Ufugaji wa Kuku wa Kienyeji na Masoko yake

Nakushukuru sana kwa Mchango wako, Baada ya kusoma maelezo yako nafikiri Nitajishughulisha na ufugaji wa kuku wa kienyeji, ufugaji wangu utakuwa wa ndani ya banda

SWALI
wale kuku Machotara wanauwezo wa kuhatamia na kutotoa mayai?

Kuna mtu nimeona alipost hapa JF kuwa ana kuku aina ya MALAY ni kuku wa kienyeji ila asiliyao ni kutoka Malaysia. Hebu jaribu kutafuta post yake kama utaweza mtafute usikie kutoka kwake.
Angalia hii link
https://www.jamiiforums.com/ujasiriamali/616728-habari-njema-kwa-wajasiriamali-na-wafugaji.html
 
Malila najua tu kuku aitwa chotara ila aina gani ndo sijui na wana bei gani,so nipenipe kiongozi nijue nafenyeje nipe contants pia nataka niwafugie Kifuru asee
 
Last edited by a moderator:
elnino tupatie pia tuangaze na uko
na hongera sana kiongozi kazi nzuri sana iyo
 
Last edited by a moderator:
Mi naona kwa kuanzia hawa wa kienyeji ni bora zaidi,wastahimilivu na si wa kuchagua chakula.Tofauti na wengineo lazima uwe na mtaji mkubwa kidogo.
Halafu hawa ndo watakaokuwezesha kufuga hao wa mayai au wa nyama kwani mayai yao tu kwa bei ni mara 2 ya wale wa mayai/ layers.Na ukiwalisha vizuri wanataga vizuri sana na interval ya kutaga kwa kuku mmoja inakuwa ni ya muda mfupi tu.
Anza na kuku wa kienyeji kama mtaji wa kawaida.
 
Ndugu zangu kuna kuku wanaitwa silkies je kuna mtu anao...hawa wananyama nyeusi
 
Nitawapataje hao Chotara?
 
Oh karibu sana mkuu, umehamia mbugani tena lololooo miti na wanyama watakuwa salama??? Joking kwakweli ulipotea sana, sisi tunamshukuru Mungu tunaendelea na ufugaji mchanganyiko kulingana na soko si unajua tena "the law of demand and supply", Hongera kwa chotara nasi tuko nao pia. Wadau wengine wa kijiwe naona walisusa ila watarudi hapa kuna wengine wapya wanachangamoto mbalimbali tulijaribu kushauriana hapa. Karibuni na siku njema
 
habari zenu wana jamii forums, ivi ugonjwa wa ndui kuku anakuwa anaharisha nyeupe? au nao ni ugonjwa mwingine tena? huo wa kuharisha nyeupe kama njano mpauko.


asanteni,
 
Asante Zipuwawa, yaani nilikua nikijaribu siku nyingi kujoin nikawa nashindwa sasa nimeweza nimejisikia raha sana, maana nitakua na share na wafugaji wenzangu, Zipuwawa uko pande zipi wewe? mimi niko arusha.
 
natamani cku moja kila mmoja atoe historia au aelezee jinsi anavyopambana na ufugaji wa kuku maana itakuwa inamfundisha na kumpa changamoto mwingine, yaan mfano nilianza na kuku kadhaaa, sasa nina kuku kadhaa, na nimepitia changamoto kadhaaa, yaan kama kubota alivyotoa mauzoefu yake.

Asanteni, nawapenda wote.
 
Malila alisema ana contacts za mtu ana kuku chotara,namsubiri kweli anambie
 
Last edited by a moderator:
Asante Zipuwawa, yaani nilikua nikijaribu siku nyingi kujoin nikawa nashindwa sasa nimeweza nimejisikia raha sana, maana nitakua na share na wafugaji wenzangu, Zipuwawa uko pande zipi wewe? mimi niko arusha.

Mi nipo Morogoro ndg yagu napambana nashukuru kwakweli hata mimi natamani niungane na watu mbalimbali kwaajili ya kubadilishana ujuzi na mbegu pia........karibu Mama Carol
 
Shaka Ondoa
 
Kawatafutie kuku chanjo inauzwa 6000 tu,kidonge kiimoja kwa kuku 1000 wala hawawezi kuugua kamwe,
 
Hakika nimeusoma huu uzi toka page ya kwanza mpaka mwisho,nimehamasika sana.Ila mimi nimemaliza shahada ya kwanza ya sayansi ya chakula na teknolojia kutoka SUA,mi nataka nianzishe ufugaji wa kuku wa kienyeji. Mimi ni mwenyeji wa Bariadi,lakini malengo yangu zaidi ni kupata mtaji na kuanzisha factory ndogo ya usindikaji wa nyama ya jamii ya kuku.Nawapenda sana vijana wenzangu nawaombeni msada wa kimawazo na utaalamu kwa mawazo yangu ya usindikaji wa nyama ya jamii ya kuku,ahsanteni sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…