Ufugaji wa Kuku wa Kisasa: Fahamu Mbinu, Faida, Changamoto na Masoko

Ufugaji wa Kuku wa Kisasa: Fahamu Mbinu, Faida, Changamoto na Masoko

Kuna kitu kina nitatiza kidogo, kulingana na taarifa mbalimbali nazo pata ni kwamba kuku wanahitaji joto la kutosha na hewa safi. Je, unafanyaje hivi kwa pamoja bila kuwakosesha kimojawapo na kuwaletea athari za kiafya?
 
Re: Biashara ya kuku wa kisasa.

Ushauri uliopata ni mwingi ila jitahidi upate literature nyingi kadri iwezekanavyo; nenda pale wizarani kilimo wafuate ndiyo kazi yao kusaidia wafugaji, wasibweteke na sisi wananchi tusiwabweteshe! Wanapaswa kutupa utaalam wa ugani. Binafsi sikubaliani na hoja eti lazima uwe na uzoefu! Yule aliyeanza alipata wapi uzoefu? Uzoefu huletwa na uthubutu na kutenda!

Pamoja na yote uliyoambiwa, labda ungeamua kuanza na kuku wa kienyeji na ukawafuga kisasa zaidi, wanalipa hasa ukizingatia kuwa watu wengi siku hizi, baada ya kupata uelewa juu ya sababu mbalimbali za magonjwa mengi, wanataka vitu natural, siyo artficial kama hawa kuku wa kisasa!

Pale kanisani Mikocheni B kwa Mama Lwakatre, wana mafunzoya wajasiriamali kila Jumamosi. Hebu explore hiyo opportunity pia; naamini inaweza kukupa mwanga wa wapi pa kuanzia.

All the best guy!
 
Habar wana jamii!

Plz naomba msaada jinsi ya kutengeneza chick mash nakaa mbali na maduka ya chakula.
 
Wana jamii naomba msaada kwa wale wanaofuga kuku wa kisasa (broilers) mie kumbukumbu zao zinanipa shida japo faida napata lakini nashindwa kutenganisha hesabu za kila batch kwa kuwa ukianza na vifaranga wiki ya kwanza baada ya wiki mbili nachukua wengine tena na baada ya hapo kuku wa batch ya kwanza wanashirikiana chakula na madawa. Kwa wenzangu mliopiga hatua kwenye hili naomba mwanga.
Hakikisha kila bechi lina counter book yake au ukurasa na kila bechi liwe na jina au namba wake na hivyo
utaweza kuendesha ufugaji wako kwa faida inayojulikana.
 
Mwana mimi nilifuga kuku wa nyama mia tatu, bahati mbaya nilikuwa nafugia kwa ndugu yangu ambaye yeye ni mfanyakazi baada ya kuona wiki sita tu kuku tayari na nikatafuta market nikauza, basi yeye akatamani hiyo biashara afanye yeye, akaanza kufanya, kwa hiyo kwa ushauri kuwa wafanyakazi waendelee na kazi ni sawa halafu sisi tukimbizane na kuku na biashara zingine.
 
Shukrani kwa aliyeanzisha huu uzi, umenipa cha kuongeza kwenye business plan yangu
 
Mama Joe,

Asante kwa michango yako nakufuatilia nina mipango ya hiyo biashara nimechukua hiyo wibesite. Ubarikiwe sana.
 
Dr wa Ukweli .... ulifanikiwa kuanza mradi huu? plz nipatie information hii (ujenzi wa banda la kisasa, wapi napata ramani na garama zake zikoje ?) THAX

Sikufanya tena mkuu ninaye mtumikia alinihamisha mjini now nipo kusini mwa TZ naangalia ustarabu mwingine
 
Ndugu wana jamii forum, sasa ni wakati wa kuacha kulalamika, tunapaswa kujituma na kupiga kazi kwa bidii. Vijana graduates kutoka vyuo mbalimbali tuwaze zaidi kwenye kujiajiri kuliko kuajiriwa, kujiajiri kunatoa uhuru wa kufanya kazi na kutoa maamuzi binafsi tena kwa wakati. Kuajiriwa kimsingi hakuna tofauti na utumwa na kama utapiga hesabu vizuri utagundua kuwa kuajiriwa ni hasara na pia huzuia mtu kuitumia elimu yake ipasavyo hasa ukiajiriwa serikalini. Kwa wastaafu pia wana fursa ya kutumia mafao yao vyema kwenye miradi ya ufugaji.

Kwa kuanzia tu naruhusu kuulizwa maswali kutoka kwa wale wote wanaojihusisha na ufugaji wa kuku, kama kuna jambo lolote linasumbua na kutaka kupata ufafanuzi. Pia kwa wanaohitaji kuanzisha mradi wa ufugaji wa kuku,utotoreshaji wa vifaranga,biashara ya uchanganyaji na uuzaji wa vyakula vya kuku nk , kama watanzania tunaweza kusaidiana ili hatimae tuondokane na umasikini. Tukitaka kuyaona maendeleo ya kweli, kila mtu awe msaada kwa watu wengine kwa fani aliyesomea.

Pia kama una changamoto katika ufugaji wako wa kuku, mfano magonjwa, utagaji mdogo wa kuku ili hali hawana ugonjwa, michanganuo ya mradi wa ufugaji wa kuku nk nipigie simu namba 0767989713, 0715989713 na 0786989713 niko tayari kukusaidia kuhusu ufugaji wenye tija wa kuku wako na .

Karibuni kwa mjadala.
 
Muda sahihi wa kuwalisha kuku ni kuanzia saa mbili asubuhi mpaka watakapo maliza share yao kwa siku. Kiasi cha chakula (kgs) watakachokula mfano kuku 100, itategemea umri wao,hivyo ulitakiwa unipe umri wao katika wiki kwani kiwango cha chakula hubadirika kila wiki.
 
Ndugu Lweganwa, kiasi cha fedha kitakachohitajika itategemea na ukubwa wa mradi wako, yaani idadi ya kuku na uwepo wa mabanda ya kufugia. Kama mradi wako utahusu mpaka ujenzi wa mabanda dhahiri kiwango cha pesa nacho kitakuwa kikubwa. Pia itategemea aina ya kuku utakao wafuga kama ni wa nyama au mayai.
 
Ndugu wana jamii forum,ifike wakati tuache kulalamika, tujitume kwa bidii kufanya kazi kwani kazi ndio msingi wa maisha yetu.Vijana graduates kutoka vyuo mbalimbali tuwaze zaidi kwenye kujiajiri kuliko kuajiriwa,kuajilikiwa ni utumwa pia ni hasara kama utapiga vizuri hesabu zako.Kwa wastaafu pia wana fursa ya kutumia mafao yao vyema kwenye miradi ya ufugaji.

Kwa kuanzia tu naruhusu kuulizwa maswali kutoka kwa wale wote wanaojihusisha na ufugaji wa kuku, kama kuna jambo lolote linasumbua na kutaka kupata ufafanuzi .Pia kwa wanaohitaji kuanzisha mradi wa ufugaji wa kuku,utotoreshaji wa vifaranga,biashara ya uchanganyaji na uuzaji wa vyakula vya kuku nk ,kama watanzania tunaweza kusaidiana ili hatimae tuondokane na umasikini.Kila mtu awe msaada kwa watu wengine kwa fani aliyesomea.

Karibuni kwa mjadala.
Mie naomba uzoefu wako tu kwa ufupi. Hasa Changamoto na Masoko.
Na kwa beginner unanishauri nianze na kuku wangapi/au mtaji Sh ngapi?
Na je ninaweza kuwa na mifugo mingi katika eneo moja e.g kuku, nguruwe, mbuzi (hasa kwa suala la maambukizo ya magonjwa)
 
Mimi nahitaji kufuga kuku wa kinyeji nyumbani(sio shamba)kwa kuanzia vifaranga wasiozidi 50. Nina mabanda madogo tayari ila

1. Sijui wapi pa kupata vifaranga vizuri vuya kienyeji ambao wakitaga watakua na uwezo wa kuatamia mayai na kuangua wakaongezeka
2. Risks za kufuga hao kuku tukiacha wizi. Yaani magonjwa kama kuna yasiyotibika au vipi maana sina uzoefu na ufugaji
 
Pia naomba kama hutajali na upo kwa ajili ya kusaidia ukubali kukutana na wafugaji wanaoanza (mimi mmojawapo)ili tuelekezane na kuuliza maswali na hata kutembelea mabanda ya wafugaji walioendelea if possible.
 
Nianze nawe ndugu yangu Zion Daughter, kwanza umeuliza uzoefu wangu kwa ufupi hasa changamoto na masoko. Kwa upande wa changamoto ni kwamba wafugaji wengi wa kuku hushindwa kuyatambua magonjwa mbalimbali ya kuku pale yanapotokea hali inayopelekea kuku wengi kufa kwa magonjwa. Kujua ugonjwa inamsaidia mfugaji kuchagua dawa sahihi. Endapo kuku watapatiwa dawa sahihi hupona haraka kama walipata maambukizo ya ugonjwa. Changamoto nyingine ni ughali wa chakula cha kuku hasa kutokana na kucompete na binaadamu.

Na kuhusu masoko, kiukweli soko la kuku sio tatizo.Demand ya kuku pamoja na mayai ni kubwa sana kuliko uzalisha uliopo. Kuhusu kukushauri uanze na kuku wangapi au mtaji shilingi ngapi hapo itabidi kwanza uniambie unahitaji kufaga kuku wa aina gani, maana kuna kuku wa nyama wa kisasa (Broilers), kuna kuku wa mayai wa kisasa (Layers), pia kuna kuku machotara na kuku wa kienyeji kwa ajili ya nyama na mayai. Na kwa wale wanaotaka kuanzishisha mradi wa utotoreshaji wa kuku watahitaji kuwa na kuku wazazi yaani Parent stock. Pia uniambie aina ya ufugaji mfano ufugaji huria, nusu kuria au wa ndani bila kuku kutoka.

Suala la ufagaji wa kuku kuchanganya na mifugo mingine kama ulivyo ainisha kwenye swali lako inaruhusiwa ilaa ni kwa kuku wa kienyeji hasa wanaofugwa huria. Kinyesi cha mifugo mfano mbuzi, ng'ombe nk husaidia kutengeneza funza ambao ni chakula kizuri kwa kuku.
 
Ndugu wana jamii forum,ifike wakati tuache kulalamika, tujitume kwa bidii kufanya kazi kwani kazi ndio msingi wa maisha yetu....
Karibuni kwa mjadala.
kichwa mbovu na wengine,

Nafikiria kufanya mradi mkubwa kiasi wa kuku wa mayai na/au wa nyama (layers na broilers) - nafikiria cycles za kuku elfu 5 mpaka 10 hivi. Ninalo eneo (shamba) kubwa tayari kwa shughuli hiyo. Lakini kwanza natafuta mtu mwenye uzoefu (wa ufugaji wa kibiashara) na ambaye anaweza kunisaidia kufanya feasibility study ya mradi huo.

Je, unaweza kunisaidia kazi hiyo? Unahitaji taarifa gani kutoka kwangu ili kufanya kazi hiyo kwa ufanisi? Au kuna mtu/kampuni unafahamu wanaweza kufanya kazi hiyo kwa ufanisi? Eneo la mradi lipo Dar, lakini nipo flexible kama mtaalamu atashauri nitafute eneo jingine - ili mradi prospects za kupata faida na sustainability ziwe za uahakika wa kuridhisha.
 
Ndugu yangu Da pretty,Sehemu ya kupata vifaranga wa kienyeji wenye uwezo wa kuatamia na kutotoa si shida hata ukitaka idadi zaidi ya hapo utapata.Kitu cha msingi unaweza ukatafuta namna ya kuwasiliana nami nitakuongoza.

Kuhusu risks ukiacha wizi kama ulivyosema ni kuwa,mara nyingi matatizo ya kuku ni magonjwa. Magonjwa ambayo ni common kwa kuku wa kienyeji ni pamoja na Kideri/mdondo hauna tiba ina chanjo, mafua yana tiba, ndui (fowl pox) nayo haina tiba ila ina chanjo, kipindupindu cha kuku (fowl cholera) ina tiba,Taifodi(fowl typoid) una tiba, Coccidiosis, una tiba pamoja ugonjwa wa homa ya matumbo kwa vifaranga(Pullorum), unatibika.

Kuhusu kutembelea wafugaji hiyo haina shida mara nyingi huwa nafanya hivyo kwa wafugaji wanaonza mradi na wale wenye matatizo, na pia wale wafugaji niliowaanzishia miradi ya ufugaji wa kuku huwa nafanya hivyo katka hali ya kuwasaidia.
 
Back
Top Bottom