Pole sana kwa kweli kuwaweka na mama zao inasaidia joto ila kuna risk kupata magonjwa kubwa sana, kifupi hawa wakubwa wakifika umri fulani wanakuwa wamepata immunity ya magonjwa mengi ingawa wanakuwa na vijidudu kwenye damu, au choo ila hayawadhuru tatizo ikitokea hawa vifaranga wamekutana na vinyesi vya wakubwa tu uambukizo kwao unakuwa ni ugonjwa. Hii inatokea kwa hata kuchanganya vyombo vya maji, ku share banda au kwa miguu ya watunzaji toka nje au banda hili kwenda hili. Ndo maana kuhofia hilo kuna wengine wanashauri kuanzia wiki ya pili hata kama hawaumwi wapewe Amprolium dose ndogo huwakinga na ugonjwa wa coccidiosis, ingawa sina uzoefu na hawa wa kienyeji ila hii ni kwa wa kisasa tumekuwa tukifanya hivyo ukichelewa na hasa kama uambukizo ukitokea inabidi watibiwe. Kutokana na dalili zako naweka hapa dalili kutoka kitabuni lakini nakushauri jieleze vizuri pharmacy wataelewa ni ugonjwa gani
Ugonjwa Dalili za Ugonjwa Kinga/Tiba
Kuharisha damu (Coccidiosis)
Kuzubaa
Kushusha mabawa kama
mtu aliyevaa koti.
Kupoteza hamu ya kula.
Kuharisha kinyesi chenyerangi ya kahawia au kilichochanganyika na damu.
Kuharisha damu
Manyoya kutimka
Kupauka kwa upanga na ndevu
Kudhoofika na hatimaye huwezakufa.
Tiba:
Ugonjwa huo unawezakutibika kwa amprolium, salfa na ESb3 kama hatua
za kuudhibitizitachukuliwa mapema
Kinga kuepuka unyevunyevukatika matandiko.
Kuwatenga kuku wanaoonyeshadalili za ugonjwa.
Kinga kwa kutumia coccidiostat.
Kutibu kwa kufuataushauri wa wataalam wa mifugo.
My take, wakati tunasubiri ushauri wa wengine nakushauri ondoa maranda au uchafu wowote bandani, ukitibu watibie kuku wote, kila yakilowa maranda ondoa weka mengine jitahidi kuwasogeza hata wagonjwa kwenye dawa, mwaka jana mie iliwapata broiler walichanganya vyombo vyao na hawa chotara wakubwa, ukijitahidi wanapona hasa vile hawa ni kienyeji wako strong. All the best