Ufugaji wa Kuku wa Kisasa: Fahamu Mbinu, Faida, Changamoto na Masoko

Ufugaji wa Kuku wa Kisasa: Fahamu Mbinu, Faida, Changamoto na Masoko

Mkuu Kichwa Bahati mbaya siko Dar Ningekutafuta hata Mimi,

Ila Mkuu nina swali kwenye Chakula Cha Kuku, Mkuu nilipata kusoma Mahali fulani na Baadae nikaja Kuprove ni kweli kabisa.

Tatizo kwenye utengenezaji wa Chakula Cha Kuku Uko kwenye kupima DCP Digestive Crude Protein, na CP kawaida haiwezi pimwa kwa macho wala kwa mizani bali kuna kifaa maalumu na Makampuni ya Kutengeneza vyakula vya Kuku watakuwa nacho na hapo no sehemu ngumu kwa wajasirimali wadogo,

Kwa kenya wao wana Maabara ya Serikali na ukisha Tengeneza chakula unapeleka Maabara kupima Kiwango cha CP,

Tatizo ni kwamba unaweza kuta zao Moja lina CP tofauti kwa kiwango, Mfano. Mahindi yanaweza kutofautina kiwango cha Protein kwa sababu nyingi sana ikiwemo sehemu yalipo limwa, ukame na kazalika, Unaweza kuta Soya inayolimwa Mbeaya ikawa na CP nyingi kuliko my be SOYA inayo limwa DODOMA, naAlzeti hivyo hivyo na kwa macho huwezi tambua kamwe so unaweza pima Kilo 10 za soya kumbe kwa hiyo soya yako ilitakiwa upime Kilo 12 na si Kumi.


Na kwa maelezo niliyo pata tatizo kubwa sana ni jinsi ya Kupima CP na hii ni kwa sababu zao moja linaweza kuwa na CP tofauti na utata uko hapo

Je wewe unafanya nini hapa kwenye kupima DCP?

SO MKUU UTAKUBALIANA NA MIMI KWAMBA HAPO KUNA KAZI KUBWA SANA NA BILA KUPROVE MAABARA HUWEZI TAMBUA DCP ILIYOPO KWENYE HICHO CHAKULA ULICHO TENGENEZA
Chasha,

Unachosema nisahii kabisa,isipokuwa unapotengeneza formula ya chukula cha kuku unatakiwa uwe na jedwali la mahitaji ya virutubisho vya kuku (Poultry nutrient specification) ambayo hutoa mwongozo wakati wa utengenezaji wa formula.

Pia unatakiwa uwe na jedwali lingine linaloonesha kiwango cha virutubisho vinavyopatikana kutoka katika kila zao.Malighafi zote zinazotumika kwenye utengenezaji wa chakula kutoka katika kila eneo hupimwa maabara kwa mkemia mkuu wa serikali,au mamlaka ya vyakula na dawa au kwenye maabara ya wizara ya maendeleo ya mifugo na uvuvi.

Washapata hizo specisfication,ndipo zinapotumiwa na watengenezaji wa formula kwenye kuandaa formula.

Ingawa crude protein na virutubisho vingine hutofautiana kulingana na mahari mazao yanapolimwa,tofauti yake haiwi kubwa sana mpaka ikaathiri kabisa ubora wa chakula,ndio maana wafugaji wengi wakipata formula tu wanatumia malighafi kutoka sehemu yoyote ile na kutengeneza chakula,na kuku wanaperform vizuri tu.

Ila kwa wanaotengeza formula na uuzaji wa vya kula vyakuku kwa eneo fulani mfano Namtumbo,na malighafi unazipata palepale,ni muhimu mmiliki wa kiwanda cha utengenezaji wa chakula akakusanya malighafi zote na kupeleka kuzipima mchango wa virutubisho kutoka katika kila zao.

Kwa mtumiaji wa formula hata isikupe shida sana,kwa kuwa kiwango kikubwa cha mahindi na malighafi zinatoka mikoa ya nyanda za juu kusini.So ni muhimu tu kama utafuata formula mambo yatakaa sawa
 
Mkuu Kicwa ni kweli ila nazani unakubaliana na mimi kwamba kupima CP ni muhimu sana, na Kenya wanayo yakwao na wanachaji kma Tsh 18000 ukipeleka Chakula chako kupimwa na ni within a day unapata matokeo,

Mkuu Incubatorsnyingi za Kisasa zina kitu kinaitwa eggs turining systema, na sehemu ya kuwekea mayai imekaa kama tray z mayai za kawaida na unap weka mayai kwenye Incubators sehemu iliyo Chongoka ndo huangalia Chini, ni hivyo, SASA SWALI,

Ni kwanini kwenye Kugeuza mayai sehemu zilizo Chongoka hazihusiki na badala yake ni upande kwa upande tu? Make incubators ukiona inavyo geuza hayo mayai ni dhahiri inageuza zile tumbo za yai pekee,
 
Mkuu kichwa mbovu mimi tayari nimeanza kufuga kuku wa mayai na ni kwa uhamasishaji wako! ubarikiwe!
Hapo kwenye masaa ya kuku kula naomba msaada kwani umesema broirer wanakula kwa saa 18 je layers ni masaa mangapi!
Mimi kwa sasa kwa kukuwa wana week kumi na moja kila mmoja nimempigia wastani wa gram 60 tu za chakula kikiisha siongezi tena, je ninakosea?Asante
Kajansi,

Layers wao wanatakiwa wawekewe toka asubuhi kuanzia saa 2 asubuhi,weendelee kula mpaka watakapomaliza share yao kwa siku.Gram 60 kwa siku kwa kuku mmoja mwenye umri wa wiki 10 ni sawa kabisa.Ila wiki ya kumi na moja kiwango kitaongezeka,pitia program ya chakula kwenye posti za nyuma.
 
Mkuu Kicwa ni kweli ila nazani unakubaliana na mimi kwamba kupima CP ni muhimu sana, na Kenya wanayo yakwao na wanachaji kma Tsh 18000 ukipeleka Chakula chako kupimwa na ni within a day unapata matokeo,

Mkuu Incubatorsnyingi za Kisasa zina kitu kinaitwa eggs turining systema, na sehemu ya kuwekea mayai imekaa kama tray z mayai za kawaida na unap weka mayai kwenye Incubators sehemu iliyo Chongoka ndo huangalia Chini, ni hivyo, SASA SWALI,

Ni kwanini kwenye Kugeuza mayai sehemu zilizo Chongoka hazihusiki na badala yake ni upande kwa upande tu? Make incubators ukiona inavyo geuza hayo mayai ni dhahiri inageuza zile tumbo za yai pekee,

Chasha,

Lengo la kugeuza mayai ni kufanya kifaranga kilichojitengeneza tayari kwenye yai kisinate kwenye kuta za yai.Kifaranga kilichonata kwenye kuta za yai hufa na hivyo kushindwa kutotolewa.Ndio maana ukichukua yai lisilototolewa na kulivunja utakuta kuna kifaranga kilichokufa.

Pia sehemu nene ya juu ya yai ndiko kuliko na kichwa cha kifaranga ambako hakutakiwi kutazame chini kwa kuwa sehimu hiyo ndiyo yenye matundu ya hewa ambayo huruhusu hewa safi kuingia na kutumiwa na kifaranga na pia sehemu hiyo kuruhusu hewa chafu kutoka.

Kifaranga kisipopata hewa safi kupitia sehemu nene ya yai hufa kabla ya siku 21.
 
Mkuu kichwa vizuri sana, vipi katika kuongeza maji kwenye Incubators ni ipi better? kuweka ya moto/uvuguvugu au ya baridi,
 
sawa, karibu sana nadhani utafaidika kwa elimu adhimu ya ufugaji na ujasiriamali.

Naandika sasa hivi saa 3:05 nikitaka kujua na ku-confirm juu ya kuwepo au kutokuwepo kwa kikao chetu cha mafunzo. Kichwa mbovu confirm tafadhali ili tupange mambo. Nasubiri feedback hapa JF vinginevyo nitakupigia kujua mambo yalivyo.

Asante kichwa mbovu!
 
naandika sasa hivi saa 3:05 nikitaka kujua na ku-confirm juu ya kuwepo au kutokuwepo kwa kikao chetu cha mafunzo. Kichwa mbovu confirm tafadhali ili tupange mambo. Nasubiri feedback hapa jf vinginevyo nitakupigia kujua mambo yalivyo. Asante kichwa mbovu!

Mzee Mukaruka,

Nakukushukuru kwa kuonyesha utayari wako kwenye mafunzo.Mpaka sasa hivi walionyesha kuwa tayari kwenye mafunzo ni watatu, yaani wewe, kunte kinte pamoja na mama Joe. Chasha Yuko safarini ingawa alikuwa tayari.

Kwa hiyo nilitariji kufanya mafunzo kama washirikia wangeanzia 5 na kuendelea,kwa idadi iliyopo sasa aina ya mafunzo yanayofaa ni yale ya farm visit. Ni mafunzo ambayo hufanyika pale mfugaji anapotembelewa kwake.

Kwa hiyo Mzee Mukarukaka unaweza ukashauri tufanyaje juu ya hili. Kama itashindikana safari hii,tunaweza tukawasiliana wakati ujao,kwani kwa mafunzo niliyokusudia kuyatoa, isinge nilipa kwa maana kwamba nilihitaji kutoa mafunzo yaliyobazi zaidi kwenye vitendo, kitu ambacho kingewasaidia sana wafugaji.
 
Mkuu kichwa vizuri sana, vipi katika kuongeza maji kwenye Incubators ni ipi better? kuweka ya moto/uvuguvugu au ya baridi,

Chasha,
Kuongeza maji ya baridi ndiyo inaswihi zaida,na mashine nyingi zinataka hivyo,ingawa kuna baadha wanaweka maji ya moto kusudi kuongeza haraka kiasi cha mvuke/unyevunyevu kwenye machine.
 
Kajansi,
Layers wao wanatakiwa wawekewe toka asubuhi kuanzia saa 2 asubuhi,weendelee kula mpaka watakapomaliza share yao kwa siku.Gram 60 kwa siku kwa kuku mmoja mwenye umri wa wiki 10 ni sawa kabisa.Ila wiki ya kumi na moja kiwango kitaongezeka,pitia program ya chakula kwenye posti za nyuma.

Asante sana kichwa! kwa ufafanuzi! kiukweli ningependa kushiriki ila umbali ndo tatizo kwani nipo mwanza!

Nitajitahidi kukusanya wadau kama kumi na tupange na wewe jinsi ya kutufikia!
 
Asante sana kichwa! kwa ufafanuzi! kiukweli ningependa kushiriki ila umbali ndo tatizo kwani nipo mwanza!

Nitajitahidi kukusanya wadau kama kumi na tupange na wewe jinsi ya kutufikia!

Ok sawa mkuu,nadhani hiyo itakuwa nzuri.Niko tayari kualikwa sehemu yoyote kwa ajili ya kutoa mafunzo.
 
Mkuu kichwa mbovu, kama hapa Tanzania siwezi kupata kuku wazazi kwa ajili ya broilers. Je, naweza kupata mayai kwa ajili ya kuyatotolesha hayo hayo ya broilers kwa hapa Tanzania?
 
Mkuu kichwa mbovu, kama hapa Tanzania siwezi kupata kuku wazazi kwa ajili ya broilers Je naweza kupata mayai kwa ajili ya kuyatotolesha hayo hayo ya broilers kwa hapa Tanzania??

King kingo,

Kwa hapa Tanzania huwezi pata kwani makampuni mengi yanayozalisha mayai nchini ,yanayotosha mahitaji yao tu,lakini pia hii ni biashara kukuuzia wewe mayai ya kuku wazazi ni kama kuharibu biashara yao,mara nyingi huwa hawako tayari kufanya hivyo labda kuwe na ziada kubwa ambayo bila kuyauza yanaharibika,au Incubators zao ziharibike,hapo wanakuwa hawana namna zaidi ya kuyauza.

Kwa mujibu wa sheria ya nchi inayosimamiwa na wizara ya maendeleo ya mifugo na uvuvi,wamezuia uingizaji wa mayai ya kuku wazazi kwa ajili ya kuzuia magonjwa kuingia nchini kutoka kwa mayai ya kuku wazazi. Mfano, wazazi wa kuku wazazi (Grand parent stock) kama watakuwa na uambukizo wa magonjwa ni rahisi kurithisha magonjwa kwa kuku wazazi kupitia mayai.

Kwa sababu hiyo, serikali iliamua ipige stop kabisa uingizaji wa mayai ya kuku wazazi nchini badala yake wameruhusu uingizaji wa kuku wazazi waliochanjwa chanjo zilizoamriwa na serikali kutoka kwenye nchi husika ambayo unaagizia vifaranga wa kuku wazazi.
 
Wanajamii forum hasa jukwaa hili la ujasiriamali,

Nina habari njema kwa watu wa Dar-es-salaam,kuanzia ijumaa ya wiki ijayo tarehe 12,13 na 14 siku ya jumapili nitakuwa huko.Kwa wale watakaonihitaji ili kuwakagulia na kuwashauri juu ya miradi yao ya ufugaji wa kuku tuwasiliane kwa email yangu amanngoma@gmail.com au kwa namba 0767989713 au 0715989713.

Kama mnaweza kujikusanya sehemu watu kadhaa naweza nikawaendeshea mafunzo ya ufugaji wa kuku kwa faida na kama kutakuwa na matatizo mengine yanawasumbua mtapata fursa ya kuyauliza na nitawajibu kwa ufasaha,mfano unafuga kuku wa mayai,wamefikia umri wa kutaga lakini wanataga wachache au hawatagi kabisa,ninao ufumbuzi wa tatizo hilo.

Watakaohudhuria wataweza kujipatia bonus ya feed formula za kuku wa nyama aina ya broilers(aina zote za feed formula) na pia zile za Layers mash.Formula zangu za kutengeneza chakula ni zile za Industrial ambazo ni nzuri na huwezi kuzipata sehemu yoyote.Kwa makampuni au watu binafsi ambao hujishughulisha na utotoreshaji wa vifaranga,pia tuwasiliane nina feed formula za kuku wazazi aina zote.

Kwa kawaida feed formula moja mfano formula za broiler laki moja,lakini tukionana huko itakuwa itakuwa ni bonus.Ukitengeneza mwenyewe chakula inakulipa sana kuliko kununua.

Kwa wanaohitaji gharama kwa washiriki ambao watajikusanya pamoja ni tsh 30,000/=tu.Na pia watakaohitaji mwongozo wa ufugaji bora na wa kisasa wa kuku,kutakuwa na punguzo maalum.

Kwa sababu mifugo ni taaluma yetu,pia kutakuwa na fursa ya kuuliza maswali ya miradi ya ufugaji wa wanyama aina nyingine mfano Ng'ombe,mbuzi,kondoo,nk.

Kuonyesha uko tayari like post kisha nipm au ni email au nipigie.
MADA ZA MAFUNZO
1. Mafunzo kwa vitendo.
  • Tiba ya mayai kabla hayajatotoreshwa.
  • Tiba za magonjwa ya kuku kwa njia ya sindano mfano Ndui,taifodi na kipindupindu cha kuku,namna ya kuchoma,sehemu ya kuchoma,dawa za kutumia na dozi yake
  • Ukataji wa midomo ya kuku(Debeaking) ili kuzuia kudonoana wenyewe kwa wenyewe na mayai.
  • Uchanganyaji wa dawa maalum zitakazo wafanya kuku wasiotaga au wanaotaga kidogo watage zaidi ili kuongeza tija kwa mfugaji.
2. Utambuaji,ukusanyaji,uandaaji na uhifadhi wa malighafi.

3. Namna ya kutambua magonjwa na Tiba zake.
 
MADA ZA MAFUNZO
1. Mafunzo kwa vitendo.
  • Tiba ya mayai kabla hayajatotoreshwa.
  • Tiba za magonjwa ya kuku kwa njia ya sindano mfano Ndui,taifodi na kipindupindu cha kuku,namna ya kuchoma,sehemu ya kuchoma,dawa za kutumia na dozi yake
  • Ukataji wa midomo ya kuku(Debeaking) ili kuzuia kudonoana wenyewe kwa wenyewe na mayai.
  • Uchanganyaji wa dawa maalum zitakazo wafanya kuku wasiotaga au wanaotaga kidogo watage zaidi ili kuongeza tija kwa mfugaji.
2. Utambuaji,ukusanyaji,uandaaji na uhifadhi wa malighafi.

3. Namna ya kutambua magonjwa na Tiba zake.

Mkuu Mada zimekaa sawa!!
 
Back
Top Bottom