Ufugaji wa Kuku wa Kisasa: Fahamu Mbinu, Faida, Changamoto na Masoko

Ufugaji wa Kuku wa Kisasa: Fahamu Mbinu, Faida, Changamoto na Masoko

Je, faida za kuku wa nyama zikoje? Kuna mtu ameniambia faida ni 50%.i.e ukiweka vifaranga vya milioni moja, then tarajia faida ya laki 5.

Mimi nataka nianze na uzalishaji wa chakula cha mifugo, walio wahi kuzalisha chakula cha kuku naomba ushauri na jinsi ya kuanza.
 
Je, faida za kuku wa nyama zikoje? Kuna mtu ameniambia faida ni 50%.i.e ukiweka vifaranga vya milioni moja,then tarajia faida ya laki 5.

Mimi nataka nianze na uzalishaji wa chakula cha mifugo,walio wahi kuzalisha chakula cha kuku naomba ushauri na jinsi ya kuanza.

Ni wazo zuri lazima uwe na mashine ya uhakika na upate fomla ya utengenezaji broiler wana uchanganyaji wao na layers pia ukishapata fomla na ukawa mwaminifu kwenye vipimo utapata wateja tu.
 
Je faida za kuku wa nyama zikoje?kuna mtu ameniambia faida ni 50%.i.e ukiweka vifaranga vya milioni moja,then tarajia faida ya laki 5.

mimi nataka nianze na uzalishaji wa chakula cha mifugo,walio wahi kuzalisha chakula cha kuku naomba ushauri na jinsi ya kuanza.

YES ni wazo zuri sana, ku deal na mifugo kuna risk zake lakini kama wewe ukijikita kwenye uzalishaji wa vyakula vya mifugo ni poa sana ila inahitaji mtaji mkubwa.

Kwa mfano utahitaji materials toka mikoani eg dagaa, mahindi, mashudu, pumba nk ambapo average kwa kunza lazima utengeneze tani zaidi ya 50 kwa mwezi.

Mimi nitaanza kutengeneza chakula cha kuku wangu mwenyewe (Layers) ili kupata super profit. nitajikita mikoani pia kukusanya materials.
 
Kwa wafugaji wa kuku humu ndani, naomba formula ya Growers Mesh, nataka kufanya mixing mwenyewe badala ya kununu chakula kilichotengenezwa tayari.

Msaada kwenye tuta please!!
 
Kwa wafugaji wa kuku humu ndani, naomba formula ya Growers Mesh, nataka kufanya mixing mwenyewe badala ya kununu chakula kilichotengenezwa tayari.

Msaada kwenye tuta please!!

Madaktari wa mifugo na Animal scientist nawaona humu lakini wanakunyamazia, mpeni hiyo formula msihofu makachero wa JF watawafanya nini?
 
Madaktari wa mifugo na Animal scientist nawaona humu lakini wanakunyamazia, mpeni hiyo formula msihofu makachero wa JF watawafanya nini?

Mkuu sijawahi kusikia kama formula za chakula cha mifugo huwa zinatolewa kienyeji! jaribu kumtafuta jamaa yako ambaye amesoma mambo ya mifugo atakusaidia, lakini kusema eti formula iwekwe hapa kweupe! Siyo rahisi maana hilo nalo ni deal la watu mkuu. Si unajua sasa hivi ni biashara kwa kwenda mbele! Hiyo nayo ni biashara (inaweza tolewa kwa mtindo wa consultancy na kukawa na malipo kidogo).

Ukienda kichwa kichwa ndugu utapewa formula zilizochakachuliwa halafu usipate mazao yanayotarajiwa!
 
Inaelekea wenzetu hawa wana kauchoyo fulani eh, wafanye kama wale wataalam wa kompyuta kule kwenye jukwaa la teknolojia, jamaa hawanyimani ujuzi hata kidogo, utashindwa wewe tu.
 
Fuso kesho nitakupatia formula ninayo ila nimeiacha home, mi ndo ninayotumia nitaiweka kesho usikonde.
 
Inaelekea wenzetu hawa wana kauchoyo fulani eh, Wafanye kama wale wataalam wa kompyuta kule kwenye jukwaa la teknolojia, jamaa hawanyimani ujuzi hata kidogo, utashindwa wewe tu.

Si utani wale ndiyo wasomi wa kweli, Saa yoyote unapata kitu unachohitaji.
 
Na mimi naiomba wazee maana ujasiri wa mali ni muhimu kwa maisha ya leo. Kama inawezekana naomba unitumie kwa mail yangu hii: yonahphares @yahoo.com

Nitashukuru sana wana JF kwa mambo yenu mazuri haya.
 
Ifuatayo ni formula ninayoitumia wakati nikianza kuwapa growers mash na imekuwa ikinisaidia najua kila mfugaji ana namna yake ila hii ni ya kwangu

Kwa ton 1 ya chakula cha kuku

Mahindi kg 400
Dagaa kg 80
Chokaa kg 100
Mifupa kg 20
Alizeti kg 160
Chumvi kg 3
Premix kg 3
DCP kg 10
Pumba kg 240
Hapo utaweka na machine cost kwa kg ambayo ni kama shs 15 mpaka 20 kwa kg

Kabla hawajaanza kutaga wape chakula wale washibe mpaka wakianza kutaga ndo unawapa kwa kipimo na wakishiba miezi minne mpaka mitano tu utaona mayai kibao

Kila la kheri
 
Mkuu ubarikiwe sana, hii ndiyo faida ya JF. Tutazidi kuwasiliana ngoja niifanyie kazi hii formula Jmosi.
 
Ifuatayo ni formula ninayoitumia wakati nikianza kuwapa growers mash na imekuwa ikinisaidia najua kila mfugaji ana namna yake ila hii ni ya kwangu

Kwa ton 1 ya chakula cha kuku

Mahindi kg 400
Dagaa kg 80
Chokaa kg 100
Mifupa kg 20
Alizeti kg 160
Chumvi kg 3
Premix kg 3
DCP kg 10
Pumba kg 240
Hapo utaweka na machine cost kwa kg ambayo ni kama shs 15 mpaka 20 kwa kg

Kabla hawajaanza kutaga wape chakula wale washibe mpaka wakianza kutaga ndo unawapa kwa kipimo na wakishiba miezi minne mpaka mitano tu utaona mayai kibao

Kila la kheri

Asante kwa mchanganuo wako! Nikipata nafasi nitajaribu kuuhakiki kama unakubaliana na formula za growers. Maana kuna kitu kinaitwa Crude Protein (CP) ni lazima kiendane na mahitaji ya growers vinginevyo utakuwa unawapa chakula kilichochakachuliwa ambayo madhara yake ni makubwa sana kwa kuku wa mayai. Hapa namaanisha kuwa unaweza kuwapa chakula cha kuwanenepesha kuliko kawaida na wakashindwa kukupa mazao tarajiwa au ukawapunja wakapata utapiamlo.
 
Mzee hebu lifanyie kazi hilo then utujulishe.
 
Habari zenu mabibi na mabwana.

Jamani nna ombi moja naomba mnisaidie,ni kwamba nimeamua kujivua gamba la umasikini na kuplan kufuga kuku wa mayai kwenye eneo langu la robo eka mitaa ya mbezi mwisho lakini tatizo ni kwamba mimi sikai huko.

Nataka nijenge tu mabanda afu niweke mtu wa kukaa huko sasa tatizo linakuja sijawai kufanya hii kitu hivo nahofia security naomba kwa wale wenye uzoefu na hii kazi ni security features zipi natakiwa niweke ili nikilala usiku niwe na amani na hiki ki project changu.

Michango yenu tafadhali.
Nawakilisha
 
Mkuu, take my words. Fuga kuku wa mayai utapata faida. Security ni mtu utakayemweka hapo awe mwaminifu

All the best
 
Mradi wa kuku wa mayai ni mzuri, but note the following:

- Kuku wanahitaji uangalizi wa karibu sana, ni muhimu mtu anayemweka awe mwaminifu na awe serious na kazi hiyo

- msimamizi wa banda lako ni muhimu awe na upendo kwa kuku kwani itakuwa rahisi kwake kutambua tatizo lolote watakalopata. Kumbuka sio suala tu la mtu kuweka chakula na maji na kuondoka

- Pata elimu ya magonjwa ya kuku, kinga na matibabu. Elimu hiyo mpatie pia msimamizi wa banda

- Hakikisha wakati wote una hela ya akiba kwa ajili ya madawa. Ni kosa kubwa sana kuku wakianza kuugua halafu hauna hela ya kuwahudumia
 
  • Thanks
Reactions: LAT
Changamoto kubwa sana kwa ufugaji wa sasa (hasa Dar) ni pamoja na

(1) Kuuziwa vyakula visivyokidhi viwango, hivyo kuathiri utagaji na afya ya kuku - wengine hadi huamua kujisagishia chakula chao wenyewe
(2) Madawa na chanjo feki au vilivyoexpire - hivyo watu hujikuta wakitibu kuku bila mafanikio
(3) Baadhi ya source za vifaranga hawatimizi yote yapasayo, - mfano kutokutoa chanjo za magonjwa kama Maleks
(4) Uangalizi makini wa kuku - na hasa mhudumiaji anapokuwa mwajiriwa asiye na usimamizi wa kila siku, bila kusahau uaminifu kwa idadi ya mayai yanayookotwa

Lengo la comment hii sio kukuogofya bali kukupa taarifa nyingi iwezekanavyo za kukuwezesha kufuga vema!
 
Back
Top Bottom