Tutor B
JF-Expert Member
- Jun 11, 2011
- 9,025
- 6,598
Asante kwa kutoa nafasi ya kuuliza maswali mkuu.....mimi niliamua kuanza kufuga kuku wa kisasa wa mayai. Nina miliki kuku 199. Kwa sasa wako na umri wa wiki 27. Ni mgeni kabisa wa biashara hii. Katika mwongozo wangu inaonyesha wanatakiwa kutaga kwa 90% to 95 kwa sasa. Yaani mayai 179 mpaka 189 kwa siku. Lakini nazalisha wastani wa mayai 120 mpaka 130....nahisi kuna tatizo ingawa sijui nini shida..je nifanyeje niweze kuzidisha uzalishaji?
Chakula unachowapatia hakina virutubisho vyote kama inavyotakiwa kitaalam. Wafugaji wengi wakishachanganya pumba na mashudu basi - dagaa hakuna, premix chokaa etc. Nadhani kuna wengine watachangia