Ufugaji wa Kuku wa Kienyeji na Masoko yake

Mkuu Kubota nakusubiri kwa hamu kwenye magonjwa, kwakweli shule hii ni kiboko. Nimiekuwa nikifuga kwa sasa ni miezi mitatu. Tatizo ni vifaranga nimekuwa nikiwalisha starter toka kutotolewa mpaka week ya tano. niliwachanja chanjo ya jicho. wakakua vizuri mpaka wakaanza kuota manyoya. week ya tano nikaanza kuwatoa nje, mara nikaona kama watatu hivi ghafla wakaanza kuvaa makoti. kwanini wakati nimewachanja na wataalamu waliniambia nikiwachanja chanjo ya jicho hawatapata huo ugonjwa. nimechanganyikiwa maana nategemea kupata vifaranga wasiopungua arobaini maana kuna kuku wanne wanaatamia mayai 15 kila mmoja.

Polee sana mkuu guta kwa kupoteza vifaranga wako hizo ni baadhi ya changamoto za ufugaji.kuwachanja vifaranga ni jambo zuri na kitalaamu inashauriwa hivyo.hiyo chanjo uliyochanja ni dhidi ya ugonjwa wa mdondo(new castle disease).na kutoka na maelezo yako inaonekana ulitumia ya matone.hii ya matone ni nzuri kwa sababu inaweza kukaa muda mrefu endapo tu itahifadhiwa kwenye ubaridi na kutumika zaidi ya mara moja.hivyo basi kama haitahifadhiwa kwenye mazingira niliyotaja hapo juu uwezekano ni mkubwa kwa hii chanjo kupungua nguvu na hivyo kupelekea kufail pindi utakapo chanja. Na kwa kuiangalia huwezi kugundua kama imepungua nguvu madhara utaona kuku kuanza kuumwa huo ugonjwa wakati uliwachanja.Asante
 
Last edited by a moderator:

Mkuu Dafo asante, ukweli uko hivyo hivyo kama ulivosema! Huwezi jua iwapo hiyo chanjo nzima au imekufa, inakuwa ni fumbo la imani ...
 
Mkuu LiverpoolFC shukrani kwa kunitia moyo jinsi unavyofuatilia stori! Nivumilie kidogo pitia hapa jumatatu nitakuwa naendeleza story kuhusu chakula, sina uhakika kama nitafikia magonjwa. Ila uzuri ni kwamba wachangiaji wameshaanza kutoa vidokezo vyenye nguvu sana na ukweli usiokuwa na chenga hata kidogo! Mkuu Dafo ni mmojawao!
 
Kubota;

Hakika tupo pamoja mwanzo mwisho!
Na hata hivyo nitakuseach hiyo jumatatu yani kesho majaliwa! Na hata hivyo uwe na wakati mzuri Mkubwa!

Mkuu LiverpoolFC shukrani kwa kunitia moyo jinsi unavyofuatilia stori! Nivumilie kidogo pitia hapa jumatatu nitakuwa naendeleza story kuhusu chakula, sina uhakika kama nitafikia magonjwa. Ila uzuri ni kwamba wachangiaji wameshaanza kutoa vidokezo vyenye nguvu sana na ukweli usiokuwa na chenga hata kidogo! Mkuu Dafo ni mmojawao!
 
Last edited by a moderator:
Yellow diarrhea or fowl typhoid (kuvaa koti) white chalky diarrhoea is bacillary dysentry. Nenda na dalili izo pharmacy wakupe dawa. Osha vyombo vyote. Ondoa maranda na vinyesi tenga wagonjwa
 
Pamoja na kuwapata kuku chanjo zote na kuwa tibia wapatapo Maradhi,wawekee majani ya muarobaini kwenye maji Yao ya kunywa walau mara moja kwa wiki itasaidia sana kwa kuku kupata maradhi kwa urahisi.ninafanya hivyo naona mafanikio[SUB]​[/SUB]
 
Mama timmy;

Hebu pitia tena hii post yako hasa hapo penye red!

Pamoja na kuwapata kuku chanjo zote na kuwa tibia wapatapo Maradhi,wawekee majani ya muarobaini kwenye maji Yao ya kunywa walau mara moja kwa wiki

itasaidia sana kwa kuku kupata maradhi kwa urahisi.

ninafanya hivyo naona mafanikio[SUB][/SUB]

Dear Mama timmy; siyo umepitiwa ukachanganya lugha kweli?
 
Last edited by a moderator:
Kweli muarobaini na mlonge majani yake kinga nzuri sana me nafanya ivo ila wakipata uambukizo inabidi watibiwe. Mie nilikuwa na broiler wk ya kwanza wakati ninahawa hybrid banda jingine kwa kweli nilizembea kidogo kuchanganya vyombo wakapata coccidiosis nayo ni kuharisha na inaua wengi. Vifo vingi ni umri wa vifaranga mimi siwatoi nje maana hawana kinga kama wakubwa.
 
Ni kweli usemavyo.kutibiwa ni lazima kuku akipata maradhi.ila Kama ukiwa na mazoea ya kutumia Haya majani Kama lishe inasaidia sana kuku kutokuonewa na magonjwa hovyo hovyo.mimi nafuga wa kienyeji kabisa na ninawatoa kwa mama Yao mara wanapoanguliwa na kukauka nawafuga Kama broiler kwa wiki Sita tu.baada ya hapo naendelea nao Kama kawaida ya kienyeji.
 
Polee sana mkuu guta kwa kupoteza vifaranga wako hizo ni baadhi ya changamoto za ufugaji.kuwachanja vifaranga ni jambo zuri na kitalaamu inashauriwa hivyo.hiyo chanjo uliyochanja ni dhidi ya ugonjwa wa mdondo(new castle disease).na kutoka na maelezo yako inaonekana ulitumia ya matone.hii ya matone ni nzuri kwa sababu inaweza kukaa muda mrefu endapo tu itahifadhiwa kwenye ubaridi na kutumika zaidi ya mara moja.hivyo basi kama haitahifadhiwa kwenye mazingira niliyotaja hapo juu uwezekano ni mkubwa kwa hii chanjo kupungua nguvu na hivyo kupelekea kufail pindi utakapo chanja. Na kwa kuiangalia huwezi kugundua kama imepungua nguvu madhara utaona kuku kuanza kuumwa huo ugonjwa wakati uliwachanja.Asante

Ahsante Mkuu Dafo , sina uhakika na chanjo niliyowapa kama ina fanya kazi, niliinunua na duka liko karibu na ninapoishi niliitumia maramoja tu nikatupa iliyobaki kwa kuwa waliniaambia ikiishiwa ubaridi inaishiwa nguvu.
kama itawezekana wakati tunamsubiri Kubota unaweza kutuelezea magonjwa ya kuku na dalili zake hasa vifaranga. magonjwa yananichanganya kati ya mdondo na huu wa kuvaa makoti Yellow diarrhea or fowl typhoid kama Mama Joe
alivyodokeza. @Mama timmy inaelekea tiba mbadala unauzoefu nazo thanks. Ngoja tusubiri na mbinu za kubota naamini tutafanikiwa. thanks all.
 
Last edited by a moderator:
Wadau naendelea tena na hadithi yangu. Niliishia kusimulia utayarishaji chakula cha vifaranga. Nashukuru kwa michango toka kwa wakuu, Dafo, Mama Timmy, Mama Joe na wengine jinsi mnavyojadiliana kama vile tuko pamoja physically, kumbe jukwaa hili likitumika ipasavyo mtu hujisikii mpweke.

Kabla sijasimulia kuhusu ulishaji wangu kwa kuku wakubwa kwanza niseme yafuatayo: Kwa mtazamo wangu ufugaji wa kuku wa kienyeji kibiashara unahitaji kufanyika kwa ujanja sana ili kuweza kupata faida. Japo kuku hawa wanaonekana wanabei kubwa sokoni inahitajika kuwa makini sana jinsi ya kuwahudumia ili kupata faida. Kuku wa kienyeji hukua taratibu sana ukilinganisha na kuku wa kisasa. Hata wakipewa chakula kile kile ambacho wanapewa broiler, broiler hufikia uzito wa kuuzwa sokoni haraka sana wakati kuku wa kienyeji anachukua muda mrefu zaidi kupindukia. Hata wakipewa chakula kile kile ambacho wanapewa kuku wa mayai (Layers) kuku wa kienyeji hawawezi kutaga mayai kwa wingi kama ilivyo kwa kuku wa kisasa wa mayai. Unapojenga banda la kuku, unapoamua aina ya vyombo vya kulishia kuku na unapoamua aina ya chakula cha kulisha kuku wako wa kienyeji lazima kuzingatia sana iwapo gharama hiyo itarudi au la! Iwapo utafuga kuku wa kienyeji kwa kuwajengea mazingira ya kiwango cha juu kama ifanywavyo kwa kuku wa kisasa ni busara mfugaji ukafuga moja kwa moja kuku wa kisasa.

Kuku wa kienyeji wanalipa sana kwenye ufugaji huu mdogo mdogo katika hatua za mwanzo za kutafuta kasi ya kukuza mitaji. Hata pale mfugaji akipenda kuwafuga kuku hawa kwa wingi kabisa, inalipa zaidi iwapo kuku hawa watafugwa kwa aina ya ufugaji huria ambapo wanakuwa na fursa ya kuchunga. Hivyo inabidi kutafuta eneo kubwa la uwazi kadri ya uwezo wa mfugaji! Kuna vipimo vipo vya idadi ya kuku kwa kila ekari moja ya eneo la kuchunga kuku. Ufugaji wa kuku wa kienyeji kwa mtindo wa kuwaweka ndani muda wote kama ilivyo kwa kuku wa kisasa inahitaji kupiga mahesabu vizuri kuweza kujua kama kuna faida kweli hasa kwenye gharama za chakula! Kuku wa kisasa wanakua haraka haraka sana na wanataga mayai sana kwa hiyo gharama za kuwalea kwa kuwalishia ndani hurudi na faida kubwa hupatikana.

Pamoja na kwamba kuku wa kienyeji huchunga wenyewe, mimi kwa wakati wote nilikuwana nawawekea chakula kwenye vyombo. Vyombo hivyo vilikuwa vikijazwa asubuhi chakula kilitosha kulisha kuku kutwa nzima. Kwa kiyo kuku wakifunguliwa asubuhi walikuwa wanakula chakula walichowekewa kisha wanakwenda kuokoteza au kuchunga kisha badae walikuwa wakirudi nyumbani kuja kujazia/chakula ambacho muda wote kilikuwepo nyumbani. Kwa kufanya hivyo kuku walikuwa wanashiba kwa uhakika.

Kuku wanapokula kwa kawaida huwa wanamwaga mwaga sana na hiyo ni hasara kubwa ambayo hupunguza faida! Ili kupunguza tatizo hili chakula nilikuwa ninakiwekea maji maji kidogo ili kishikamane lakini siyo maji ya kukifanya kiwe rojo rojo. Vyombo vyangu vya chakula cha kuku zilikuwa ni ndoo za lita 10 ambazo nilizitoboa katikati matundu ya kutosha kuingiza vichwa vya kuku kwa kuzunguka ndoo kama wanavyofanya wengi, huku kukiwa na kina cha kutosha kubeba chakula ndani yake.

Kuku wakishiba wanatabia ya kuchagua chenga au vitu wanavyopenda wenyewe ndani ya chakula, wanapofanya hivyo hurusha chakula nje ya chombo na kukimwagamwaga. Kuku pia husimama juu ya vyombo vya chakula kama hakina mfuniko juu, hukichafua chakula kwa kinyesi, kuku pia wanaweza kumwaga chakula chote kwenye chombo iwapo chombo hakijashikizwa kukizuia kisianguke, kuku hubwaga chini vyombo vyenye chakula wanapokimbizana au kupanda juu ya ya vyombo hivyo. Nilichukua taadhari zote kuepuka hayo yote niliyosema hapo juu yasitokee.
 
Ilibidi nichague maeneo maalumu ya kuweka vyombo vya chakula baada ya kubaini kuwa chakula kingi kilikuwa kinapotea kwa kuliwa na mifugo wa majirani ambapo mbuzi na ngombe wao walikuwa wakisukuma vyombo vya chakula na kumwaga chini kisha wanakila. Kuepuka mifugo ya majirani niliamua vyombo vya maji na chakula kuviacha bandani muda wote. Siku moja nilikuta ngombe amejilazimisha kuingia bandani kufuata unono wa pumba na mashudu ya alizeti kwenye chakula. Katika kujilazimisha huko alihatarisha banda kwani mlango ulikuwa mdogo hivyo alijitikisa sana kiasi cha kutikisika banda lote. Ilibidi kuanzia hapo niweke kizuizi mlangoni kuzuia mbuzi na ngombe kuingia bila kuathiri uingiaji wa kuku.

Baadae niligundua pia kuwa uwepo wa chakula kwenye vyombo mabandani ulivuta panya wengi ambao walikuwa wanakuja kwa wingi kula chakula wakati wa usiku, walikuwa wanaleta hasara kwa kupunguza chakula hicho, bahati nzuri tu ni kwamba kuku wanapokaribia kulala ile jioni hula sana chakula kwa wingi hivyo nilipunguza uwekaji chakula kwenye vyombo ili kwamba wanapolala usiku chakula kinakuwa kimeshaisha kwenye vyombo. Nilikuwa ninaweka vyombo vya maji ambavyo vilikuwa na uwezo wa kuhifadhi maji kutwa nzima. Hapo nililazimika kununua vyombo vya maji vya kisasa ambavyo vilikuwa vinatunza maji kwa usafi zaidi kutosha siku nzima. Maji ya kunywa kuku ni kitu nyeti niliona ni lazima ninunue.

Kulikuwa pia kuna tatizo la kuku wakubwa kuwadhibiti wadogo wasipate chakula hadi wao wakubwa kwanza washibe, kama huujui ubabe ni kitu gani hapa duniani tazama mfano huo kwa kuku wenye umri tofauti wanapokula. Wingi wa vyombo ulisaidia kupunguza tatizo hili ingawa baadae ili kuwatetea kuku wadogo nilitengeneza wigo wenye milango ambamo ndani yake niliweka chakula na kuku wakubwa kwa umbo lao kubwa hawakuweza kuingia humo.

Utengenezaji wa chakula cha kuku wakubwa nilikuwa nachanganya mchanganyiko wa pumba za mahindi na mashudu ya alizeti yaliyosagwa. Sikutaka kuremba remba sana kwenye chakula cha kuku wakubwa kwa kuzingatia kuwa kuku hawa walikuwa wanafursa ya kuokoteza wadudu, kula mimea na matunda vitu kadha wa kadha ambavyo walikuwa wanaokoteza wachungapo.

Mashudu ya alizeti popote yapatikanapo yanapaswa yachukuliwe kama ni hazina kubwa sana kwenye chakula cha mifugo yote! Mashudu ya alizeti si kama pumba za mahindi! Pumba za mahindi ni ganda tu la nje la punje za mahindi labda itokee kuwepo na chenga chenga kulingana na ubora wa mashine iliyokoboa mahindi baada ya kutolewa wanga na kiini cha mbegu kiasi! Lakini mashudu ya alizeti ni punje zilizosheheni wanga, protein, madini na mafuta kiasi! Mashudu ya alizeti kama yalivyo mashudu ya mazao mengine yanayokamuliwa mafuta, kinachopunguzwa humo kwenye mbegu huwa ni mafuta tu virutubisho vingine vingi hubaki kama vilivyo! Kwa hiyo kwa kujua hili nilikuwa ninachanganya kwa uwiano wa debe moja la mashudu yaliyosagwa na debe mbili za pumba za mahindi. Kuku wangu walikuwa wanataga kwa wingi bila mashaka na wakipikwa walikuwa wamenona ipasavyo na walikuwa na uzito mzuri. Kwa hiyo nilichukulia kuwa ulishaji wangu huu ulikuwa umefanikiwa. Bei ya mashudu na pumba kwa mazingira niliyokuwa nikiishi haikuhichemsha kichwa.

Jambo ambalo nilikuja kuligundua baadae ni kwamba kuku wakipewa chakula wakashiba hawaendi mbali! Kuku wanaozurula sana mtaa hadi mtaa huwa ni shauri ya kutafuta chakula! Kuku wangu walikuwa hawaendi kusumbua bustani za jirani zangu. Kilichotokea tu ni kwamba kuku wa jirani zangu ndiyo walishinda kwangu kitu ambacho hata nikiuza jogoo wangu wote haikuwa shida maana kuku wangu walipata huduma za jogoo wa jirani bila wasiwasi!!

Nilifanikiwa kuhakikisha kuku wanashinda wameshiba na waliweza kutaga na walikuwa na uzito mzuri kwa kutumia mbinu hiyo.

ITAENDELEA…………………..
 
Wadau naendelea tena na hadithi yangu. Niliishia kusimulia utayarishaji chakula cha vifaranga. Nashukuru kwa michango toka kwa wakuu, Dafo, Mama Timmy, Mama Joe na wengine jinsi mnavyojadiliana kama vile tuko pamoja physically, kumbe jukwaa hili likitumika ipasavyo mtu hujisikii mpweke.

Kabla sijasimulia kuhusu ulishaji wangu kwa kuku wakubwa kwanza niseme yafuatayo: Kwa mtazamo wangu ufugaji wa kuku wa kienyeji kibiashara unahitaji kufanyika kwa ujanja sana ili kuweza kupata faida. Japo kuku hawa wanaonekana wanabei kubwa sokoni inahitajika kuwa makini sana jinsi ya kuwahudumia ili kupata faida. Kuku wa kienyeji hukua taratibu sana ukilinganisha na kuku wa kisasa. Hata wakipewa chakula kile kile ambacho wanapewa broiler, broiler hufikia uzito wa kuuzwa sokoni haraka sana wakati kuku wa kienyeji anachukua muda mrefu zaidi kupindukia. Hata wakipewa chakula kile kile ambacho wanapewa kuku wa mayai (Layers) kuku wa kienyeji hawawezi kutaga mayai kwa wingi kama ilivyo kwa kuku wa kisasa wa mayai. Unapojenga banda la kuku, unapoamua aina ya vyombo vya kulishia kuku na unapoamua aina ya chakula cha kulisha kuku wako wa kienyeji lazima kuzingatia sana iwapo gharama hiyo itarudi au la! Iwapo utafuga kuku wa kienyeji kwa kuwajengea mazingira ya kiwango cha juu kama ifanywavyo kwa kuku wa kisasa ni busara mfugaji ukafuga moja kwa moja kuku wa kisasa.

Kuku wa kienyeji wanalipa sana kwenye ufugaji huu mdogo mdogo katika hatua za mwanzo za kutafuta kasi ya kukuza mitaji. Hata pale mfugaji akipenda kuwafuga kuku hawa kwa wingi kabisa, inalipa zaidi iwapo kuku hawa watafugwa kwa aina ya ufugaji huria ambapo wanakuwa na fursa ya kuchunga. Hivyo inabidi kutafuta eneo kubwa la uwazi kadri ya uwezo wa mfugaji! Kuna vipimo vipo vya idadi ya kuku kwa kila ekari moja ya eneo la kuchunga kuku. Ufugaji wa kuku wa kienyeji kwa mtindo wa kuwaweka ndani muda wote kama ilivyo kwa kuku wa kisasa inahitaji kupiga mahesabu vizuri kuweza kujua kama kuna faida kweli hasa kwenye gharama za chakula! Kuku wa kisasa wanakua haraka haraka sana na wanataga mayai sana kwa hiyo gharama za kuwalea kwa kuwalishia ndani hurudi na faida kubwa hupatikana.

Pamoja na kwamba kuku wa kienyeji huchunga wenyewe, mimi kwa wakati wote nilikuwana nawawekea chakula kwenye vyombo. Vyombo hivyo vilikuwa vikijazwa asubuhi chakula kilitosha kulisha kuku kutwa nzima. Kwa kiyo kuku wakifunguliwa asubuhi walikuwa wanakula chakula walichowekewa kisha wanakwenda kuokoteza au kuchunga kisha badae walikuwa wakirudi nyumbani kuja kujazia/chakula ambacho muda wote kilikuwepo nyumbani. Kwa kufanya hivyo kuku walikuwa wanashiba kwa uhakika.

Kuku wanapokula kwa kawaida huwa wanamwaga mwaga sana na hiyo ni hasara kubwa ambayo hupunguza faida! Ili kupunguza tatizo hili chakula nilikuwa ninakiwekea maji maji kidogo ili kishikamane lakini siyo maji ya kukifanya kiwe rojo rojo. Vyombo vyangu vya chakula cha kuku zilikuwa ni ndoo za lita 10 ambazo nilizitoboa katikati matundu ya kutosha kuingiza vichwa vya kuku kwa kuzunguka ndoo kama wanavyofanya wengi, huku kukiwa na kina cha kutosha kubeba chakula ndani yake.

Kuku wakishiba wanatabia ya kuchagua chenga au vitu wanavyopenda wenyewe ndani ya chakula, wanapofanya hivyo hurusha chakula nje ya chombo na kukimwagamwaga. Kuku pia husimama juu ya vyombo vya chakula kama hakina mfuniko juu, hukichafua chakula kwa kinyesi, kuku pia wanaweza kumwaga chakula chote kwenye chombo iwapo chombo hakijashikizwa kukizuia kisianguke, kuku hubwaga chini vyombo vyenye chakula wanapokimbizana au kupanda juu ya ya vyombo hivyo. Nilichukua taadhari zote kuepuka hayo yote niliyosema hapo juu yasitokee.

Ahsante sana kwa darasa zuri. Mimi sijaanza ufugaji lkn najifunza sana katika hii thread na ipo siku nitaanza kazi hii.
 
Ahsante Mkuu Dafo , sina uhakika na chanjo niliyowapa kama ina fanya kazi, niliinunua na duka liko karibu na ninapoishi niliitumia maramoja tu nikatupa iliyobaki kwa kuwa waliniaambia ikiishiwa ubaridi inaishiwa nguvu.
kama itawezekana wakati tunamsubiri Kubota unaweza kutuelezea magonjwa ya kuku na dalili zake hasa vifaranga. magonjwa yananichanganya kati ya mdondo na huu wa kuvaa makoti Yellow diarrhea or fowl typhoid kama Mama Joe
alivyodokeza. @Mama timmy inaelekea tiba mbadala unauzoefu nazo thanks. Ngoja tusubiri na mbinu za kubota naamini tutafanikiwa. thanks all.
Sawa mkuu Guta.naomba nikiri kwanza mimi sio mtaalam wa mifugo ila naongea kutoka na uzoefu wangu kwenye ufugaji na hobby niliyonayo katika ufugaji.katika ufugaji hasa wa kuku hiki kipindi cha kuanzia siku 1 hadi wiki ya 4 kuna changamoto sana.na katika kipindi hicho ndio kuku na mazao yaliyobora yanapo andaliwa, kifaranga asipotunza vizuri ni uwezekano wa kutoa mazao bora ni mdogo sana.vifaranga uwa wanasumbuliwa sana na homa za matumbo kama fowl typhoid, coccidiosis etc. kipindi hicho.ugonjwa wa mdondo ndo ugonjwa unaofahamika na wafugaji wengi sana hata wale ambao hawajawahi fuga kuku uwa wanausikia sana huu ugonjwa na sifa kubwa ya huu ugonjwa uwa unasababisha vifo vingi sana na hauna tiba ingawa ukienda kwa watalaamu wanaweza kukupa antibiotics ili kupunguza madhara na baadhi ya kuku wakapona.hivyo basi inashauriwa kuwachanja kuku siku ya 3, siku ya 21 na kila baada ya miezi mitatu.(assumption ni kuwa chanjo ina ubora, umezingatia masharti ya kuchanja na pia usichanje kuku mgonjwa)..baadhi ya dalili za ugonjwa huu kuku husinzia, anakua hali vizuri, hachangamki.
Ugonjwa huo wa kuharisha machano ni dalili ya ugonjwa matumbo na hii ndio dalili kubwa mara nyingi vifo vinakuwa sio vingi kwa muda mfupi.
NB: mara tu uonapo kuku mgonjwa haraka iwezekanvyo mtenge usisite kufanya hvyo mapema na inashauriwa kwa haraka pia uende ukamuone watalaamu wa mifugo kwa ushauri usipende tu kukimbilia kutumia dawa.Pia nakushauri epuka kununua dawa kwenye haya maduka ya mtaani ambayo hayana watalaamu wanakuuzia tu kama wanakuuzia pen.
Pia katika ufugaji usafi wa vyombo na mazingira yao ni muhimu sana hasa vifaranga uwa hawataki kabisa unyevunyevu.Asante
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Kubota bado tuko pamoja kwenye hili darasa.Kwajinsi navyosoma uzoefu wako hapa kuna wakati najihisi kabisa kama nafahamu mazingira yako na jinsi unavyojitoa katika ufugaji.Kiukweli kuku wetu wa asili tulizoea kuwafuga hasa kama kitoweo ukuaji wake ni mdogo, ingawa akipunguziwa shughuli ile ya kutafuta chakula mwenyewe anaweza akaongezeka kasi ya kukua kidogo lakini sio sawa na wa kisasa.Kuku wa asili inamuhitaji miezi 5 hadi 6 hadi aanze kutaga ambayo ni sawa na kuku wa mayai lakini tofauti inakuja kwenye idadi ya mayai kwa mwaka anyoweza kutaga.Kutokana na kutorishishwa na ukuaji wa kukua wa asili nadhani ndio maana watu wakaamua kuanza kufuga kuku chotara ambao kwa kweli ukuaji wao unarihisha na hata ukiwafuga unafurahia kuwaona na uzito wa kutosha.Katika hali ya kawaida kabisa ukimwambia mtu ambaye hajawahi kufuga kuwa unafuga kuku wa kienyeji moja kwa moja anachulia ni kitu rahisi sana ni kiasi cha kufungua banda asubuhi na kufunga jioni lakini ukija kumpa hii shule na uliyopitia atakuwa umemfungua akili na kuona sio shughuli rahisi hivyo.Mimi naelewa ulikopitia kwa sababu mimi pia nina uzoefu wa ufugaji na ni hobby yangu kubwa tu.Kwa sasa ngoja niishie hapa tukisubiria nondo zako mkuu.
 
Wadau naendelea tena na hadithi yangu. Niliishia kusimulia utayarishaji chakula cha vifaranga. Nashukuru kwa michango toka kwa wakuu, Dafo, Mama Timmy, Mama Joe na wengine jinsi mnavyojadiliana kama vile tuko pamoja physically, kumbe jukwaa hili likitumika ipasavyo mtu hujisikii mpweke.

Kabla sijasimulia kuhusu ulishaji wangu kwa kuku wakubwa kwanza niseme yafuatayo: Kwa mtazamo wangu ufugaji wa kuku wa kienyeji kibiashara unahitaji kufanyika kwa ujanja sana ili kuweza kupata faida. Japo kuku hawa wanaonekana wanabei kubwa sokoni inahitajika kuwa makini sana jinsi ya kuwahudumia ili kupata faida. Kuku wa kienyeji hukua taratibu sana ukilinganisha na kuku wa kisasa. Hata wakipewa chakula kile kile ambacho wanapewa broiler, broiler hufikia uzito wa kuuzwa sokoni haraka sana wakati kuku wa kienyeji anachukua muda mrefu zaidi kupindukia. Hata wakipewa chakula kile kile ambacho wanapewa kuku wa mayai (Layers) kuku wa kienyeji hawawezi kutaga mayai kwa wingi kama ilivyo kwa kuku wa kisasa wa mayai. Unapojenga banda la kuku, unapoamua aina ya vyombo vya kulishia kuku na unapoamua aina ya chakula cha kulisha kuku wako wa kienyeji lazima kuzingatia sana iwapo gharama hiyo itarudi au la! Iwapo utafuga kuku wa kienyeji kwa kuwajengea mazingira ya kiwango cha juu kama ifanywavyo kwa kuku wa kisasa ni busara mfugaji ukafuga moja kwa moja kuku wa kisasa.

Kuku wa kienyeji wanalipa sana kwenye ufugaji huu mdogo mdogo katika hatua za mwanzo za kutafuta kasi ya kukuza mitaji. Hata pale mfugaji akipenda kuwafuga kuku hawa kwa wingi kabisa, inalipa zaidi iwapo kuku hawa watafugwa kwa aina ya ufugaji huria ambapo wanakuwa na fursa ya kuchunga. Hivyo inabidi kutafuta eneo kubwa la uwazi kadri ya uwezo wa mfugaji! Kuna vipimo vipo vya idadi ya kuku kwa kila ekari moja ya eneo la kuchunga kuku. Ufugaji wa kuku wa kienyeji kwa mtindo wa kuwaweka ndani muda wote kama ilivyo kwa kuku wa kisasa inahitaji kupiga mahesabu vizuri kuweza kujua kama kuna faida kweli hasa kwenye gharama za chakula! Kuku wa kisasa wanakua haraka haraka sana na wanataga mayai sana kwa hiyo gharama za kuwalea kwa kuwalishia ndani hurudi na faida kubwa hupatikana.

Pamoja na kwamba kuku wa kienyeji huchunga wenyewe, mimi kwa wakati wote nilikuwana nawawekea chakula kwenye vyombo. Vyombo hivyo vilikuwa vikijazwa asubuhi chakula kilitosha kulisha kuku kutwa nzima. Kwa kiyo kuku wakifunguliwa asubuhi walikuwa wanakula chakula walichowekewa kisha wanakwenda kuokoteza au kuchunga kisha badae walikuwa wakirudi nyumbani kuja kujazia/chakula ambacho muda wote kilikuwepo nyumbani. Kwa kufanya hivyo kuku walikuwa wanashiba kwa uhakika.

Kuku wanapokula kwa kawaida huwa wanamwaga mwaga sana na hiyo ni hasara kubwa ambayo hupunguza faida! Ili kupunguza tatizo hili chakula nilikuwa ninakiwekea maji maji kidogo ili kishikamane lakini siyo maji ya kukifanya kiwe rojo rojo. Vyombo vyangu vya chakula cha kuku zilikuwa ni ndoo za lita 10 ambazo nilizitoboa katikati matundu ya kutosha kuingiza vichwa vya kuku kwa kuzunguka ndoo kama wanavyofanya wengi, huku kukiwa na kina cha kutosha kubeba chakula ndani yake.

Kuku wakishiba wanatabia ya kuchagua chenga au vitu wanavyopenda wenyewe ndani ya chakula, wanapofanya hivyo hurusha chakula nje ya chombo na kukimwagamwaga. Kuku pia husimama juu ya vyombo vya chakula kama hakina mfuniko juu, hukichafua chakula kwa kinyesi, kuku pia wanaweza kumwaga chakula chote kwenye chombo iwapo chombo hakijashikizwa kukizuia kisianguke, kuku hubwaga chini vyombo vyenye chakula wanapokimbizana au kupanda juu ya ya vyombo hivyo. Nilichukua taadhari zote kuepuka hayo yote niliyosema hapo juu yasitokee.
Ndugu yangu Kubota hii mbinu ya kulowesha chakula niliwahi itumia baada ya muda kuku walipata mafua.nilipoenda kwa daktari akanielekeza kuacha kuwapa chakula Chenye unyevu na pumba zao akanielekeza nizikaushie kwenye kivuli.vp wewe haikukupa tabu?
 
Back
Top Bottom