Mimi nnachoweza kukushauri mkuu wanapototoleshwa tumia mfumo wa ndani sio huria kwanza kuwaepusha na maadui kama mwewe kunguru na paka ila pia wasiambukizwe magonjwa na kuku wakubwa .
Hakikisha wanapata joto la kutosha hasa wakati wa usiku (kama umewatenga na mama zao unaweza kutumia taa au yale majiko ya kukuzia vifaranga).
Wapatie chanjo (sana sana kuku wa kienyeji wanasumbiliwa na magnjwa kama kideli na mafua na minyoo ).chanjo ya kideli vifaranga wako wape siku ya saba toka wametotoleshwa baada ya hapo siku ya 21 then mwsho wa mwezi minyoo .
Hakikisha unawafuga katika mazingira safi na mabanda bora wasiwe wasiwe overcrowdng .
Wapatia chakula kwa ratio sahihi ya virutubisho namaanisha hakikisha chakula wanachotumia kina muunganiko wa wanga protini mafuta na vitamin bila kusahau maji ya kutosha .
La kuongeza kwa upande ufagaji wa hawa ndege wakishaanza kuumwa kupona kidogo hua ni mthani kwa hio chanjo ni bora kuliko tiba
Tumia vitu kama OTC na multivitamin ili kuuwa vijidudu nyemelezi na kuwaongezea hamu ya kula mpka watakapofikia stage nzuri ya kuwaachia
Sent from my SM-J200H using
JamiiForums mobile app
@Joninho Nakushauri pia upitie za post za
Kubota kule juu kuhusu uleaji wa vifaranga. Pia ongezea na haya;
1. Joto.
Vifaranga wapewe joto la kutosha mpaka watakapochangamka. Hii haina formula. Yaweza kuwa siku 3, 7, 14, 21, nk kutegemeana na observation juu ya uchangamfu wao. Tumia jiko maalum la kuku ili kupata matokeo mazuri; joto hutolewa taratibu na hivyo kupunguza matumizi ya mkaa na usumbufu wa kuongeza ongeza mkaa. Mie huweka mara moja tu jioni na asubuhi ndiyo unaishia na chumba bado cha moto. Hii ni ikiwa mkaa wako ni mzuri.
2. Chakula
Kwa mujibu wa hii thread (ukiisoma yote), hauwezi kutengeneza chakula cha vifaranga yaani starter. Nishawahi kujaribu kukinzana na huu ukweli nikadondokea pua. Vifaranga wapewe chakula "special" cha kiwandani cha watengenezaji wanaoaminika kama 'Silverlands'.
Kifaranga wa nyama apewe broiler starter na yule wa mayai apewe Layer's starter. Kuepuka risk ya vifo kabla ya kufikisha mwezi mmoja, waweza kuwapa vifaranga wa mayai broiler starter kwa wiki 1, 2, mwisho 3 kabla ya kuwapa layer's starter mpaka watakapotimu wiki 6 ambapo utaanza kuwapa grower feeds.
NB: Ukiona huwezi kununua chakula mfuko mzima kwa wakati mmoja au ikiwa vifaranga ni wachache, nunua katika kilo.
PIA: Vifaranga wanapaswa kupewa chakula masaa 24 siku 7 za wiki ikiwa kweli uko siriaz.
3. Dawa
Pamoja na kwamba starter nzuri ya kiwandani huwa na dawa tayari, ni muhimu kuwapa dawa vifaranga wako kwa utaratibu ufuatao:
Vifaranga wapewe maji ya kunywa muda wote yenye dawa/chanjo zifuatazo;
I. Sukari.
Badala ya kuingia gharama ya kununua glucose, wewe wape ile sukari unayotumiaga mezani. Weka kijiko kimoja cha chakula kwenye maji lita 1. Wape kwa angalau siku 7 mpaka pale utakapoona yafaa, zingatia uchumi pia.
II. Amplolium.
Hii ni dawa na chanjo (vyote kwa mpigo) ya kukinga na kutibu ugonjwa wa coccidiosis. Ule ugonjwa ambao vifaranga au kuku husinzia na kuvaa makoti.
Hii ndiyo muhimu zaidi kwenye huu mchanganyo kwa vifaranga. Ugonjwa husababishwa na unyevu hivyo hakikisha banda ni kavu muda wote.
Amplolium iwekwe kwenye maji kwa angalau siku 7. Kipimo ni gramu 5 sawa na kijiko kimoja (level) cha chai. Yaani kale kakijiko kadogo kawe level kasiwe na mlima kwenye maji lita tano. Mimi huweka na mlima.
III. Vitamins
Vifaranga wapewe maji yenye vitamini kwa mwezi mzima wa kwanza. Ikipungua sana wiki 3. Pendelea zaidi kutumia vitamin zenye O.T.C ndani. Kama vitamini yako haina OTC ndani, nasa
hauri ununue OTC ikiwe uchumi unaruhusu, uchanganye na vitamins.
Hivi vyote viwekwe pamoja kwenye maji ambayo kuku watakunywa muda wote. Siku za chanjo vifaranga wanywe maji plain. Yaani baada ya kuondoa maji ya chanjo husika, wape maji ya kawaida. Kesho yake ndiyo uendelee na ukemia. Hii ni ikiwa unatumia chanjo za kuweka kwenye maji (kwa Newcastle na Gumboro).
4. Chanjo
Wape chanjo 4 zifuatazo ndani ya mwezi wa kwanza:
I. Newcastle.
Siku ya 3, 4, 5, 6 au 7
II. Ndui ya kuku (fowl pox);
Wiki ya 2. Yaani siku ya 14. Usisikilize vitabu vya kibongo utafeli. Chanjo hii yaweza kutolewa hata siku ya kwanza. Tunavuta muda kudogo ili kifaranga kitengeneze bawa litakaloshikika na kuchomeka sindano kirahisi.
Vitabu vyetu vimeandika wape wiki ya 6 hadi 8! Utapotea. Ugonjwa huu umekuwa sugu kwa baadhi ya koo za kuku na huja mapema, mpaka wiki ya 3 hivyo wape mara tu wanapoanza kuota mabawa.
III. Gumboro
Wiki ya 3
IV. Newcastle tena.
Wiki ya 4
Kwa kutumia program hii, siku ya 30 unakuwa na idadi ile ile ya vifaranga ulioanza nao, tena wakiwa na afya tele.
Endelea kusoma zaidi kwenye vyanzo vingine.