Ufugaji wa Kuku wa Kienyeji na Masoko yake

Ufugaji wa Kuku wa Kienyeji na Masoko yake

Ufugaji wa kuku wa kienyeji unaweza kuimarika kupitia uzalishaji na utunzaji sahihi

Wafugaji wengi wa Tanzania wanafuga kuku wa kienyeji. Ndege hawa kwa kawaida wanafugwa sehemu za vijijini ambapo wanaachiwa huru kuzurura.

Kuna uwezekano mkubwa sana wa kizazi kujirudia kwa kuwa jogoo anaweza kumpanda mtetea ambaye alitokana naye, au kumpanda mtetea ambaye wamezaliwa pamoja. Kuzaliana kwa namna hiyo kunasababisha matatizo makubwa, ikiwa ni pamoja na kudumaa, kupunguza uzalishaji wa mayai, kuwa na vifaranga dhaifu ambavyo ni rahisi kushambuliwa na magonjwa, na mengineyo mengi yasiyokuwa ya kawaida. Ufugaji huru ambao una udhibiti ni muhimu sana ili kuepuka kizazi kujirudia. Kuku wanaweza kuwekwa kwenye makundi na kuachiwa kwa makundi ili kuzuia uwezekano wa kuzaliana kwa kizazi kimoja.

Mfugaji anayetaka kufanikiwa katika ufugaji wa kuku wa kienyeji ni lazima achanganye mbinu za kienyeji na za kisasa. Hii inajumuisha njia zifuatazo:

Kuchagua aina ya mbegu

Kuchagua mbegu inamaanisha: Mtetea au jogoo mwenye ubora wa hali ya juu , akiwa na sifa kama uzalishaji wa juu wa mayai au uzalishaji wa nyama, wanachanganywa na aina mfugaji alionayo, au kuboresha mbegu ambayo ni dhaifu. Kuna makundi matatu ya aina za kuku;

• Kuku wenye umbo dogo ni wazuri zaidi kwa uzalishaji wa mayai.
• Kuku wenye umbo kubwa ni wazuri zaidi kwa uzalishaji wa nyama.
• Mbegu iliyochanganywa ni nzuri kwa uzalishaji wa mayai na nyama.

Endapo mfugaji anataka kufuga kuku kwa ajili ya mayai, basi anaweza kuchanganya mbegu ya kienyeji aliyonayo na mbegu yenye umbo dogo ambao wana historia nzuri ya uzalishaji wa mayai, na kama anataka kuzalisha kwa ajili ya nyama, basi anaweza kuchagua wenye umbo kubwa. Na ambae anahitaji kwa ajili ya mayai na nyama, basi anaweza kuchanganya mbegu.

Chagua mbegu kwa umakini

Wafugaji wenye uzoefu huchanganya mbegu tofauti ambazo zina ubora na sifa maalumu, kama vile uwezo wa kukabiliana na magonjwa, ukubwa wa mayai, umbo, na kiasi cha chakula wanachohitaji.

Vigezo vifuatavyo vinaruhusu uchaguzi sahihi:

1. Mtetea au jogoo kati ya kilo 1 mpaka 2, anahesabiwa kuwa kwenye kundi la umbo dogo.
2. Kuku wote wenye uzito wa kilo 3 au zaidi wanahesabiwa kwenye umbo kubwa.

Kuku wenye kilo 2 mpaka 3 wanahesabiwa kuwa mbegu mchanganyiko (Chotara).

Uzalishaji mzuri wa kuku ni pamoja na kuhakikisha kuwa, kila baada ya mzunguko mmoja, jogoo anabadilishwa, au kuku wote pamoja na mayai yake wanauzwa na kuleta aina nyingine ili kuzuia kizazi kujirudia. Ruhusu jogoo mmoja kuhudumia kuku 10 tu. Mfugaji pia anaweza kuzuia uwezekano wa kizazi kujirudia kwa kuweka kumbukumbu rahisi, kwa mfano, unaweza kuweka viota na kufahamu ni kuku yupi yupo kwenye kiota kipi na kwa muda upi.

Kumbukumbu ni muhimu

Uwekaji wa kumbukumbu ni lazima! Kumbukumbu humsaidia mfugaji kufahamu kizazi na tabia za kila kuku ambaye amechaguliwa kwa ajili ya uzalishaji, kiasi kwamba anaweza kuelezea kuhusu kila kuku aliye naye bandani, kwa kuzingatia uzalishaji wa mayai na nyama.

Emmanefarms tumejipanga kuhakikisha unapata mbegu bora kwa kufanya kwa vitendo ufugaji wa kisasa kibiashara,tunatotolesha na kuuza vifaranga vya kienyeji chotara kwa bei ya shilingi 2,000, pia tunauza mayai kwa bei ya shilingi 12,000 kwa tray,tunapatikana mbezi louis,tupigie,tuma sms au WhatApp 0657666740.
 
Mkuu Kubota kwanza nashukuru sana kwa kunipa maujanja ya ufugaji wa kuku wa kienyeji.
Leo naomba nami niongezee kitu hasa kwenye dawa za kuku wa kienyeji.ni cku nyingi sana nimefuatilia dawa ya alovera nimegundua ni dawa sahihi ila alovera iliyonipa mafanikio siyo ile chungu la ni ile isiyo chungu mara nyingi iinapatikana porini.nimeijaribu mara nyingi kwa kuku wagonjwa imenipa mafanikio naombeni nanyi muijaribu. Nami baada ya kugundua nimepanda kwa hom.Picha yake hii hapa chini.
 

Attachments

  • 1475915036773.jpg
    1475915036773.jpg
    53.6 KB · Views: 156
  • 1475915059692.jpg
    1475915059692.jpg
    50 KB · Views: 133
Mkuu Kubota kwanza nashukuru sana kwa kunipa maujanja ya ufugaji wa kuku wa kienyeji.
Leo naomba nami niongezee kitu hasa kwenye dawa za kuku wa kienyeji.ni cku nyingi sana nimefuatilia dawa ya alovera nimegundua ni dawa sahihi ila alovera iliyonipa mafanikio siyo ile chungu la ni ile isiyo chungu mara nyingi iinapatikana porini.nimeijaribu mara nyingi kwa kuku wagonjwa imenipa mafanikio naombeni nanyi muijaribu. Nami baada ya kugundua nimepanda kwa hom.Picha yake hii hapa chini.
Alovera hii inapatikana wp mkuu?
 
Mhh! Wakuu Mama Joe na Chasha huu ukarimu wa kudumbukiza hizi documents hapa you make me crazy!! Mungu awabariki kwa ukarimu huu ambao mitaani ni adimu isipokuwa JF pekee!
thanx, watu kama nyie Mama Joe MUNGU awabarik
 
Nakushauri ufuge wa kisasa - Layers. wa kienyeji it takes time na faida si kubwa vile unavyodhani - nitafute nikupe ushauri wa bure - meanwhile angalia kazi hii hapa

attachment.php


Hawa wako 900, wanatoa Tray 24 kila siku kila Tray 5000- Chakula chao ni kilo 125 approx Tshs 55,000/-

Mtaji wa kuanzia unahitaji kuwa na not less than 6m before you start production. Kama unataka mchakato mzima sema nitakutumia database yangu.
Mi ndio Niko kwenye process ya kujenga banda,unaweza nisaidia hiyo data base mkuu? Namba yangu ni + 1 616 334 3260,Niko whatsaap masaa 24
 
Back
Top Bottom