Kubota; mbwa wangu wanakula kuku tatizo nini? unawapa dawa gani ya kuwafanya wakae kwenye lindo wasizulure usiku?
Mkuu umenivunja mbavu zangu natamani ungeniona. Kwamba mbwa anakula kuku na hakai kwenye lindo! Mkuu Ibra6 mbwa nao wako wa kila sampuli na tabia pia. Kunajambo moja naomba uelewe hapa, mimi niliwahi kustajaabu sana kuku wangu kutokuzurula acha mbwa! Nilikuwa naona jinsi kuku wa majirani walikuwa wakienda miji ya mbali kuzurula na wengi walikuwa wanashinda nyumbani kwangu na kuchangia kutaga kwenye viota vyangu. Kuku walikuwa hawazuruli kabisa na ndivyo walivyokuwa mbwa wangu! Kama mbwa ukimpenda, kumjali na kumpa chakula kizuri na akashiba kabisa mbwa anajua kujipendekeza kwa Master wake hakuna mfano!! Mbwa si rahisi kukuangusha eti akazurule usiku? mimi haijanitokea!
Ufugaji mwingi wa kiswahili wa kuku na mbwa ni wa kuwaacha viumbe kujitafutia wenyewe. Mbwa wana akili, wakishaona nyumbani wao ni kupigwa tu na kupewa mabaki ya chakula wasishibe vizuri nafasi yao nzuri kushiba ni usiku kuzurula kuokoteza. Ili kuhakikisha mbwa wako hazuruli mchana na usiku anza kwanza kuhakikisha wanapata balanced diet. Wasagie dona, nunua dagaa, ugali mseto na dagaa! Mimi siyo mtaalamu wa mbwa ni uzoefu tu. Nakumbuka nikiwa mdogo kwetu mbwa alikatiwa ugali au alipikiwa ugali wa pumba, chakula cha aina hii humshibisha tumbo tu lakini ki afya hakina ukamilifu hapo mbwa lazima azurule kujazia lishe. Mbwa wako akishiba hatawinda kuku wako na wala hatazurula usiku. Hiki kitu kinaitwa protein ni muhimu sana kwa mifugo, tusikazanie kuwalisha mifugo wetu vyakula vya wanga pekee!
Njia nyingine ya kuzuia mbwa asizurule usiku ni kufuga dume na jike. Ukiwa na jike unanafasi kubwa ya kupata msaada wa walinzi kutokana na wachumba watakaokuwa nanakuja kumendea jike.
Njia nyingine ambayo sina uthibitisho wa kitaalamu ila kwa hisia zangu nadhani kumfungia mbwa mchana ili asizurule yaweza kusaidia kupunguza uzurulaji wakati wa usiku. Mbwa wangu wanaminyororo, mchana huwafunga kwenye kivuli. Mbwa anapokuwa hazuruli sana anakuwa hana uenyeji sana na hana mbwa marafiki wa kuwatembelea usiku! Ni hisia zangu lakini. Kama tulivyowatu wanyama nao wako hivyo hivyo.
Pia njia nyingine nzuri ni ya kununua mbwa watoto unawakuza mwenyewe, mbwa wanapokulia kwako ukawalisha na kuwafuatilia matunzo vizuri mbwa hujua hadi unayowazia maana wamekulia kwako wanakufahamu vema kuliko unavyozania, mimi mbwa wangu nikikaribia nyumbani hunikimbilia! Sijawahi kuwavutisha bangi wala madawa yoyote lakini mbwa wangu wamevuma mtaani kwamba ni wakali hakuna mfano! Haya mambo yananifanya nashangaa sana!! Jamani unachoipa dunia hii ndiyo hicho hicho dunia itakurudishia! Kama umamtunza vema mbwa wako lakini anakutia maudhi piga bei ujue ni hajatulia huyo na mbwa wapo wa hivyo.
Naomba nimalizie hapa kwa kusema kwamba nilishashikwa na mshangao sana lakini mwishowe nilielewa ni kwa nini. Tunapokula chakula nyumbani kwangu ni mimi tu huwa nasumbuliwa sana na paka wetu, akitaka nimpe chakula na hata kupanda miguuni kwangu kwa kujiamini, wenzangu huona paka ni msumbufu humpiga au kumkamata na kumfungia sehemu, mimi huwa natambua huyu ni mnyama anaenitegemea, akililia chakula mara moja lazima nimkatie msosi wa nguvu, kwa kufanya hivi nimejenga urafiki wa ajabu na mifugo, nimeshuhudia paka akiwakimbia baadhi ya member wa nyumbani kwangu kila anapowaona, mbwa wangu pia ni hivyo hivyo, nikifungua mlango asubuhi mbwa wapo kunirukia rukia, wengine wanasema paka ukimpa msosi hakamati panya wanasahau kuwa kunawakati panya huwa wajanja kiasi kwamba paka huwa haambui kitu! Matokeo yake paka anabadilika tabia anaanza kula vifaranga!
Samahani Mkuu kwa maelezo marefu sana hii ni hulka yangu sikujaliwa kuwa na maneno mafupi nivumilieni tu.