Ufugaji wa Kuku wa Kisasa: Fahamu Mbinu, Faida, Changamoto na Masoko

Zinazotengenezwa tanzania na zinazotoka nje. Zakuanzia mayai 100 mpaka 500. Bei zikoje?
 
Napenda kufahanu bei ya incubator zinazotengenezwa tanzania na zinazotoka china bei yake kuanzia ya mayai 100 mpaka 500.
 
Mimi naona unisaidie ushauri nina kuku wangu chotara mwanzon walikuwa wanataga vizur lakini kwa sasa ni kama hawatagi maana wanaweza taga mayai 10 au pungufu na nina kuku kama 80 hv. Halafu ikifikia kulalia hawa kuku wanalalia kweli maana nina wawili walilalia wakaangua vzur ila kama kuku wa5 hv waliharibu mayai wiki ya 2, tatizo ni nini?

Natanguliza shukrani
 
Kuhusu utagaji kuna dawa maalam za kuwapa ili kuwabust na kuwafanya waongoze kutaga, zaidi tunaweza kuwasiliana kwa msaada zaidi.Kuhusu kuharibu mayai, ni kutokana na kutotibiwa.Ni muhimu mayai kutibiwa kabla kuku hajaanza kuyaatamia.
 
Ina maana hayo mayai yakitibiwa kama unavyosema kuku hawa wanao uwezo wa kuangua vifaranga kama ilivyo kwa kuku wa kienyeji kabisa? Na je hizo dawa za kuwa boost ili watage hazina madhara maana nakwepa kufuga kuku wa kisasa kwa sababu ya madawa.
 
Ninatafuta vitabu au majarida yanayoelezea vizuri namna bora ya ufugaji wa kuku wa kienyeji, Je nitafute kitabu gani kizuri?
Tuwasiliane mkuu,nanavyo.Ni pamphlects zinazotoa mwongozo wa ufugaji bora wa kuku wa kienyeji,chotara na wa kisasa.
 
Ina maana hayo mayai yakitibiwa kama unavyosema kuku hawa wanao uwezo wa kuangua vifaranga kama ilivyo kwa kuku wa kienyeji kabisa? Na je hizo dawa za kuwa boost ili watage hazina madhara maana nakwepa kufuga kuku wa kisasa kwa sababu ya madawa.

Moureen,

Kuku wa kisasa hana uwezo wa kuangua mayai mwenyewe kama ilivyo kwa kuku wa kienyeji,isipokuwa mayai ya kuku wa kisasa (kuku wazazi) hutotolewa vifaranga kwa kutumia Incubators.

Busta hazina madhara,ni kama zilivyo dawa zingine. Dawa maalum ambazo huwachochea kuku kudaga zaidi.Busta mara nyingi hutumika kutokana na mfugaji kuwa na formula isiyofa isiyokidhi mahitaji kuwafanya kuku waweze kutaga zaidi, lakini kama mfugaji atakapata formula nzuri ya uchanganyaji wa chakula kuku wake watataga tu vizuri.
 
Hi! kichwa mbovu nilitaka kujua kama biashara ya mayai ya kuku wa kienyeji inalipa kwa hapa Tanzania. Nina plan za kufanya hii biashara on commercial basis. Na je unaposema kuku chotara inamaanisha bado mayai yake yatakuwa ni kama ya kuku wa kienyeji? Kuna aina ya kuku inaitwa Longhorn inasemekana ni aina ya kuku wanaotaga mayai mengi zaidi duniani je hii ni aina ya kuku wa kienyeji kama sio ni aina gani ya kuku wa kienyeji wanaotaga mayai mengi zaidi nijuze tu hata kama wanapatikana nje ya Tanzania ilimradi tu wawe wa kienyeji maana ndio biashara ninayotaka kufanya kwa sasa.
 
Salari,

Kiasili kuku wa kienyeji si watagaji sana,kama ilivyo kwa kuku wa kisasa wa mayai.Ndio maana ili kuboresha kosaafu ya kuku wa kienyeji tuna wacross na kuku wa kisasa wenye wenye uwezo mkubwa wa kutaga mayai.Na kwa kufanya hivyo,tunakuwa tumewaongezea uwezo wa utagaji wa hawa kuku wa kienyeji. Mayai yanayotagwa na kuku chotara hayana tofauti na kuku wa kienyeji.

Na kwa upande wa longhorn, hao ni kuku wa kisasa,kama walivyo kuku wengine wa kisasa.Mara nyingi kuku wa kienyeji wanapatikana zaidi kwenye nchi zetu za afrika,kwa nchi za wanzetu nje ya Afrika hii kosaafu ya kuku wa kienyeji imetoweka na waliobaki nao ni kuku wa kisasa ambao wamepitia kwenye mlolongo mwigi wa mabadiliko yao.Kuku wa kienyeji aina ya kuchi ukimcross na kuku wa kisasa aina rhode island red au Barred polymouth rock wale wachotara watakaozaliwa huwa wana uwezo mkubwa wa kutaga mayai.

Soko la mayai hapa nchini ni kubwa sana kuazia kwenye supermakerts hadi mitaani kwa wachoma chips.
 
Mkuu Kichwa, si kweli kwamba Kuku wa kienyeji wako Africa pekee, Bado hata baadhi ya Nchi za Ulaya wako wengi tu, Asia ndo usiseme, na Kuna Mbegu fulani ya kuku wa Kienyeji kutoka Israeli naifuatalia Kenya make niliambiwa wanapatikana huko so niko kwenye process za kuwanunua baadhi nione wako vipi
 

Chasha,

Nashukrani kwa kunifahamisha hilo,nilikuwa sijui maana siku zote huwa naagiza kuku wazazi kutoka nje ila sijapata kusikia uwepo wa kuku wa kienyeji huko. Nimepata somo jipya leo nitafuatilia zaidi ili nipate kuwajua zaidi tena ikibidi majina yao kama ilivyo kwetu mfano kuchi nk.
 
Nimekupata mtaalam. Nipi hizo contact zako tuwasiliane.

 

Ok nitawahitaji hao mwezi uao, wasiwasi yangu ni moja tu. Nayo ni kuwa hawataathirika na mabadiliko ya ghafla ya mizingira? Kuna uwezekano mkubwa wa kuwepo na tofauti kubwa ya mazingira yako na yangu na pia hata chakula kwani unajua kuna mavyakula mengi tu sokoni yeynye ubora tofauti tofauti. hebu saidia katika hili mkuu wetu.
 

Asante sana kwa yote kichwa mbovu. Mimi pia nitawahitaji labda mwezi ujao kwani sasa hivi kwenye Mpango Kazi wa ukarabati wa mabanda. Wasiwasi au hofu yangu ni moja tu. Hawa hawataathirika na mabadiliko ya ghafla ya mazingira. Kwani mazingira ya huko kwako yanaweza kuwa tafauti na ya kwangu.

Hata chakula pia, kuna uwezekano wa kuwa na tofauti za vyakula kwani siku hizi mavyakula ya kuku yako ya aina nyingi sana na yaliyo chakachuliwa ni mengi sana. Tusaidie katika hili. By the way nilielezwa kuwa asali pia ni good appetizer kwa kuku, hili lina ukweli gani kitaalam mkuu?
 
Inategemea unataka incubator za kutoka wapi,hapa hapa nchini au nje ya nchi

Kwa ajili ya incubator za nje, jaribuni pia kupitia website ya Egg incubators | Poultry incubator | Egg incubation | Chicken incubation | Incubation eggs pia deliveriestheincubatorshop.co.uk.Wana incubators nyingi na vitu vingine vingi kwa ajili ya ufugaji wa kuku na hata hao parent stock wanoa. Ebu wapitieni ila tatizo lao ni kuwa sheria za EU haziwaruhusu kuuza moja kwa moja nje ya EU lakini
ukiwa na mtu au ndugu yako huko Ulaya, anaweza kukununulia na kukutumia. Hii haizuiliwi. Asanteni kwa leo.
 

Nimehamasika kwa kiasi kikubwa na ufugaji wa kuku wa kizungu na kienyeji, shida yangu kubwa ni kupata soko la uhakika, je unaweza kunisaisia kupata masoko ya aina tajwa ya kuku hao ili kupunguza usumbufu wa kupata masoko ya uhakika? Usisite kuwasiliana nami. Regards
 
Jamani msione kimya kwa muda mrefu,nilikuwa kwenye mitihani kwa muda wa wiki tatu mfululizo,na baada ya kumaliza mitihani nikawa nimeondoka kuelekea Songea na mpaka hivi sasa nipo huku Songea.Nimefika huku Songea moderm yangu ya tigo inasumbua kidogo,nashindwa kujibu kwa wakati na kuendelea na darasa letu.Ila kwa wale wanaohitaji miongozo mbalimbali ya ufugaji bora wa kuku wa kisasa na kienyeji naomba tuwasiliane kwa namba 0767989713 au 0715989713.

Hata kama una mambo yanakutatatiza kwenye ufugaji wako pia usisite kuwasiliana nami,tutasaidiana.

Pia kwa wale ambao wanafuga kuku wa mayai,wamejitahidi kuwahudumia kwa kila namna lakini kuku wakawa hawatagi katika kiwango cha kukuwezesha kupata faida,nina ufumbuzi wa tatizo hilo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…