Ufugaji wa Kuku wa Kisasa: Fahamu Mbinu, Faida, Changamoto na Masoko

Ufugaji wa Kuku wa Kisasa: Fahamu Mbinu, Faida, Changamoto na Masoko

Mbona kuku wangu wa kisasa wananyonyoka manyoya mgongoni
 
Mbona kuku wangu wa kisasa wananyonyoka manyoya mgongoni
Ni kawaida kwa kuku wa kisasa hasa wa mayai kunyonyoka manyoya na mara nyingi hali hii hutokea baada ya kuku kutimiza umri wa mwaka mmoja.

Unyonyokaji wa manyoya kitaalamu huitwa moulting.Moulting inapotokea kuku hupunguza utagaji na huendelea tena na utagaji mara manyoya yatakapoota tena.
 
Ni kawaida kwa kuku wa kisasa hasa wa mayai kunyonyoka manyoya na mara nyingi hali hii hutokea baada ya kuku kutimiza umri wa mwaka mmoja.

Unyonyokaji wa manyoya kitaalamu huitwa moulting.Moulting inapotokea kuku hupunguza utagaji na huendelea tena na utagaji mara manyoya yatakapoota tena.

Kaka naomba nipm nataka ile hardcopy.
 
Ukataji Wa Midomo

Ukataji wa kuku midomo ni hatua muhimu sana ambayo mfugaji lazima aipitie.Kazi ya ukataji wa midomo inapendekezwa ifanyike kabla kuku hawajaanza kutaga.

Kwa kawaida kuku huanza kutaga wanapofikia umri kati ya wiki 19 na 20 toka kuzaliwa. Kuku watatakiwa wakatwe midomo watakapokuwa na umri wa wiki 15. Kama wataanza kudonoana mapema zaidi kabla ya umri huo kufika, basi wakatwe midomo yao mapema zaidi kadri iwezekanavyo.

Sababu zinazochangia kuku kudonoana ni pamoja na mlundikano mkubwa wa kuku kwenye chumba kimoja, upungufu wa madini na vitamini kwenye chakula, vyombo vya chakula na maji kuwa vichache, mwanga mkali kupita kiasi kwenye mabanda ya kuku na wadudu mfano, utitiri, chawa na viroboto. Tatizo hili pia linachochewa na unyonyokaji wa manyoya (moulting) unaoambatana na utokaji damu ambayo huwavutia kuku na hivyo kuwafanya waanze kudonoana wao kwa wao.

Ili kudhibiti tatizo hili kutokea, mfugaji anashauriwa kuku wake, wakati wa mchana, waning'iniziwe majani au mboga kama vile chainizi, wapewe pia dawa zenye vitamini kwa wingi mfano, Egymycine, multivitamin, amin'total na vitalyte. Pia wawekewe bembea ambayo kuku watatumia kuchezea. Hiyo yote ni kuwafanya kuku wawe bize na hivyo kuwasahaulisha na kudonoana wao kwa wao.

Tatizo la kuku kudonoana iwapo mfugaji hatowahi kulidhibiti mapema atasababisha kuku wengi wafe na kuwafanya pia kuku wanaotaga washindwe kutaga kutokana na mshituko wa vidonda vya kudonolewa.

Ukizingatia kwa umakini yote yaliyoelezwa, hutapata shida kwenye ufugaji, kuku wako watakuwa wazuri na wachangamfu pia vifo havitakuwepo na hivyo utaweza kunufaika na kazi ya ufugaji.
 
Wanajamvi,

Kufuatia maoni yenu juu ya jina langu la kichwa mbovu nililokuwa nalitumia humu jamvini kutaka nilibadilishe,hatimaye nimelibadillisha na sasa nitajulikana kama Zantsan.Nawahukuru wote kwa mapendekezo yenu kwani wengine walisikia vibaya sana kuniita kichwa mbovu.

Tuendelee kushirikiana.
 
Naweza kupata mawasiliano yako mm napenda kufuga kuku wa kienyeji
 
Namshukuru Mungu majukumu yaliyokuwa yakinikabili sasa hivi nimeyakamilisha,niko free na kwa yeyote atakayenihitaji,mtu mmoja mmoja au kikundi mnaweza kunitafuta kwa ushauri, na semina ya mafunzo ya ufugaji bora wa kuku.
 
mkuu kwa nn hamjawa wazi sana kutueleza location na contacs zenu au seminars mnazofanya?
 
mkuu kwa nn hamjawa wazi sana kutueleza location na contacs zenu au seminars mnazofanya?
Sisi kwa sasa tuko morogoro,but tuko movable,kokote tutakakohitajika kwa ajili ya kuendesha mafunzo. Sisi ada zetu ni tsh 250000/=kwa siku kwa kila watu 25 waliojukusanya pamoja na kuhitaji mafunzo ya kujua mbinu na namna ya ufugaji bora wenye tija kwa mfugaji.
 
Mdau, vifaranga wa kuku wa nyama kwa sasa ni bei gani? Tunaweza kujua pia gharama za vyakula kwa batch ya kuku 300/kwa wiki?
 
Kaka mi naomba pia mawasiliano yako, nahitaji kuanza huu mradi ndani ya mwezi huu wa nane.
Asante sana.
 
mdau, vifaranga wa kuku wa nyama kwa sasa ni bei gani?, tunaweza kujua pia gharama za vyakula kwa batch ya kuku 300/kwa wiki?
Vifaranga wa kuku wa nyama kwa sasa ni tsh 1500,kuhusu gharama za chakula kwa kuku 3000,nipigie nitakujulisha.
 
Mimi nafuga kuku wa mayai mkoani , kwa sasa tumefikisha elfu moja. Maono ni kupanua kufikia kuku elfu 5 hadi 10. Naweza pata msaada wa feasibility study/ business plan kwa kiwango hiki. Ukinitumia contacts nitafafanua zaidi.
 
Back
Top Bottom