Nashukuru Kamuzu kwa kuonyesha uwepo wako nilifikiri niko mwenyewe tu peke yangu hapa jukwaani maana wakubwa wamekasirika wameondoka kwa kuwa nimechelewa kuwasilisha, jamani tuvumiliane!
Nilivyoendelea kufuga baada ya kuona kuwa kuku wanaoatamia wanapata usumbufu sana kutoka kwa kuku wanaoendelea kutaga, Banda langu la kuku nililigawa kukawa chumba na sebule! Nitaeleza wakati ukifika nilivyojenga mabanda yangu. Kwa hiyo chumbani niliweka viota na ndiko ambako nilikuwa nawaweka kuku wanaoatamia ili wasibughudhiwe kabisa na kuku wenzao, mlango wa kuingia chumbani nilitengeneza geti la mianzi iliyopigiliwa karibu karibu kuzuia kuku kupenya. Hapo sebuleni ndiko kuku wote watagao na wasiotaga walikuwa wanalala, kwa hiyo kulikuwa na viota vingi ambavyo juu yake nilikuwa naviwekea kizuizi kwa kutumia Mabanzi ya mbao ili usiku kuku wengine wanaposimama juu yake wasichafue kwa kinyesi chao kwenye viota. Viota hivi nilikuwa navitengeneza kwa kuweka partitions (yaani vijivyumba) kwa kutumia tofari za tope, zenye saizi kama ya matofali ya kuchoma. Kwa hiyo kwa kuambaa ukuta nilikuwa nalaza tofari nne chini kwenda juu, nilifanya hivyo kila baada ya upana wa futi moja, juu ya hizo tofali ndiyo niliweka Banzi! Ndani ya hivyo vijivyumba nilitifua umbo kama kijibeseni na kuweka Majani laini ili mayai yatulie yasisambae. Huko chumbani wakati wote kulikuwa na chombo chenye chakula na chenye maji! Hakuna kuku kutoka na hakuna kuku wa kuwaingilia! Ilikuwa ni incubator TOSHA! Nilikuwa nawaona kuku kama wananishukuru kwa kuwatengenezea mazingira safi maana walikuwa hawabughudhiwi na walikuwa wanashiba chakula vizuri tu! Nitaeleza siku nyingine juu ya harakati zangu za kutengeneza chakula na changamoto nilizokutana nazo! Huko chumbani nilikuwa nimetandaza carpet la nyasi; kando kando ya kuta zote kulikuwa na viota ambavyo nilivizamisha ndani ya hilo kapeti la nyasi nadhani mtanielewa! Ninaposema carpet la nyasi, ni nyasi tu nilizisambaza kwa unene wa kama sm 15 au nchi sita! Kwa hiyo kipindi hawa kuku wanapokuwa wanaatamia nilikuwa nazuia wengine wasiatamie hadi hawa watakapototoa! Kwa hiyo mayai yanayopatikana wakati hawa wengine wanaatamia nilikuwa ninakula na mengine kuuza maana mpango wangu ilikuwa kutotolesha mara moja tu kuku mia kwa mwezi! Hii ndiyo Incubator yangu ambayo nilikuwa ninatotolesha vifaranga 100 kwa siku moja!! Kwa kuwa nilikuwa ninajukumu pia la kulea kuku utotoleshaji nilikuwa ninaudhibiti uendane na miundombinu yangu ya kulea kuku na vifaranga.
ITAENDELEA ............