Ufugaji wa Kuku wa Kienyeji na Masoko yake

Ufugaji wa Kuku wa Kienyeji na Masoko yake

Source: ufugaji Wa kwenye makaratasi n rahisi sana,

Ingia uone mziki wakeKuwa tajiri kwa mtaji wa laki 2 na Nusu tu kupitia ufugaji wa kuku wa kienyeji. Tazama Hapa


Mpendwa msomaji wetu, yawezekana umekuwa ukiwaza sana nini ufanye ili uweze kufanikiwa na kuondokana na adha za umaskini. Kulalamika tu vyuma vimekaza haitakusaidia kitu kama hutaki kujiongeza ili uongeze kipato chako.

Yako mambo mengi ya kufanya ili kujikwamua kiuchumi. Usitegemee mshahara wako tu. Mimi nataka kukufungua macho kwa jambo moja tu tena kwa uchache. Jambo hili anaweza kulifanya mwenye mtaji mkubwa au mdogo.

Somo ni dogo tu lakini naamini wapo watakaopata mafanikio makubwa sana.
Unaweza kuanza kwa mtaji wa Mil.1 mpaka laki tano au hata chini ya hapo.

Mfano. Unaweza kutumia Tsh 250,000 kununua kuku 25 kwa bei ya Tsh 10,000 kwa kuku mmoja (kadirio la juu) Majogoo watakuwa 5 kwa uwiano wa 1:4.

Hii ina maana kuwa wakishaanza kutaga utakuwa na vifaranga 20 x 10 = 200 Watunze vizuri. Wale vifaranga tunakadiria kuwa majike watakuwa 150 ambao ndani ya miezi 3 au zaidi nao wataanza kutaga.

Utakuwa na kuku 200 + 25( ulioanza nao) =225 ndani ya miezi 6. Miezi 6 inayofuata 225 - (majogoo 55) = 170 Hii ina maana kuwa 170 x 10= 1,700.

Ndugu msomaji, hayo niliyotoa ni makadirio ya chini sana hivyo mpaka mwisho wa mwaka utakuwa na kuku zaidi ya 2000.

Mwaka utakaofuata utakuwa na kuku wangapi baada ya kuuza kuku baadhi ili upate fedha ya kuwalisha ????

Ukiuza kuku 1000, utabaki na kuku 1000, kati yao tuseme majike ni 750. Ndani ya Miaka 2 maanake ni 750(majike) x 10 = kuku 7500 (uza wengine upate pesa ya kutumia kuwalisha) .

Tuseme sasa utabakiwa na kuku jike 3000 x 10( jike moja ni mayai 10) = kuku 30,000.

Hao kuku 30,000 ukiwauza wote utapata; 30,000x 13000( bei ya kawaida kbsa)= 390,000,000. Je, bado utakuwa masikini? Bado vyuma vitakuwa vimekaza?

Nina uhakika, mpaka mwisho wa mwaka huo wa pili utakuwa umefanikiwa sana kuukimbia UMASIKINI.

Kwenye hayo mamilioni, hata ukitoa milioni 100 kwamba tuseme ndo zimetuka kuendeshea mradi wako, bado utakuwa ni milionea tu. Kumbuka huu ni mwongozo tu, fanya utafiti na ufuatilie zaidi.

NB: Ukiyapata hayo mamilioni ya pesa, kumbuka kutoa Zaka, sadaka na kusaidia masikini wasiojiweza ili ubarikiwe zaidi
 
alafu unasema haujawai kubeti
Mbona hata 1000 (buku) unatajirika? Ingia sokoni majira ya jioni au alfajiri bei ya bidhaa iko chini.

DAY1
Nunua Tikiti zima la 1000 ( buku), nenda sehemu yenye uhitaji katakata pata vipande 5. Jero isevu.

500× 5= 2500

DAY2
Nunua matikiti 2 kwa 2000 na mia tano itumie tu.

Katakata tena safari hii utakuwa na vipande 10.

500× 10 = Sh. 5000

DAY3
Nenda nunua tikiti 5.

Hapa kila tikiti 1 vipande 5 ×5 = 25
500×25 =7,500

DAY 4
Tikiti 8 kwa nikimaanisha 7500 + 500 uliyosevu DAY1 = 8000.

This time tikiti 8 utapata vipande 40
40 × 500 = 20,000

DAY 5
Tikiti 20
Utapata vipande 100

100×500= 50,000

DAY6
Tikiti 50
Utapata vipande 5 × tikiti 50= 250
Vipande 250 × 500 = 75,000

DAY 7
Nenda kachukue tikiti 75 na fungua kijiwe kingine weka kijana afanye internship.

Hapo utakuwa na vipande 375 ukiuza kwa bei yetu 500 unapata Sh. 187500/=

Wiki inayofuata kuwa constant tu kwamba

Kila siku unachukua tikiti 100 za bukubuku kwa Sh. 100,000. Ile 87,500 isevu.

Tikiti 100 kwa wastani wetu wa kila tikiti moja vipande 5 na unauza kwa 500.

Kila siku utakuwa unauza vipande 500 unapata Sh. 250,000/=.

250,000 × siku 30 (mwezi1) = 7,500,000

7,500,000 × mara miezi 12= 90,000,000

Kipato chako kwa mwaka kitakuwa Sh. 90,000,0000.

Huna mtaji wa 1000 (Buku!) Unasubiri nini kuanza.
 
Huo ni ufugaji wa mtandaoni, wa kimakadirio ambao ni rahisi sana kuliko ufugaji halisi.

Kuku wanahitaji nafasi, banda chakula, virutubisho, chanjo(dawa) n.k

Pitia tena mchanganuo wako una mapungufu ya kiuhalisia.
 
Huo ni ufugaji wa mtandaoni, wa kimakadirio ambao ni rahisi sana kuliko ufugaji halisi.

Kuku wanahitaji nafasi, banda chakula, virutubisho, chanjo(dawa) n.k

Pitia tena mchanganuo wako una mapungufu ya kiuhalisia.
Mkuu hii sishauri mtu aifuate maana ataumia sana kama anategenea kuku haohao, binafsi nilitenga laki 4 nikanunua kuku wa miezi 2 kwa shs 3500 kijijini walikuwa kama 23 hivi, nikajipanga chakula kizuri plus,chanjo zote maana banda lilikuwepo.

kuku walikufa wengine kwamagonjwa ambayo umewapa chanjo wakabaki 15 hivi ndo walivuka salama wakawa wakubwa wote tetea nikanunua jogoo 1 kwa 15.

hapo kuna vifaranga kufa kutokana na sababu fulani kuna kuku kutolalia vizuri unakuta mayai 12 anatotoa 3.....sema naahukuru kipato ninacho so nawahudumia ila sijapata profit yoyote zaidi ya nyama tu.

Kutotoa wanatotoa ila kunachangamoto sana kuvivusha vifaranga kwenda kwenye stage ya 2.
 
Mkuu hii sishauri mtu aifuate maana ataumia sana kama anategenea kuku haohao......binafsi nilitenga laki 4 nikanunua kuku wa miezi 2 kwa shs 3500 kijijini walikuwa kama 23 hivi....nikajipanga chakula kizuri plus,chanjo zote maana banda lilikuwepo.......

kuku walikufa wengine kwamagonjwa ambayo umewapa chanjo wakabaki 15 hivi ndo walivuka salama wakawa wakubwa wote tetea nikanunua jogoo 1 kwa 15...

hapo kuna vifaranga kufa kutokana na sababu fulani kuna kuku kutolalia vizuri unakuta mayai 12 anatotoa 3.....sema naahukuru kipato ninacho so nawahudumia ila sijapata profit yoyote zaidi ya nyama tu......

Kutotoa wanatotoa ila kunachangamoto sana kuvivusha vifaranga kwenda kwenye stage ya 2....
Uko sahihi. Ni vema kupata ushauri wa wataalamu.

Ninafuga kuku, nina fanya kwasababu napenda kufuga. Nawamudu sana.
 
Banda la kuku unatugaia? Kuweni serious basi
Katoa mwongozo haraka, changamoto zipo nyingi sana, otherwise wakuria hapa town wangeshakuwa matajiri sana kwa hiyo biashara.
 
Kama kuna concept wajasiriamali wengi wana overate ni hii hapa, hayo mahesabu yanavutia kuangalia lkn ukiingia kwenye practice utaambulia hasra moja takatifu.
From experience kuna vitu kma magonjwa, chakula, security na mengine. Nilijidanganya Just like mtoa mada, i lost pesa nyingi sana mainly because hatuna experts wa kutosha linapokuja kwa kuku wa kienyeji. Inshort never buy the dogma


Sent using Jamii Forums mobile app

Acha woga.
 
Nakushauri ufuge wa kisasa - Layers. wa kienyeji it takes time na faida si kubwa vile unavyodhani - nitafute nikupe ushauri wa bure - meanwhile angalia kazi hii hapa

Hawa wako 900, wanatoa Tray 24 kila siku kila Tray 5000- Chakula chao ni kilo 125 approx Tshs 55,000/-

Mtaji wa kuanzia unahitaji kuwa na not less than 6m before you start production. Kama unataka mchakato mzima sema nitakutumia database yangu.

Umemshauri vizuri,ila amesema hataki faida kubwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
New mzalendo Nitafute nikupe ushauri mambo ni mengi pia mimi ni mfugaji wa kuku wa kienyeji soko lipo kubwa sana unatakiwa tu kujua undani wake. But it seems you are not serious hako kajogoo kamoja utafika nako weapi au unaogopa risk? nipigie 0755394701 tuongee mkuu.
Hata mm nitakupigia nikitafuta masoko

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom