newmzalendo
JF-Expert Member
- Mar 23, 2009
- 1,385
- 568
Je, faida za kuku wa nyama zikoje? Kuna mtu ameniambia faida ni 50%.i.e ukiweka vifaranga vya milioni moja,then tarajia faida ya laki 5.
Mimi nataka nianze na uzalishaji wa chakula cha mifugo,walio wahi kuzalisha chakula cha kuku naomba ushauri na jinsi ya kuanza.
Je faida za kuku wa nyama zikoje?kuna mtu ameniambia faida ni 50%.i.e ukiweka vifaranga vya milioni moja,then tarajia faida ya laki 5.
mimi nataka nianze na uzalishaji wa chakula cha mifugo,walio wahi kuzalisha chakula cha kuku naomba ushauri na jinsi ya kuanza.
Kwa wafugaji wa kuku humu ndani, naomba formula ya Growers Mesh, nataka kufanya mixing mwenyewe badala ya kununu chakula kilichotengenezwa tayari.
Msaada kwenye tuta please!!
Madaktari wa mifugo na Animal scientist nawaona humu lakini wanakunyamazia, mpeni hiyo formula msihofu makachero wa JF watawafanya nini?
Mkuu sijawahi kusikia kama formula za chakula cha mifugo huwa zinatolewa kienyeji! jaribu kumtafuta jamaa yako ambaye amesoma mambo ya mifugo atakusaidia, lakini kusema eti formula iwekwe hapa kweupe! Siyo rahisi maana hilo nalo ni deal la watu mkuu. Si unajua sasa hivi ni biashara kwa kwenda mbele! Hiyo nayo ni biashara (inaweza tolewa kwa mtindo wa consultancy na kukawa na malipo kidogo).
Ukienda kichwa kichwa ndugu utapewa formula zilizochakachuliwa halafu usipate mazao yanayotarajiwa!
Inaelekea wenzetu hawa wana kauchoyo fulani eh, Wafanye kama wale wataalam wa kompyuta kule kwenye jukwaa la teknolojia, jamaa hawanyimani ujuzi hata kidogo, utashindwa wewe tu.
Fuso kesho nitakupatia formula ninayo ila nimeiacha home, mi ndo ninayotumia nitaiweka kesho usikonde
Ifuatayo ni formula ninayoitumia wakati nikianza kuwapa growers mash na imekuwa ikinisaidia najua kila mfugaji ana namna yake ila hii ni ya kwangu
Kwa ton 1 ya chakula cha kuku
Mahindi kg 400
Dagaa kg 80
Chokaa kg 100
Mifupa kg 20
Alizeti kg 160
Chumvi kg 3
Premix kg 3
DCP kg 10
Pumba kg 240
Hapo utaweka na machine cost kwa kg ambayo ni kama shs 15 mpaka 20 kwa kg
Kabla hawajaanza kutaga wape chakula wale washibe mpaka wakianza kutaga ndo unawapa kwa kipimo na wakishiba miezi minne mpaka mitano tu utaona mayai kibao
Kila la kheri
Ifuatayo ni formula ninayoitumia wakati nikianza kuwapa growers mash na imekuwa ikinisaidia najua kila mfugaji ana namna yake ila hii ni ya kwangu
Kwa ton 1 ya chakula cha kuku
Mahindi kg 400
Dagaa kg 80
Chokaa kg 100
Mifupa kg 20
Alizeti kg 160
Chumvi kg 3
Premix kg 3
DCP kg 10
Pumba kg 240
Hapo utaweka na machine cost kwa kg ambayo ni kama shs 15 mpaka 20 kwa kg
Kabla hawajaanza kutaga wape chakula wale washibe mpaka wakianza kutaga ndo unawapa kwa kipimo na wakishiba miezi minne mpaka mitano tu utaona mayai kibao
Kila la kheri
Asante kwa mchanganuo wako! Nikipata nafasi nitajaribu kuuhakiki kama unakubaliana na formula za growers. Maana kuna kitu kinaitwa Crude Protein (CP) ni lazima kiendane na mahitaji ya growers vinginevyo utakuwa unawapa chakula kilichochakachuliwa ambayo madhara yake ni makubwa sana kwa kuku wa mayai. Hapa namaanisha kuwa unaweza kuwapa chakula cha kuwanenepesha kuliko kawaida na wakashindwa kukupa mazao tarajiwa au ukawapunja wakapata utapiamlo.