Ufugaji wa Kuku wa Kienyeji na Masoko yake

Ufugaji wa Kuku wa Kienyeji na Masoko yake

Wakuu Kubota, Mama Joe, asigwa, Chasha na wengine naombeni mwongozo (mambo ya kuzingatia) nikitaka kununua incubator, nahisi nitaihitaji muda si mrefu. Ila sasa nachanganyikia ipi ninunue! kwa mawazo niliyopata humu so far ni kwamba nzuri ni automatic, sasa kimbembe hizo automatic zenyewe zipo za kumwaga! nimesikia kuna za china, Uk etc, wengine wanaenda mbali zaidi wanadai za chini usinunue, wakati huo huo tunaambiwa vitu vingi vibovu na imara vinatokea huko huko china. Kifupi kwa sisi tusio na ufahamu nzuri wa hizi mashine tunazidi kuchanganyikiwa!

Haya, hapo hapo bado nasikia zinatofautiana uwezo sijui ukubwa, manake nimesikia mdau anatangaza anazo za UK za mayai 64 na mayai 176 kama sikosei, cha ajabu baadhi ya wadau akiwemo Mama Joe akahitaji ya mayai 200 au 300, hapo hapo kuna mdau ameibuka anataka ya 540 daah! mi hapo ni kuchanganyikiwa kwa kwenda mbele.....!!

Wakuu mwenye uzoefu na hizi mashine atudondoshee ABC zake namna ya kupata kitu bora, hata kama unajua point moja tu ya kuzingatia we tumwagie hapa, tukiunganishe na za wengine tutapata kitu kamili, si mnajua hela zenyewe hizi za kudunduliza au mkopo halafu tena uingie mkenge, umejinyima weeee unaishia kununua incubator ya ovyo, inabuma baada ya muda tu au inashindwa kabisa kutoa matokeo mazuri, si tutapata pressure bure aisee!!!

Mkuu kwa masuala ya incubator mkuu Chasha NI MZURI SANA, ana uzi wake unazungumiza sana hili, hebu utafute au mtafute mwenyewe anakupa details nzuri sana...
 
Last edited by a moderator:
Kubota come this way please! Mito sisi wengine tupo kama wewe tunapapasa tu hatujui kipi ni bora zaidi ila kifupi ninachojua ni namba ya mayai inayotajwa ni uwezo wa incubator kutotoa vifaranga idadi hiyo kwa pamoja. Sasa ndio maana nimeuliza walau ya 200-300 maana hata kwa matumizi binafsi kulea vifaranga 50 sioni kama ni faida ugharamie chanjo chakula utunzaji nk karibia miezi 6 hela haitarudi kwa kweli. N pia baadae waweza wasaidia wengine au kuamua kuuza vifaranga napoa kupata wateja wa hizo namba itakuwa shida. Kumbuka na umeme wetu itakugharimu generator iwashwe walau mara kwa mara ktk siku 21. Naomba wengine watachangia kiasi cha joto, unyevu na uanguaji (hatching) bado navisoma taratibu. Mkuu Kubota tuwekee hapa hayo material.
 
New mzalendo Nitafute nikupe ushauri mambo ni mengi pia mimi ni mfugaji wa kuku wa kienyeji soko lipo kubwa sana unatakiwa tu kujua undani wake. But it seems you are not serious hako kajogoo kamoja utafika nako weapi au unaogopa risk? nipigie 0755394701 tuongee mkuu

Utaniwia radhi na mimi nitakutafuta kwani nina Interest na ufugaji kuku wa kienyeji.Ninajaribu kufanya cross breed na kuku wa kisasa nione nitaongezaje uzalishaji wa mayai na kuku wenyewe.
 
mkuu mm eneo langu huwa naogopa wezi maana mitaa ya uswahilini bana nomaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa
Umeongea kweli kabisa Mkuu. Wezi ni kikwazo kikubwa kabisa kwa ufugaji na shughuri nyingi za maendeleo. Maeneo ya uswahilini yenye msongamano mkubwa wa makazi ni vigumu kufanya mradi wa ufugaji wowote kwa usalama. Inahitaji kuwa kwenye eneo la pembezoni au low density area.
 
Kubota nilianza na kuku 30 niliwapa chanjo. Umepita ugonjwa nimebakiwa na kuku sita nimekosa raha kbsa.
Changamoto ni nyingi Mkuu Kubota.
 
Last edited by a moderator:
Sikuwai kufikiria lakini kupitia hii thread nimepata elimu ya kutosha na wazo la kujipanga siku za mbeleni nianzishe kilimo cha ufugaji kuku. Asanteni wote mlio toa mawazo yenu na michango yenu.
 
Kubota uweke na picha tuone mabanda yako na kuku wako
"Vox popoli vox dei"
 
Kubota nilianza na kuku 30 niliwapa chanjo. Umepita ugonjwa nimebakiwa na kuku sita nimekosa raha kbsa.
Changamoto ni nyingi Mkuu Kubota.

Mkuu Kwemisaa kama umeshasoma story yangu yote mimi pia nilipitia changamoto hizo. Isikukatishe tamaa kabisa, hilo ni darasa la muhimu wewe kupitia. Bila matatizo hayo hutaweza kujua ufugaji. Ndiyo maana tunashauriwa unapoanza mradi ambao hujawahi kufanya ni vema ukaanza na kidogo ili ujifunze na ukue kwa kujipanua kadri unavyozidi kujiamini. Kuhusu chanjo ni kwamba kama chanjo ni nzima na imetumika ipasavyo huwa ni kinga madhubuti. Lakini tunatatizo la uchakachuaji ambapo chanjo zingine huwa ama ni feki au zilisha-expire lakini huwezi kuzigundua kwa macho! Kwa kujihami ni vema kuku wapya ukawachanja japo mara tatu mfululizo kwa kununua dawa toka vyanzo tofauti. Na ikibidi kutumia dawa aina zote za maji na za matone. Tutafanyaje hakuna jinsi, hata kwenye madawa ya mboga mboga mbinu ni hizo hizo ukikalia dawa aina moja toka source moja ni sawa na kubeba mayai kwenye kikapu kimoja. Akili mu kichwa. Kuhusu kupukutika kwa kuku wako tafuta ujue chanzo cha tatizo ili lisijirudie tena. Je walikuwa ni vifaranga, je chanjo ilikuwa ya kudhibiti ugonjwa gani, na unadhani kuku walikufa kwa ugonjwa gani. Pole mkuu ila sasa safari ya ufugaji ndiyo inaanza, simama usikate tamaa!
 
Kubota uweke na picha tuone mabanda yako na kuku wako
"Vox popoli vox dei"
Mkuu Adharusi, kwenye thread hii kuna picha nimepost na mabanda hadi picha ya mbwa. Nadhani tufanye utaratibu uje ujionee mwenyewe shambani kwangu. Mkuu hii kitu "Vox popoli vox dei" tafsiri yake ni nini sijapata ujumbe wa hicho kipogolo, msaada tutani please!!
 
Mkuu Kwemisaa kama umeshasoma story yangu yote mimi pia nilipitia changamoto hizo. Isikukatishe tamaa kabisa, hilo ni darasa la muhimu
wewe kupitia. Bila matatizo hayo hutaweza kujua ufugaji. Ndiyo maana tunashauriwa unapoanza mradi ambao hujawahi kufanya ni vema ukaanza na kidogo ili ujifunze na ukue kwa kujipanua kadri unavyozidi kujiamini. Kuhusu chanjo ni kwamba kama chanjo ni nzima na imetumika ipasavyo huwa ni kinga madhubuti. Lakini tunatatizo la uchakachuaji ambapo chanjo zingine huwa ama ni feki au zilisha-expire lakini huwezi kuzigundua kwa macho! Kwa kujihami ni vema kuku wapya ukawachanja japo mara tatu mfululizo kwa kununua dawa toka vyanzo tofauti. Na ikibidi kutumia dawa aina zote za maji na za matone. Tutafanyaje hakuna jinsi, hata kwenye madawa ya mboga mboga mbinu ni hizo hizo ukikalia dawa aina moja toka source moja ni sawa na kubeba mayai kwenye kikapu kimoja. Akili mu kichwa. Kuhusu kupukutika kwa kuku wako tafuta ujue chanzo cha tatizo ili lisijirudie tena. Je walikuwa ni vifaranga, je chanjo ilikuwa ya kudhibiti ugonjwa gani, na unadhani kuku walikufa kwa ugonjwa gani. Pole mkuu ila sasa safari ya ufugaji ndiyo inaanza, simama usikate tamaa!

Mkuu mimi nafuga hao kuku wa kienyeji natotoresha kwa incubeta ya kienyeji tuuu.

Tatizo nilizalisha vifaranga 150 lakin wengi walikufa kwa umri mdogo kwa ugonjwa wa kutetemeka na miguu kukosa nguvu mwisho kufa wamebak km 30

Nilipokwenda duka la dawa walinipa dawa zifuatazo Esb3 30% zagro na gluklosi ya kuku,tatizo hazinisaidiii

nitumie dawa gani kwa ajili yao hao kuku mkuu msaada tafadhali.
Maana nimeanza tena kuzalisha
 
Mkuu mimi nafuga hao kuku wa kienyeji natotoresha kwa incubeta ya kienyeji tuuu.

Tatizo nilizalisha vifaranga 150 lakin wengi walikufa kwa umri mdogo kwa ugonjwa wa kutetemeka na miguu kukosa nguvu mwisho kufa wamebak km 30

Nilipokwenda duka la dawa walinipa dawa zifuatazo Esb3 30% zagro na gluklosi ya kuku,tatizo hazinisaidiii

nitumie dawa gani kwa ajili yao hao kuku mkuu msaada tafadhali.
Maana nimeanza tena kuzalisha

Mkuu hao vifaranga walikufa wakiwa na muda gani? Make kuna magonjwa mengi sana ya kuku na si yote yanajulikana, na some time wana rith magojwa kutoka kwa mama zao
 
Mkuu mimi nafuga hao kuku wa kienyeji natotoresha kwa incubeta ya kienyeji tuuu.

Tatizo nilizalisha vifaranga 150 lakin wengi walikufa kwa umri mdogo kwa ugonjwa wa kutetemeka na miguu kukosa nguvu mwisho kufa wamebak km 30

Nilipokwenda duka la dawa walinipa dawa zifuatazo Esb3 30% zagro na gluklosi ya kuku,tatizo hazinisaidiii

nitumie dawa gani kwa ajili yao hao kuku mkuu msaada tafadhali.
Maana nimeanza tena kuzalisha
Mkuu lazalaza pamoja na maswali ya Mkuu Chasha hapo juu pia hebu sema juu ya aina ya chakula ulichowalisha hao kuku! Je ulitengeneza mwenyewe? Au ulinunua kilichotengenezwa tayari? Je ni aina gani ya hicho chakula na nani manufacturer wake! Kabla hatujachukua darubini kuchunguza chanzo kilichopukutisha kuku wako naomba tujiridhishe kwanza kwenye aina ya lishe uliyokuwa ukiwapa. Ninahisi hawa kuku walikufa kwa utapiamlo! Matatizo ya kutetemeka miguu na hata kupooza hutokana na upungufu wa madini kwenye chakula. Nilishawahi simulia kuwa uduni wa lishe ni chanzo kikubwa cha matatizo mengi sana kwenye ukuzaji wa vifaranga. Tafadhari ukiwa muwazi utapata solution halisi, ukificha ukweli tatizo litabaki kwako mwenyewe. Wataalamu mtaongezea.
 
Mkuu lazalaza pamoja na maswali ya Mkuu Chasha hapo juu pia hebu sema juu ya aina ya chakula ulichowalisha hao kuku! Je ulitengeneza mwenyewe? A
u ulinunua kilichotengenezwa tayari? Je ni aina gani ya hicho chakula na nani manufacturer wake! Kabla hatujachukua darubini kuchunguza chanzo kilichopukutisha kuku wako naomba tujiridhishe kwanza kwenye aina ya lishe uliyokuwa ukiwapa. Ninahisi hawa kuku walikufa kwa utapiamlo! Matatizo ya kutetemeka miguu na hata kupooza hutokana na upungufu wa madini kwenye chakula. Nilishawahi simulia kuwa uduni wa lishe ni chanzo kikubwa cha matatizo mengi sana kwenye ukuzaji wa vifaranga. Tafadhari ukiwa muwazi utapata solution halisi, ukificha ukweli tatizo litabaki kwako mwenyewe. Wataalamu mtaongezea.

Muheshiwa sina sababu ya kuficha sababu naitaji kunufaika na huo mradi ndugu,ratiba yangu iko hivi

Nawatoa kwenye mashine baada ya siku tatu bila kuwapa chochote humo kwenye mashine.
Nikiwatoa huwa nawapa gluclose kwa masaa kuanzia asubuhi na baada ya hapo huwa nawapa chakula kinaitwa stata mpaka wakomee km wiki 2 nawapa pumba na dagaa mchanganiyko, Pia huwa na makoti Ndo hivyo mkuuu wangu nawakilisha
 
Mkuu hao vifaranga walikufa wakiwa na muda gani? Make kuna magonjwa mengi sana ya kuku na si yote yanajulikana, na some time wana rith magojwa kutoka kwa mama zao


Mkuu mara nying baada ya wiki mbili hiyo hali huwa inajitokeza, na kuku mama zao huwa nachukua mayai ya mama zao kwa ajili ya kutotoleshea vifaranga.asante
 
Asante mkuu kwa elimu,lkn naomba kujua dawa gani naweza kutumia mwanzo unapotaka kufuga kuku wa kienyeji ili kuepukana au kuwakinga na maradhi?
 
Muheshiwa sina sababu ya kuficha sababu naitaji kunufaika na huo mradi ndugu,ratiba yangu iko hivi

Nawatoa kwenye mashine baada ya siku tatu bila kuwapa chochote humo kwenye mashine.
Nikiwatoa huwa nawapa gluclose kwa masaa kuanzia asubuhi na baada ya hapo huwa nawapa chakula kinaitwa stata mpaka wakomee km wiki 2 nawapa pumba na dagaa mchanganiyko, Pia huwa na makoti Ndo hivyo mkuuu wangu nawakilisha
Mkuu hiyo stata kama iko standard unapaswa uwalishe hadi waote mnyoya ya ukubwa, yaani hadi manyoya ya kifaranga yatoweke, kipindi hicho huwa tunachukulia kifaranga kimevuka kipindi nyeti na kigumu. Nakushauri tafuta muda usome thread hii yote, nilipitia changamoto hiyo hiyo nikafanikiwa kuitatua na ndiyo chanzo cha kuanzisha thread hii! Kisha fuatilia kinga muhimu ya chanjo kwa vifaranga na madawa mengine. Mkuu nilipokusoma tu kuwa uliacha kuwapa stata baada ya wiki mbili, hili ni jibu tosha kuwa kinachokusumbua ni Lishe. Walishe hiyo stata mwezi mzima au hadi wiki 6 baada ya hapo unaweza kuwapatia chakula chako cha kutengeneza mwenyewe napo usiwabadilishie ghafla, anza kuchanganyia taratibu na hicho ulichotengeneza. Naomba utulie usome thread nzima upate maarifa, ufumbuzi wa tatizo lako ni kujifunza zaidi. Narudia tena soma Thread hii kuhusu changamoto nilizokutana nazo za lishe na magonjwa na ufumbuzi niliofikia itakupa mwanga zaidi.
 
Back
Top Bottom