Ufugaji wa Kuku wa Kisasa: Fahamu Mbinu, Faida, Changamoto na Masoko

Ufugaji wa Kuku wa Kisasa: Fahamu Mbinu, Faida, Changamoto na Masoko

Sasa kila mtu akifanya biashara ya maduka nani atafuga kuku? Ndio maana bei ya mayai inapanda kila kukicha kwasababu watu wameikimbia hii biashara. Kama mtu anaushauri mzuri wa kufuga kuku plse atujuze wengine tuna interest

Hakuna biashara ambayo haina risk linalotakiwa kama mtu una nia ya kufuga kuku ni kupata uelewa wa ufugaji wenyewe, na kufuata taratibu zinazotakiwa ikiwemo ushauri wa kitalaam, kwa mfano wafugaji wengi wa kuku hupata hasara kwa sababu hawafuati viz
 
Kuku ni biashara nzuri sana lakini inabidi uwe mjanja, kwanza jifunze kutengeneza chakula cha kuku mwenyewe, usiwe unanunua. Pili usiwe mbahili. Hakikisha wanakula vizuri na madawa ya kupulizia kwenye mabanda unatumia. Anza na kuku 2000,
good luck.

Kaka mm nina uzoefu kaka, ila nakushauri kama una kazi usiiache kuku ni kizunguzungu mm nilifikia nafuga mpaka 500 ila faida ni ndogo sana na wanunuzi hao uliowataja ndo wanapanga bei bila kujali umetumia kiasi gani kuwakuza hao kuku, na ukijidai mjanja kutokuuza inakula kwako maana vijamaa vinakula ile mbaya ukichelewesha kuwauza kwa wiki moja kwa kujidai kusubiri bei nzuri inakula kwako, maana watakuwa wamekula pesa ambayo hutaweza kuifidia katika selling price. Kama una uzoefu fuga wa mayai, wa nyama kimeo.
 
Nimeanza majaribio ya ufugaji kuku wa kienyeji na vijogoo, lakini tatizo kubwa ninalolipata ni huu ugonjwa wa kushusha mabawa (kuvaa koti)Coccidiosis! Ninaweza kupata ushauri wa nini kinga na matibabu yake. Nawasilisha wakuu..

Pole sana, cocidiosis unazuiwa kwa kuhakikisha sakafu ya banda lako ni kavu, kwa tiba muone doc wa mifugo
 
Heshima wana JF,nataka kufuga kuku wa kisasa lakini sehemu nayotaka kwenda kufugia umeme haujafika bado naombeni njia nyengine ya kusolve tatizo la umeme.
 
Aidha nunua jenereta ama wekeza kwenye solar panels, tatizo ninaloliona ni kwa kutumia generator profit margin ni ndogo ama pengine utapata hasara kabisa kutokana na gharama za diesel/petroli.

Kama mradi wako ni mkubwa nahisi Solar panels inaweza kukupatia faida ila sio ya harakaharaka pengine baada ya miaka 2 ama zaidi.
 
Heshema wana JF, nataka kufuga kuku wa kisasa lakini sehemu nayotaka kwenda kufugia umeme haujafika bado naombeni njia nyengine ya kusolve tatizo la umeme.

ASANTE NDUGU GUTA.Mimi nilikuwa mfugaji wa kuku wa mayai na nyama.Unaweza kufuga bila umeme na mambo yakaenda kama kawaida.Zingatia nitakavyo kuelekeza.Kwanza unapopa vifaranga uviangalie kama vimejikunyata ndo unawasha chemri.Mara nyingi inakuwa wakati wa asubuhi.Ikishafika mchana unazima taa unaacha wapate mwanga wa jua kwa joto likizid ni hatari.

Pia kama joto ni dogo unaweza kuwasha jiko la mkaa na ukaliweka kwenye kona unayofugia mpaka uone vifaranga vimechangamka.Kwa kuku wa mayai hakikisha wanalala na taa mpaka wafikishe miezi miwili kwa usalama zaidi.Lakini wakishachangamka ndani ya mwezi mmoja uwe unawazimia taa mchana na usiku unawasha mpaka miezi miwili itimie.Kama una maulizo tuwasiliane ili nikutumie maelezo yanayoelekeza ufugaji bora wa kuku aina zote.KWA SASA NIPO DAR KWA MWANA JF MWENZETU KUNA BIASHARA TUNAFANYA HIVYO KAMA UNAWEZA KUONA NI VIZURI NIKAKUPA MAELEZO KWA KINA.USIOGOPE KUULIZA USIPOELEWA.
Asante.
 
Ndugu Tizo asante sana. Hata sisi tupo Dar, tunataka kufuga kuku so tunaweza kukuonaje tupate hizo detail info.
 
Wadau nimekuwa nikisikia tetesi kwamba utumiaji wa vidonge vya majira (family plan) katika uchanganyaji wa chakula cha kuku inasaidia kuwafanya kuku wapate uzito wa kutosha na kuwa na soko zuri. Maswali:

1. Je, hili jambo lipo au linatendeka kweli?
2. Kama linatendeka; Je, kuna uhusiano wowote wa kitaalamu katika kunenepesha kuku?
3. Kama linatendeka; Je, hakuna madhara yeyote kwa watumiaji au walaji wa kuku?


Naomba kuwasilisha.
 
Nimekuta mahali panauzwa mayai ambayo wanasema ni non-cholesterol na hupatikana kutoka katika kuku maalum wanaozalisha haya mayai.

Kuna anayejua wanafugwaje?
 
Nilinunua kigari na kufilisika kwa biashara hii hii
YES, kama ulifuga bila kufuata masharti na uangalizi wako ulikuwa duni nakubali hata nyumba ungeuza bora umeshituka mapema marytina. Sisi tunapeta tu na biashara hii hii.
 
Kuku ni biashara kichaa, nimekulia kwenye ufugaji nawajua mwanzo mwisho. Kama wataka biashara mbadala ya kuku nakushauri uanze totoresha vifaranga vya kuku. Nenda sido (karibu na airport) wapo jamaa wanatengeneza incubators. au ng'ombe wa maziwa.

Wacheni uongo bado wanafaida, ila wakiugua ndio noma nafuga kuku mie.
 
Wa DSM ebu nambien tray moja ya mayai kuku wa kisasa ni sh ngap? Na kienyeji ni sh ngapi, nitaingia apo muda si mrefu!
 
wa dsm ebu nambien tray moja ya mayai kuku wa kisasa ni sh ngap? na kienyeji ni sh ngapi, nitaingia apo muda si mrefu!
Tray moja ya kuku wa kisasa ni sh elfu 6,na ya wakienyeji ni elfu 7 na mia tano.hiyo ni bei ya jumla.
 
wa dsm ebu nambien tray moja ya mayai kuku wa kisasa ni sh ngap? na kienyeji ni sh ngapi, nitaingia apo muda si mrefu!
Tray moja ya mayai wa kuku wa kisasa ni sh elfu 6,na ya wakienyeji ni elfu 7 na mia tano.hiyo ni bei ya jumla.
 
Nipo Dar nataka nianze biashara hii ya kuku wa mayai ila nataka kijana mtaalam mwenye uzoefu naweza mpata wap? na maeneo mazuri ya kuweka banda ni wap nina plot bagamoyo kma heka 2 na plot ya "20 kwa 30" Goba panafaa kujenga banda la kuku 2000?

Ujenzi wa banda la kuku wa mayai (kuku 2000) linagarimu kiasi gani cha fedha? mchoro stracture yake naweza ipata wap la kisasa na economical! ntashukuru kwa majibu yenu.
 
Wadau naomba kuuliza,

Watalaam wa ufugaji kuku wa mayai. naomba kujua eti kwa vifaranga unapoviweka bandani, kwenye sakafu unatanguliza maranda au unaweka kwanza magazeti. nataka nijue namna ya kutengeneza chick bedding!!

Nitashukuru!!
 
Back
Top Bottom