Mradi wa shamba la utotoleshaji wa vifaranga,mahitaji yanayohitajika roughly
Kuku wazazi wa mayai 1300 ,gharama ni tshs.20,800,000/=,kwa idadi hii ya kuku wazazi utahitaji incubators 4 zenye uwezo wa kubeba mayai 5280 kila moja,na kwa wiki mashine moja itaingiza mayai 1760 x 4=kwa wiki utatotolesha mayai 7040.Kuku wazazi 1130 watatoa si chini ya mayai 7210.Gharama za incubators 4 tshs.8000000/=
Gharama ya chakula mpaka kuanza kutaga ni tsh 9040000/=Gharama ya madawa na dactari ni tsh.7232000/=Utaongeza gharama za nyumba moja kwa ajili ya kutotoleshea,nyumba moja tena kwa ajili ya bruda,na nyumba nyingine kwa ajili ya kuwalelea kuku wazazi.
Utahitaji pia mixing machine kwa ajili ya kutengenezea chakula,ila haina haraka sana,kwani unaweza kuanza kwa kutengeneza manually.
Majengo unaweza ukayajenga simple kwa kuanzia na kisha ukawaajili walinzi.Pia utahitaji wafanyakazi Utahitaji wafanyakazi 5,hatchery 1,kwenye kuku wazazi 1,kwenye vifaranga 1,na kwenye utengenezaji wa chakula 2.Utahitaji pia at least ekari moja kwa ajili ujenzi wa miundo mbinu.
Mradi wa utotoleshaji wa vifaranga unalipa sana,sema tu unahitaji mtaji mkubwa wa kuanzisha biashara.