Ufugaji wa Kuku wa Kisasa: Fahamu Mbinu, Faida, Changamoto na Masoko


Thanks umenipa bonge la somo. Barikiwa sana.
 
Nataka kufuga kuku wa kienyeji,je nianze na vifaranga au matetea,nawapata wapi?nasikia wale wa singida ni wazuri sana,nataka kupeleka mtwara
 
Nataka kufuga kuku wa kienyeji,je nianze na vifaranga au matetea,nawapata wapi?nasikia wale wa singida ni wazuri sana,nataka kupeleka mtwara
Adharusi,
Kimsimsingi unaweza kuanza vyovyote, aidha vifaranga au matetea. Ila kama utaamua kuanza na vifaranga itakuwa vizuri zaidi kwa sababu ya utunzaji mzuri wa vifaranga na kuku. Kuku wakubwa matetea utunzaji wake ni mgumu kwani unakuwa huna uhakika na jinsi walivyotunzwa na kulelewa hasa ratiba ya chanjo kama ilizingatiwa, kwa mantinki hiyo, inaweza ikawa sababu ya kueneza magonjwa hapo unapofugia. Ila kama unataka kuanzia chini au mnataka kufaga katika kundi labda tuseme watu kumi ,hapo kila mfugaji atalazimika kuchangia tetea mmoja na kufunya idadi ya tetea 10, kisha mtachatachanga kila mtu elfu moja na mia tano ili kununua jogoo mmoja wa mbegu.

Mara kuku watakapoanza kutaga,mtatumia ule utaratibu wa kuwaatamisha wote kwa wakati mmoja ili watotoe kwa wakati mmoja. Ili njia hii iwezekane ni lazima tetea wote wawe wa umri mmoja na watakopoanza kutaga watataga kwa wakati mmoja hivyo itarahisisha ile sychronization na management yao.
 

Nitakutafuta kwa mawasiliano,maana nipo safarini
 
Kuku wa nyama nikipiga hesabu kama hawalipi vile
 
nahitaji machotara wenye uwenzo wa kutaga na kutamia
 
mi nahitaji kuku wa kichotara wenye uwenzo wa kutaga na kutamia
Chotara wengi wanarithi tabia ya kuku wa kisasa ya kutokuatamia mayai,hivyo kama unadili na chotara nimuhimu ukatafuta idha mashine au kuku wa kienyeji watakaofanya kazi ya kuatamia mayai yanayotagwa na kuku aina ya chotara.
 
Hello..asante kwa mara nyingine kwa nafasi ya maswali.Je ni dawa zote za kuku inapasa kutumia maji ya kisima...mto au yaliyochemshwa kuwaoea kuku...mfano newcastle.gomboro.fluban etc
 
Ahsante, Sasa Niweke Taa Kwa Vifaranga Kwa Muda Gani? Na Je? Jogoo Wa Kienyeji Akimpanda Kuku Wa Mayai Wa Kisasa, Je, Yai Litaweza Kutoa Kifahanga? Kifaranga Hicho Kikiwa Kuku Kitakuwa Na Sifa Zipi?

kuajiriwa, kujiajiri kunatoa uhuru wa kufanya kazi na kutoa maamuzi. Kuajiriwa ni utumwa na kama utapiga hesabu vizuri utagundua kuwa kuajiriwa ni hasara na pia huzuia mtu kuitumia elimu yake ipasavyo hasa ukiajiriwa serikalini. Kwa wastaafu pia wana fursa ya kutumia mafao yao vyema kwenye miradi ya ufugaji.

Kwa kuanzia tu naruhusu kuulizwa maswali kutoka kwa wale wote wanaojihusisha na ufugaji wa kuku, kama kuna jambo lolote linasumbua na kutaka kupata ufafanuzi. Pia kwa wanaohitaji kuanzisha mradi wa ufugaji wa kuku,utotoreshaji wa vifaranga,biashara ya uchanganyaji na uuzaji wa vyakula vya kuku nk , kama watanzania tunaweza kusaidiana ili hatimae tuondokane na umasikini. Kila mtu awe msaada kwa watu wengine kwa fani aliyesomea.

Karibuni kwa mjadala.[/QUOT
 



Mkuu hongera kwa ukarimu huu.
Nina swali dogo tu.
Nimenunua kuku wa kienyeji takribani siku tatu hii leo, Na hao kuku nimewatoa sehem tofauti tofauti, sasa sijui nianze kuwapa dawa gani ili niepuke magonjwa kwani wametoka sehem mbalimbali. Shukrani
 
Mkuu hongera kwa ukarimu huu.
Nina swali dogo tu.
Nimenunua kuku wa kienyeji takribani siku tatu hii leo, Na hao kuku nimewatoa sehem tofauti tofauti, sasa sijui nianze kuwapa dawa gani ili niepuke magonjwa kwani wametoka sehem mbalimbali. Shukrani
Anza kuwapa chanjo ya kideri/mdondo,kisha wape antibiotic aina ya Otc 20% changanya na Amin total kwa muda wa siku 7,kisha pumzika wiki moja kisha wape dawa ya minyoo kwa siku moja kisha pumzika siku 7 tena baada ya hapo wape coridix changanya na eggymysine.
Asante.
 

Asante mkuu,,
 

Asante kwa uzi u, naomba kulza kuku wa kienyej anayelshwa vzur anaweza kutaga mayai mangap kwa cku
 
Asante kwa uzi u, naomba kulza kuku wa kienyej anayelshwa vzur anaweza kutaga mayai mangap kwa cku
Kuku wa kienyeji si watagaji sana,hata wakati wa mzunguko wao ukifika,kila siku hutaga yai moja ingawa si lazima,inaweza ikapita siku wasitage.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…