Habari zenu wana JF,
Hongera sana Kubota kwa kuanzisha huu uzi pia na wachangiaji wote.
Umegusia Kuwa unafikiria kuanza ufugaji kwa kuanza na kuku 250 Ndan ya ekari moja na baadaye ekari nne. Swali langu ni namna gani utapambana na maadui mf: paka, panya, Mbwa, n.k yaan Wale wote wanaoweza kuwadhuru kuku.
Asante!
Niliahidi kuendelea kusimulia jinsi ambavyo nilimudu kupambana na maadui wala kuku!
Unapoanza kufuga kuku unakuwa kivutio kikubwa kwa kila aina ya midomo, kuna nyoka, vicheche, paka
pori, tai, kenge, mbwa koko, nyani, nguruwe wakiwemo na watu pia.
Nyoka na kenge walikuwa wakija kwa vipindi fulani fulani halikuwa tatizo la kila mara. Kenge walivizia zaidi mayai, nyoka walikuwa wanaua sana kuku. Nyoka anapokuja bandani ambapo mara nyingi ni usiku huwa ni rahisi kujua maana kuku hupiga kelele sana. Kudhibiti nyoka inawezekana kwa kupambana na kuwauwa kila wanapokuja, na hii inahitaji ujasiri maana usipokuwa makini unaweza kuua sana kuku badala ya nyoka mwenyewe. Njia ya kujihami ni kuhakikisha mabanda hayatoi mianya ya nyoka kupenya na kuingia bandani mara baada ya banda kufungwa. Nimewahi kusikia na nitakuja kutoa taarifa hapa bado ninafuatilia, kwamba kuna aina ya mti fulani ambao ukitumika kwa namna fulani huzuia nyoka wasifike kwenye eneo!
Ndege wa angani kama tai na kunguru wanatamba sana kama kuna uwazi hakuna vichaka vya kujifichia. Kuku ambao hushambuliwa zaidi ni vifaranga na vinyoya. Lakini hawa wote ni hodari sana kujificha iwapo kuna kitu cha kujifichia.
Kadharika ndege mara nyingi hutua kwanza kwenye mti kabla hawajachukua kasi ya kwenda kufanya mashambulizi. Uwepo wa miti mirefu kwenye eneo la ufugaji hukaribisha balaa. Unaweza kujenga kama mfano wa chanja fupifupi kama futi moja toka chini sehemu tofauti tofauti za eneo lako wanakochungia kuku. Hii itawazaidia kukimbilia chini yake pale mwewe au kunguru akianza kuleta shida.
Kuku wanaishara ambazo hutoa mara mwewe akiwasili na vinyoya hukimbia mara moja chini ya chanja hizi. Chini ya chanja hizi ni sehemu nzuri pia kuweka chakula cha nyongeza na maji. Zinaweza kuwa nyingi kadri wingi wa kuku ulivyo na kwa kutumia common sense.
Funga kazi ya yote, katika kudhibiti viumbe wengine waliosalia nilioorodhesha hapo juu nilikuwa ninatumia mbwa. Ufugani wa kuku ndiyo uliofanya kubaini kuwa mbwa ni kifaa kikubwa cha ulinzi ambacho kinaufanisi mkubwa sana kikihudumiwa vizuri na kutumika vizuri. Ujuzi huu wa kutumia mbwa niliupata kwa mfugaji kuku mwanamama ambaye ndiye aliyeniuzia kuku wa mbegu.
Mazingira yake ya kufugia yalifanana na mazingira yangu, alikuwa amepakana na eneo lenye uwazi kubwa sana amabako kuku walikuwa wakisambaa na kwenda mbali sana. Kulikuwa na points mbili ambako ndiko huko maadui wengi walikuwa wakiingilia kuleta midomo yao kuvizia kuku. Huyu mfugaji alinisimulia mbinu yake akijiamini bila mashaka ambapo nami niliichukua na kuitumia na kuleta mafanikio makubwa.
Kwa hiyo mfugaji huyo mwanamama shupavu alikuwa amefuga mbwa watatu tu wenye maumbile ya kawaida ya mbwa wetu wa kiswahili. Mbwa wawili kila mmoja alimfunga aliwafunga kwenye kivuli kwenye zile points ambako ndiyo huijia maadui! Kama nilivyosema yeye kwa jiographia ya eneo lake alikuwa ametambua sehemu mbili kuu ambako ndiko huko vicheche, mbwa koko, paka n.k walikuwa wakiingilia eneo wanakochungia kuku.
Mbwa mwingine wa tatu yeye alikuwa anamwacha free kuzunguka huku na kule. Kwa hiyo alikuwa amewafundisha kwamba inapotokea................. INAENDELEA