bluetooth
JF-Expert Member
- Jan 12, 2011
- 4,402
- 2,550
huku Kibaha kuna mtu namjua anayo hii Lucerne
Kibaha Group
Ninaomba msaada wako wa jinsi ya kuwasiliana na huyo mtu
Natanguliza shukurani
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
huku Kibaha kuna mtu namjua anayo hii Lucerne
Asante mkuu,
Njia ambayo naifahamu na wengi wanatumia ni ya kutengeneza mchwa na funza kwa kutumia kinyenyesi cha Ng'ombe. Kinyesi hicho humwagiwa maji na kuwekwa kwenye mtungi na kufunikwa kwa masaa 24, baada ya hapo utatakiwa funua mtundi huo,mchwa na funza watakuwa wamejitengeneza, hivyo kuku wanaweza kuruhusiwa kula.
na mimi pia naomba niandikie namba yako pmJubilant nimekutumia kwenye private message yako ya JF
Adharusi,Nataka kufuga kuku wa kienyeji,je nianze na vifaranga au matetea,nawapata wapi?nasikia wale wa singida ni wazuri sana,nataka kupeleka mtwara
Banda la kuku 1000 nianze kwa kufyatua matofali mangapi?[/QUOT
Inategemea na aina ya banda unalotaka kujenga na mahali ulipo.Zaidi tuwasiliane kwa maelezo zaidi,
Adharusi,
Kimsimsingi unaweza kuanza vyovyote, aidha vifaranga au matetea. Ila kama utaamua kuanza na vifaranga itakuwa vizuri zaidi kwa sababu ya utunzaji mzuri wa vifaranga na kuku. Kuku wakubwa matetea utunzaji wake ni mgumu kwani unakuwa huna uhakika na jinsi walivyotunzwa na kulelewa hasa ratiba ya chanjo kama ilizingatiwa, kwa mantinki hiyo, inaweza ikawa sababu ya kueneza magonjwa hapo unapofugia. Ila kama unataka kuanzia chini au mnataka kufaga katika kundi labda tuseme watu kumi ,hapo kila mfugaji atalazimika kuchangia tetea mmoja na kufunya idadi ya tetea 10, kisha mtachatachanga kila mtu elfu moja na mia tano ili kununua jogoo mmoja wa mbegu.
Mara kuku watakapoanza kutaga,mtatumia ule utaratibu wa kuwaatamisha wote kwa wakati mmoja ili watotoe kwa wakati mmoja. Ili njia hii iwezekane ni lazima tetea wote wawe wa umri mmoja na watakopoanza kutaga watataga kwa wakati mmoja hivyo itarahisisha ile sychronization na management yao.
Banda la kuku 1000 nianze kwa kufyatua matofali mangapi?[/QUOT
Inategemea na aina ya banda unalotaka kujenga na mahali ulipo.Zaidi tuwasiliane kwa maelezo zaidi,
Mawasiliano yako tunaomba tafadhali.
nahitaji machotara wenye uwenzo wa kutaga na kutamiaNdugu yangu Da pretty,Sehemu ya kupata vifaranga wa kienyeji wenye uwezo wa kuatamia na kutotoa si shida hata ukitaka idadi zaidi ya hapo utapata.Kitu cha msingi unaweza ukatafuta namna ya kuwasiliana nami nitakuongoza.
Kuhusu risks ukiacha wizi kama ulivyosema ni kuwa,mara nyingi matatizo ya kuku ni magonjwa.Magonjwa ambayo ni common kwa kuku wa kienyeji ni pamoja na Kideri/mdondo hauna tiba ina chanjo,mafua yana tiba,Ndui(fowl pox) nayo haina tiba ila ina chanjo,Kipindupindu cha kuku(fowl cholera) ina tiba,Taifodi(fowl typoid) una tiba, Coccidiosis, una tiba pamoja ugonjwa wa homa ya matumbo kwa vifaranga(Pullorum),unatibika.
Kuhusu kutembelea wafugaji hiyo haina shida mara nyingi huwa nafanya hivyo kwa wafugaji wanaonza mradi na wale wenye matatizo, na pia wale wafugaji niliowaanzishia miradi ya ufugaji wa kuku huwa nafanya hivyo katka hali ya kuwasaidia.
Chotara wengi wanarithi tabia ya kuku wa kisasa ya kutokuatamia mayai,hivyo kama unadili na chotara nimuhimu ukatafuta idha mashine au kuku wa kienyeji watakaofanya kazi ya kuatamia mayai yanayotagwa na kuku aina ya chotara.mi nahitaji kuku wa kichotara wenye uwenzo wa kutaga na kutamia
Ndugu wana jamii forum, sasa ni wakati wa kuacha kulalamika, tunapaswa kujituma na kupiga kazi kwa bidii. Vijana graduates kutoka vyuo mbalimbali tuwaze zaidi kwenye kujiajiri kuliko kuajiriwa, kujiajiri kunatoa uhuru wa kufanya kazi na kutoa maamuzi. Kuajiriwa ni utumwa na kama utapiga hesabu vizuri utagundua kuwa kuajiriwa ni hasara na pia huzuia mtu kuitumia elimu yake ipasavyo hasa ukiajiriwa serikalini. Kwa wastaafu pia wana fursa ya kutumia mafao yao vyema kwenye miradi ya ufugaji.
Kwa kuanzia tu naruhusu kuulizwa maswali kutoka kwa wale wote wanaojihusisha na ufugaji wa kuku, kama kuna jambo lolote linasumbua na kutaka kupata ufafanuzi. Pia kwa wanaohitaji kuanzisha mradi wa ufugaji wa kuku,utotoreshaji wa vifaranga,biashara ya uchanganyaji na uuzaji wa vyakula vya kuku nk , kama watanzania tunaweza kusaidiana ili hatimae tuondokane na umasikini. Kila mtu awe msaada kwa watu wengine kwa fani aliyesomea.
Karibuni kwa mjadala.
Anza kuwapa chanjo ya kideri/mdondo,kisha wape antibiotic aina ya Otc 20% changanya na Amin total kwa muda wa siku 7,kisha pumzika wiki moja kisha wape dawa ya minyoo kwa siku moja kisha pumzika siku 7 tena baada ya hapo wape coridix changanya na eggymysine.Mkuu hongera kwa ukarimu huu.
Nina swali dogo tu.
Nimenunua kuku wa kienyeji takribani siku tatu hii leo, Na hao kuku nimewatoa sehem tofauti tofauti, sasa sijui nianze kuwapa dawa gani ili niepuke magonjwa kwani wametoka sehem mbalimbali. Shukrani
Anza kuwapa chanjo ya kidero/mdondo,kisha wape antibiotic aina ya Otc 20% changanya na Amin total kwa muda wa siku 7,kisha pumzika wiki moja kisha wape dawa ya minyoo kwa siku moja kisha pumzika siku 7 tena baada ya hapo wape coridix changanya na eggymysine.
Asante.
Ndugu wana jamii forum, sasa ni wakati wa kuacha kulalamika, tunapaswa kujituma na kupiga kazi kwa bidii. Vijana graduates kutoka vyuo mbalimbali tuwaze zaidi kwenye kujiajiri kuliko kuajiriwa, kujiajiri kunatoa uhuru wa kufanya kazi na kutoa maamuzi. Kuajiriwa ni utumwa na kama utapiga hesabu vizuri utagundua kuwa kuajiriwa ni hasara na pia huzuia mtu kuitumia elimu yake ipasavyo hasa ukiajiriwa serikalini. Kwa wastaafu pia wana fursa ya kutumia mafao yao vyema kwenye miradi ya ufugaji.
Kwa kuanzia tu naruhusu kuulizwa maswali kutoka kwa wale wote wanaojihusisha na ufugaji wa kuku, kama kuna jambo lolote linasumbua na kutaka kupata ufafanuzi. Pia kwa wanaohitaji kuanzisha mradi wa ufugaji wa kuku,utotoreshaji wa vifaranga,biashara ya uchanganyaji na uuzaji wa vyakula vya kuku nk , kama watanzania tunaweza kusaidiana ili hatimae tuondokane na umasikini. Kila mtu awe msaada kwa watu wengine kwa fani aliyesomea.
Karibuni kwa mjadala.
Kuku wa kienyeji si watagaji sana,hata wakati wa mzunguko wao ukifika,kila siku hutaga yai moja ingawa si lazima,inaweza ikapita siku wasitage.Asante kwa uzi u, naomba kulza kuku wa kienyej anayelshwa vzur anaweza kutaga mayai mangap kwa cku