Sawa mkuu lakini umesahau kutuwekea na gharama za kuwalea hao kuku kwa wiki 20 kabla hawajataga. Kwa maana hiyo kuku 2000 wanakula wastani wa gm 80 kwa siku, watakula kilo 160 sawa na mifuko 4 ya 50kg kwa siku, so mifuko 4 x Tsh33,000 x siku 150 = 19,800,000. Pia usisahau uliwanunua kwa Tsh 2200 kila mmoja, yaani 2000 x 2200 = 4,400,000, so kabla hujaanza kufuga kuku 2000 uwe na milioni 25 kibindoni, hapo hujapigia garama za banda, chanjo, madawa, vifaa n.k...
Mkuu, kuhusu chakula hesabu zako si sahihi sana, kifaranga hakili msosi sawa na kuku mkubwa, hebu cheki mchanganuo huu,
Hebu tuone hesabu hii:
Kuwanunua 2000 @2400 = 4,800,000/=
Chakula:
Mwezi wa kwanza (Wiki 0- 4) average kilo 75 kwa siku ( Mfuko mmoja na nusu hii ni Stater) @ 34,000 = 51,000 X 30 days =1,530,000/=
Mwezi wa pili ( Wiki ya 5 - 8) average kilo 100 kwa siku ( Mifuko miwili finisher) @ 34,000 = 2,040,000/=
Glower (wiki ya 9 - 11) siku 14, kila siku mifuko 3 @28,000 = 1,176,000/=
Glower (wiki ya 12 - 18) siku 42, kila siku mifuko 5 @28,000 = 5,880,000/=
Layers (wiki ya 19 -23) siku 28, kila siku mifuko 5 @32,000 = 4,480,000/=
------------------------
15,070,000
add Manunuzi 4,800,000
------------------------
19,870,000
-------------------------
Wiki ya 19 wataanza kutaga kidogo kidogo mpaka wiki ya 24 utaanza sales ya 50% ikiongezeka kadri siku zinavyosonga. Kwa hiyo mtu anayetaka kuanza ufugaji kwa kuku 2000 anahitaji mil 20,000,000/=. Ukiweka na gharama za banda na uendeshaji hadi waanze kutaga ni lazima uwe na 27m- 30million.
shughuli pevu hii, nashauri anayeanza, ni vyema basi aanze na kuku 500 then aongeze taratibu taratibu huku akijifunza challenges.