Mzee Mukaruka
JF-Expert Member
- Jun 18, 2012
- 712
- 393
Kweli lichwa mbovu unatisha! Kwa mwonekano huo, namini na mambo yaliyomo ndani ni ya uhakika na kwa hiyo bei ni halali. Hata nikipata sofy copy, lazima nitafute hiyo hard copy. Asante kichwa mbovu kwa yote na tuko pamoja.View attachment 97196
Huu ndiyo mwonekano wa mbele wa kitabu changu cha mwongozo wa ufugaji bora wa kuku.Bado naendelea kukiuza kwa wafugaji mbalimbali kote nchini.
Mh.king kingo,unatakiwa angalau uwe na kuku wazazi 200.
King kingo,Mkuu kichwa,
Asante kwa ufafanuzi wako hivi ni shilingi ngapi hao kuku wazazi na inachukua muda gani mimi kuwapata toka nimetoa order? Na wanakuja wakiwa na umri gani?
Kweli lichwa mbovu unatisha! Kwa mwonekano huo, namini na mambo yaliyomo ndani ni ya uhakika na kwa hiyo bei ni halali. Hata nikipata sofy copy, lazima nitafute hiyo hard copy. Asante kichwa mbovu kwa yote na tuko pamoja.
King kingo,
Toka umeweka order,inachukua wiki 4 tu mpaka kuwapata.Kuku hawa wanakuja wakiwa na umri wa siku moja.Gharama kwa kifaranga mmoja ni tsh 16,000/=ikiwa ni pamoja na usafiri mpaka Dar es salaam (Mwl Nyerere International airport).Bei hizi ni kwa mujibu wa poforma invoice niliyotumia kuagizia vifaranga hao wazazi 6 july 2010.
Ok sawa na je huwa wanachukua muda gani kuanza kutaga? na chakula chao ni kama cha layers wa kawaida na kwa mfano nikiagiza 200 nitapataje uhakika kuwa wote watakuwa wanataga? kwasababu nilishawahi kufuga kuku wa mayai lakini sio wote walikuwa wanataga
King kingo,
Kuku hawa wanaanza kutaga wakiwa na umri wa wiki kumi na tisa.Kuku wazazi wa mayai wanataga sana kama utafuata masharti yao ya malezi pamoja na chakula.Kwa kawaida sio rahisi kuku wote katika kundi wakawa wanataga,isipokuwa kwa kuku wazazi wa mayai wanapokuwa kwenye kilele cha utagaji wanataga hadi asilimia 96.
Kuku wako wa mayai hawakuwa wanataga wote inategemea na aina ya management uliyokuwa unawapa.Lakini vinginevyo kuku hawa ni watagaji wazuri tu,laita ungewasiliana na mimi ningekuuzia uchawi wa dactari na kuku wako wangetaga vizuri.
Najua changamoto kubwa inayowakabili wafugaji wa kuku ni kwenye utagaji hasa kutokana na chakula wanachowalisha kutokuwa na ubora unaotakiwa,pia kuku hawa kukabiliwa na magonjwa na mfugaji kushindwa kuyatambua n.k Kuhusu suala la utagaji nishalifanyia utafiti na nimepata mafanikio makubwa sana.Kama una kuku ambao hawatagi au wameonekana wanaelekea kuchoka katika utagaji kabla ya muda wake tuwasiliane hata usiwauze,watataga vizuri sana mpaka utashangaa.
Kiukweli katika ufugaji wa kuku hakuna kubahatisha kwenye ushughulikiwaji matatizo vinginevyo hasara haiepukiki.Kwa suala la kuku kushindwa kutaga katika malengo yaliyokusudiwa siyo tatizo tena ukifanya mawasiliano nami.
Kuku wazazi wanachakula chao maalum ambacho kinatengenezwa kwa kutumia malighafi hizi hizi zinazotumika kutengenezea chakula cha kuku wa kawaida yaani Layers na Broilers.Kuku wazazi wa kuku wa mayai ni watagaji sana na ndio maana hiyo tabia wamewarisisha watoto wao yaani kuku wa mayai wa kawaida.
Kuku wazazi wa mayai au nyama ninaowaagiza ndio hao hao hata hayo makampuni makubwa ya utotoleshaji wa vifaranga ndiyo waliyokuwa nao,na wengi wao wao wanaagizia huko huko ambako mimi naagizia.
Sabayi,Mkuu wewe unauza vifaranga wa kuku wayai? siku hizi kupata kuku wazuri ni issue
Vifaranga wazazi wa kuku wa nyama n mayai wanazalishwa kwa sasa nchini Kenya, kuna kampuni moja inawazalisha na kuuza nchi mbalimbali
Mradi wa shamba la utotoleshaji wa vifaranga,mahitaji yanayohitajika roughly
Kuku wazazi wa mayai 1300 ,gharama ni tshs.20,800,000/=,kwa idadi hii ya kuku wazazi utahitaji incubators 4 zenye uwezo wa kubeba mayai 5280 kila moja,na kwa wiki mashine moja itaingiza mayai 1760 x 4=kwa wiki utatotolesha mayai 7040.Kuku wazazi 1130 watatoa si chini ya mayai 7210.Gharama za incubators 4 tshs.8000000/=
Gharama ya chakula mpaka kuanza kutaga ni tsh 9040000/=Gharama ya madawa na dactari ni tsh.7232000/=Utaongeza gharama za nyumba moja kwa ajili ya kutotoleshea,nyumba moja tena kwa ajili ya bruda,na nyumba nyingine kwa ajili ya kuwalelea kuku wazazi.
Utahitaji pia mixing machine kwa ajili ya kutengenezea chakula,ila haina haraka sana,kwani unaweza kuanza kwa kutengeneza manually.
Majengo unaweza ukayajenga simple kwa kuanzia na kisha ukawaajili walinzi.Pia utahitaji wafanyakazi Utahitaji wafanyakazi 5,hatchery 1,kwenye kuku wazazi 1,kwenye vifaranga 1,na kwenye utengenezaji wa chakula 2.Utahitaji pia at least ekari moja kwa ajili ujenzi wa miundo mbinu.
Mradi wa utotoleshaji wa vifaranga unalipa sana,sema tu unahitaji mtaji mkubwa wa kuanzisha biashara.
Mkuu vp soko la vifaranga usije ukazalisha vifaranga then ukaishia kuvifuga mwenyewe

Mkuu hizo gharama zako sio kabisa, kwaza kwenye Incubator unasema incubator 4 ni Tsh 8,000,000
-Na ado razima uwe na Genereta kubwa kabisa
-Bado mafuta
-Bado gharama za umeme
-Na kujitengenezea mwenyeyewe chakula cha kuku wengi bila mixer n hatari sana,
- Na kwa biashara kama hii ni lzima uwe na zile automatic systema za chakula na maji na hata mayai yanapo tagwa
KWA KIFUPI GHARAMA ZIKO JUU SANA NGOJA KUNA MCHANGANUO FULAI NILIKUWANAO NIKIUPAT NITAKULETA UONE ILIVYO GHARI SANA