Aman Ng'oma
JF-Expert Member
- Nov 8, 2011
- 961
- 533
Inategemea unataka incubator za kutoka wapi,hapa hapa nchini au nje ya nchiNapenda kufahamu bei za incubator kuanzia ya mayai 100
mpaka 500.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Inategemea unataka incubator za kutoka wapi,hapa hapa nchini au nje ya nchiNapenda kufahamu bei za incubator kuanzia ya mayai 100
mpaka 500.
Inategemea unataka incubator za kutoka wapi, hapa hapa nchini au nje ya nchi
Well said, ni sawa kabisa, kujifunzia unaweza anza na cha kununua, ila faida hamna, tengeneza chakula mwenyewe, hakikisha usafi wa vyombo na banda, zuia ubichi bandani, hakikisha wakiumwa tu, watenge ukianza kusitasita ndo anavyosema huyo banda zima linakwisha.
Unaweza fuga kiasi chochote ila as a precaution nakushauri weka 200 banda moja kwa kuanzia ila pata ushauri wa vipimo per sq mita.
Kuhusu utagaji kuna dawa maalam za kuwapa ili kuwabust na kuwafanya waongoze kutaga, zaidi tunaweza kuwasiliana kwa msaada zaidi.Kuhusu kuharibu mayai, ni kutokana na kutotibiwa.Ni muhimu mayai kutibiwa kabla kuku hajaanza kuyaatamia.Mimi naona unisaidie ushauri nina kuku wangu chotara mwanzon walikuwa wanataga vizur lakin kwa sasa ni kama hawatagi maana wanaweza taga mayai 10 au pungufu na nina kuku kama 80 hv. Halafu ikifikia kulalia hawa kuku wanalalia kweli maana nina wawili walilalia wakaangua vzur ila kama kuku wa5 hv waliharibu mayai wiki ya 2, tatizo ni nini? Natanguliza shukrani
Tuwasiliane mkuu,nanavyo.Ni pamphlects zinazotoa mwongozo wa ufugaji bora wa kuku wa kienyeji,chotara na wa kisasa.Ninatafuta vitabu au majarida yanayoelezea vizuri namna bora ya ufugaji wa kuku wa kienyeji, Je nitafute kitabu gani kizuri?
Ina maana hayo mayai yakitibiwa kama unavyosema kuku hawa wanao uwezo wa kuangua vifaranga kama ilivyo kwa kuku wa kienyeji kabisa? Na je hizo dawa za kuwa boost ili watage hazina madhara maana nakwepa kufuga kuku wa kisasa kwa sababu ya madawa.
Salari,hi! kichwa mbovu nilitaka kujua kama biashara ya mayai ya kuku wa kienyeji inalipa kwa hapa Tanzania.Nina plan za kufanya hii biashara on commercial basis.Na je unaposema kuku chotara inamaanisha bado mayai yake yatakuwa ni kama ya kuku wa kienyeji? kuna aina ya kuku inaitwa Longhorn inasemekana ni aina ya kuku wanaotaga mayai mengi zaidi duniani je hii ni aina ya kuku wa kienyeji kama sio ni aina gani ya kuku wa kienyeji wanaotaga mayai mengi zaidi nijuze tu hata kama wanapatikana nje ya Tanzania ilimradi tu wawe wa kienyeji maana ndio biashara ninayotaka kufanya kwa sasa.
Mkuu Kichwa, si kweli kwamba Kuku wa kienyeji wako Africa pekee, Bado hata baadhi ya Nchi za Ulaya wako wengi tu, Asia ndo usiseme, na Kuna Mbegu fulani ya kuku wa Kienyeji kutoka Israeli naifuatalia Kenya make niliambiwa wanapatikana huko so niko kwenye process za kuwanunua baadhi nione wako vipi
NAFASI INAYOHITAJIKA KWA KUKU 1000 WENYE RIKA TOFAUTI (MABANDA YA KUKU)
[TABLE="class: grid, width: 500, align: center"]
[TR]
[TD]RIKA[/TD]
[TD]CHICKS
VIFARANGA[/TD]
[TD]GROWERS
KUKU
WANAOKUWA[/TD]
[TD]LAYERS
KUKU
WANAOTAGA[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]UMRI
KTK
WIKI[/TD]
[TD]0-6[/TD]
[TD]7-20[/TD]
[TD]20-80[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]KUKU/ENEO LA
M[SUP]2 [/SUP]MOJA ZA MRABA[/TD]
[TD]12[/TD]
[TD]9[/TD]
[TD]6[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]M[SUP]2 [/SUP]ZINAZOHITAJIKA
/KUKU 1000
[/TD]
[TD]83.7M[SUP]2[/SUP][/TD]
[TD]111.2M[SUP]2[/SUP][/TD]
[TD]166.6M[SUP]2[/SUP][/TD]
[/TR]
[TR]
[TD][/TD]
[TD][/TD]
[TD][/TD]
[TD][/TD]
[/TR]
[/TABLE]
Eneo watakaloshinda kuku 1000 wakati wa mchana, ambao hufugwa ktk mfumo wa nusu huria ni mita za mraba 10,000 .Hii inamaana kwamba ,kuku mmoja anahitaji eneo lenye mita za mraba 10.Kuhusu utagaji kuku wa kienji hana sifa ya utagaji wa mayai mengi.Kuku wa kienyeji hutaga kwa mzunguko.Kila mzunguko mmoja hutaga hutaga wastani wa mayai 15 na kuanza kuatamia,kutotoa na kulea vifaranga.Mzunguko huo huchukua wastani wa kipindi cha miezi 4 hadi 6 .Hali hiyo hiyo humfanya atage mayai machache kati ya mayai 30 hadi 60 kwa mwaka ukilinganisha na kuku wa kisasa ambao hutaga mayai 270 hadi 300.
Kuku wa kienyeji ukitaka watage mayai mengi wasiruhusiwa kuatamia,kila mayai yanayotagwa yaokotwe na kuhifadhiwa na kama mfugaji atahitaji kutotoresha, kama kuna kuku wengi ,ni vyema ikatumika machine ili kuzalisha vifaranga wengi zaidi.Kuku wa kienyeji anapokuwa kwenye mzunguko wa utagaji,kila siku hutaga yai moja.
Mawasiliano yangu nimekutumia kwenye private message yako ya jf,nenda kwenye notification yako fungua utaona.
Tuwasiliane tu nitakupatia.
Kwa wanaohitaji kuku mcahotara kwa ajili ya mbegu,wanapatikana, wako 1600,wana umri wa miezi 5,wote wako rika moja.Kama utawachukua utakaa nao mwezi mmoja tu kisha wataanza kutaga.Utakuwa na uwezo wa kupata mayai mengi,bora na salama ambayo utayatumia kuzalisha vifaranga kwa njia ya mashine.Pia wana uwezo wa kuatamia wenyewe.
Bei yake ni tsh 9000.Kwa anayehitaji anipm.
Kwa wanaohitaji kuku mcahotara kwa ajili ya mbegu,wanapatikana, wako 1600,wana umri wa miezi 5,wote wako rika moja.Kama utawachukua utakaa nao mwezi mmoja tu kisha wataanza kutaga.Utakuwa na uwezo wa kupata mayai mengi,bora na salama ambayo utayatumia kuzalisha vifaranga kwa njia ya mashine.Pia wana uwezo wa kuatamia wenyewe.
Bei yake ni tsh 9000.Kwa anayehitaji anipm.
Inategemea unataka incubator za kutoka wapi,hapa hapa nchini au nje ya nchi
Kimsingi kuku wote wanalipa katika ufugaji,mfano kuku wa nyama broilers,kila wiki ukaingiza let say vifaranga 300 ,ukawafuga kwa kufuata kanuni,ukawafuga kwa wiki 8 ili uwauze kwa tshs. 6000/=.Kama kila wiki utaingiza vifaranga ina maana bechi ya kwanza watakapofikia wiki 8,tayari utakuwa na bechi nyingine 7 zinafuata.Chukulia vifo ni 50 katika kuku 300 ingawa inaweza ikawa chini ya hapo.Kwa hiyo katika kila bechi kila wiki utakuwa na kuku 250.
Kimahesababu kuku 250 ukizidisha mara tshs.6000/=,utapata tshs. 1500,000/= kwa wiki na kwa mwezi utapata tshs 6000,000/=.Mapato ya broilers yanaanza baada ya miezi 2 yaani wk 8 ingawa unaweza ukawauza chini ya hapo lkn kwa uzito wa chini kidogo ndio maana inashauriwa wauzwe wk ya nane.
Kuku wa mayai pia nao wanalipa sana tatizo inatakiwa uwe na mtaji mkubwa kwa ajili ya gharama ya kuwanunua na chakula ,mathalani kwa sasa baadhi ya makampuni ya kutotoresha vifaranga wanauza kila kifaranga tshs.2500.Kila kifaranga mpaka atakapoanza kutaga atahitaji kilo 8 za chakula,ukiongeza na madawa,mfanyakazi nk utajikuta unatakiwa uwe na mtaji mkubwa kweli.Mapato ya kuku wa mayai utaanza kupata kwa wastani kuanzia mwezi wa 5 katikati .Baada ya hapo utakuwa na kazi kuuza mayai tu mpaka watakapo choka wiki ya 80 kama umewatunza kwa kufuata misingi na kanuni boro za ufugaji.
Kama ni kuku wa mayai,wakisasa ni wazuri zaidi kwa kuwa wanataga kwa wingi. Kama ni wa nyama ukiweza kufaga machotara ni wazuri zaidi kutokana na kuwa na soko la uhakika.Watu wengi sasa hivi wanapenda kuku wa kienyeji hivyo machota, nyama yake haina tofauti na kuku wa kienyeji,pia ukiweza kuwafuga kwa miezi 6 utaweza kuwauza kila kuku kwa tsh.10000/= bila mteja anayenunua kulalamika.Kuku pure wa kienyeji wana ukuaji hafifu.