Aman Ng'oma
JF-Expert Member
- Nov 8, 2011
- 961
- 533
Chasha,Mkuu Kichwa Bahati mbaya siko Dar Ningekutafuta hata Mimi,
Ila Mkuu nina swali kwenye Chakula Cha Kuku, Mkuu nilipata kusoma Mahali fulani na Baadae nikaja Kuprove ni kweli kabisa.
Tatizo kwenye utengenezaji wa Chakula Cha Kuku Uko kwenye kupima DCP Digestive Crude Protein, na CP kawaida haiwezi pimwa kwa macho wala kwa mizani bali kuna kifaa maalumu na Makampuni ya Kutengeneza vyakula vya Kuku watakuwa nacho na hapo no sehemu ngumu kwa wajasirimali wadogo,
Kwa kenya wao wana Maabara ya Serikali na ukisha Tengeneza chakula unapeleka Maabara kupima Kiwango cha CP,
Tatizo ni kwamba unaweza kuta zao Moja lina CP tofauti kwa kiwango, Mfano. Mahindi yanaweza kutofautina kiwango cha Protein kwa sababu nyingi sana ikiwemo sehemu yalipo limwa, ukame na kazalika, Unaweza kuta Soya inayolimwa Mbeaya ikawa na CP nyingi kuliko my be SOYA inayo limwa DODOMA, naAlzeti hivyo hivyo na kwa macho huwezi tambua kamwe so unaweza pima Kilo 10 za soya kumbe kwa hiyo soya yako ilitakiwa upime Kilo 12 na si Kumi.
Na kwa maelezo niliyo pata tatizo kubwa sana ni jinsi ya Kupima CP na hii ni kwa sababu zao moja linaweza kuwa na CP tofauti na utata uko hapo
Je wewe unafanya nini hapa kwenye kupima DCP?
SO MKUU UTAKUBALIANA NA MIMI KWAMBA HAPO KUNA KAZI KUBWA SANA NA BILA KUPROVE MAABARA HUWEZI TAMBUA DCP ILIYOPO KWENYE HICHO CHAKULA ULICHO TENGENEZA
Unachosema nisahii kabisa,isipokuwa unapotengeneza formula ya chukula cha kuku unatakiwa uwe na jedwali la mahitaji ya virutubisho vya kuku (Poultry nutrient specification) ambayo hutoa mwongozo wakati wa utengenezaji wa formula.
Pia unatakiwa uwe na jedwali lingine linaloonesha kiwango cha virutubisho vinavyopatikana kutoka katika kila zao.Malighafi zote zinazotumika kwenye utengenezaji wa chakula kutoka katika kila eneo hupimwa maabara kwa mkemia mkuu wa serikali,au mamlaka ya vyakula na dawa au kwenye maabara ya wizara ya maendeleo ya mifugo na uvuvi.
Washapata hizo specisfication,ndipo zinapotumiwa na watengenezaji wa formula kwenye kuandaa formula.
Ingawa crude protein na virutubisho vingine hutofautiana kulingana na mahari mazao yanapolimwa,tofauti yake haiwi kubwa sana mpaka ikaathiri kabisa ubora wa chakula,ndio maana wafugaji wengi wakipata formula tu wanatumia malighafi kutoka sehemu yoyote ile na kutengeneza chakula,na kuku wanaperform vizuri tu.
Ila kwa wanaotengeza formula na uuzaji wa vya kula vyakuku kwa eneo fulani mfano Namtumbo,na malighafi unazipata palepale,ni muhimu mmiliki wa kiwanda cha utengenezaji wa chakula akakusanya malighafi zote na kupeleka kuzipima mchango wa virutubisho kutoka katika kila zao.
Kwa mtumiaji wa formula hata isikupe shida sana,kwa kuwa kiwango kikubwa cha mahindi na malighafi zinatoka mikoa ya nyanda za juu kusini.So ni muhimu tu kama utafuata formula mambo yatakaa sawa