengeneza na matumizi
 
Wenye uvimbe kama sio vidonda wapake mafuta ya kula, ila wengine huwaosha na kuwapaka iodine. Kila la heri

Mama Joe na wafugaji wote, tafadhali mnisaidie kuku wangu 2 wanataga wakimaliza wanatoka kizazi dawa gani nitumie .?
 
Last edited by a moderator:
habari zenu wana jamii forum, nimesoma kwa makini sana makala ya ufugaji kuku wa kienyeji nimependa sana, nimependa jinsi watu wanavyotoa maujuzi katika kufuga kuku, nimewapenda bure. mubarikiwe


mama Carol
 
Shughuli hii nategemea kuifanyia Dar es salaam, nina eneo la kutosha ambalo nataraji kujenga Mabanda. Naomba ushauri kati ya Kuku wa Mayai na kuku wa kienyeji ni wepi wanaolipa kibiashara.
 
Mimi nafuga wote na wote wanafaida ila inatege.ea na capital..kama unauwezo fuga wa mayai kwani income yao ni endelevu ila kama hautaki kuinvest kwa muda mrefu as in 5 months then fuga wa nyama ambao utakua unawatoa kila wiki 5
 
Pia kati ya hawa wa mayai na kienyeji bora wa kienyeji kwasababu hizi..
1.Wastahimilivu wa magonjwa
2.Hawachagui sana chakula
3.Hawana masharti sana ya ufugaji
4.Pia muda wao wa kutaga ni sawa na hao wa mayai
5.mayai bei nzuri na yana market sana
 
Pia kati ya hawa wa mayai na kienyeji bora wa kienyeji ....

kuku wa kienyeji wataweza nipatia faida iwapo nawafuga katika mazingira ambayo hawawezi kujitafutia chakula cha ziada?
 
Ndio...kwani hata utengenezaji wao sio strict sana kwenye components kama wa mayai wa kisasa..hao ukikosea tu mixture balaa.Ukiweza mix wa kienyeji pure na chotara
 
habari zenu wana jamii forum, nimesoma kwa makini sana makala ya ufugaji kuku wa kienyeji nimependa sana, nimependa jinsi watu wanavyotoa maujuzi katika kufuga kuku, nimewapenda bure. mubarikiwe


mama Carol



Karibu sana ......................
 
Wataalamu mnaonekana kama kupotea sana tuleteni marejesho ya ufugaji kuku.....mimi kupitia uzi huu sasa nimekuwa mfugaji na nimeanza kupata matunda ya ufugaji kwani nina kuku mia moja toka nianze na kuku nane! Hapa utaalam sasa umefika mwisho hakika ufugaji ni mkombozi kama utazingatiwa na wafugaji
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…