Ufugaji wa Kuku wa Kisasa: Fahamu Mbinu, Faida, Changamoto na Masoko

Ufugaji wa Kuku wa Kisasa: Fahamu Mbinu, Faida, Changamoto na Masoko

Asante kwa kutoa nafasi ya kuuliza maswali mkuu.....mimi niliamua kuanza kufuga kuku wa kisasa wa mayai. Nina miliki kuku 199. Kwa sasa wako na umri wa wiki 27. Ni mgeni kabisa wa biashara hii. Katika mwongozo wangu inaonyesha wanatakiwa kutaga kwa 90% to 95 kwa sasa. Yaani mayai 179 mpaka 189 kwa siku. Lakini nazalisha wastani wa mayai 120 mpaka 130....nahisi kuna tatizo ingawa sijui nini shida..je nifanyeje niweze kuzidisha uzalishaji?

Chakula unachowapatia hakina virutubisho vyote kama inavyotakiwa kitaalam. Wafugaji wengi wakishachanganya pumba na mashudu basi - dagaa hakuna, premix chokaa etc. Nadhani kuna wengine watachangia
 
Mkuu nina banda la 6×10 meters kiutaalam linafaa kuweka kuku wangapi wa mayai? Nashukuru mkuu
 
Asante kwa kutoa nafasi ya kuuliza maswali mkuu.....mimi niliamua kuanza kufuga kuku wa kisasa wa mayai. Nina miliki kuku 199. Kwa sasa wako na umri wa wiki 27. Ni mgeni kabisa wa biashara hii. Katika mwongozo wangu inaonyesha wanatakiwa kutaga kwa 90% to 95 kwa sasa. Yaani mayai 179 mpaka 189 kwa siku. Lakini nazalisha wastani wa mayai 120 mpaka 130....nahisi kuna tatizo ingawa sijui nini shida..je nifanyeje niweze kuzidisha uzalishaji?[/QUOTE Nipigie nikuelekeze dawa itakayopandisha utagaji ndani ya siku tano.
 
Asante kwa kutoa nafasi ya kuuliza maswali mkuu.....mimi niliamua kuanza kufuga kuku wa kisasa wa mayai. Nina miliki kuku 199. Kwa sasa wako na umri wa wiki 27. Ni mgeni kabisa wa biashara hii. Katika mwongozo wangu inaonyesha wanatakiwa kutaga kwa 90% to 95 kwa sasa. Yaani mayai 179 mpaka 189 kwa siku. Lakini nazalisha wastani wa mayai 120 mpaka 130....nahisi kuna tatizo ingawa sijui nini shida..je nifanyeje niweze kuzidisha uzalishaji?
Tanganyika, Nipigie nikuelekeze dawa itakayopandisha utagaji ndani ya siku tano.
 
Ngamba,

Ulinipm kuhusu kuku kukatwa midomo nimeeleza huko nyuma tulikotoka. Nilisema sababu mojawapo ya kuku kukatwa midomo ni kudonoana wao kwa wao pamoja na kudonoa mayai. Mara nyingi kuku hudonoana wao kwa wao kwa sababu chakula wanachokula hukosa virutubisho vya kutosha na hasa calcium na phoshorus.

Usipowahi kuwakata midomo unaweza ukapoteza kuku wengi kwa vifo. Kuku hupenda rangi nyekindu, hivyo kama ikatokea kuku mmoja kadonolowe na akatoa damu basi kuku wote katika kundi watamdonoa kuku huyo hadi atakufa.

Ni muhimu kuku wakakatwa midomo mapema zaidi kabla hali haijawa mbaya. Inashauriwa wiki ya tisa na wiki ya kumi na tano kuku wakatwe midomo. Kuku hukatwa mdomo wa juu kwa kutumia mkasi mkubwa wanaotumia mafundi kushona kukatia nguo. Kuku hukatwa mdomo wa juu na wala si wa chini kwa sababu mdomo huo wa chini humwezesha kuku kulia chakula. Ni muhimu piawakati zoezi hili linapofanyika, kuwa makini ili kuepuka kukata ulimi. Kuku akikatwa ulimi uwezekano wa kufa ni mkubwa sana.

Inashauriwa mara baada ya kuku kukatwa mdomo kisu kilicho na moto mkali kipitishwe kwenye ule mdomo uliokatwa ili kuzuia damu isiendelee kutoka.
 
Ninashukuru sana kwa majibu mazuri, kimo cha eneo langu ni futi tisa tu! Ninahitaji kufuga kuku kwaajili ya matumizi ya nyumbani zaidi, ikiwa ni pamoja na kuwarithisha watoto shughuli za ziada tofauti na masomo yao ya darasani. pia kuwajengea nmsingi wa ajira binafsi hapo baadaye. ningependa kupata mawasiliano yako ili niweze kusaidika maana ninalo shamba kubwa zaidi ya ekari 30 ambapo ningependa kuanzisha mradi huu endapo nitafuzu huu wa eneo dogo sana la nyumbani! Nitashukuru zaidi kwa ushirikiano
 
Mimi nahitaji kufuga kuku wa kinyeji nyumbani(sio shamba)kwa kuanzia vifaranga wasiozidi 50. Nina mabanda madogo tayari ila
1.sijui wapi pa kupata vifaranga vizuri vuya kienyeji ambao wakitaga watakua na uwezo wa kuatamia mayai na kuangua wakaongezeka
2.Risks za kufuga hao kuku tukiacha wizi. Yaani magonjwa kama kuna yasiyotibika au vipi maana sina uzoefu na ufugaji

Ndugu yangu tena kama unataka kuanza kufuga kuku kuanzia 50 na kuendelea waweza kuanza kuwazalisha kwa kuwaangulia nyumbani kwako. Kuna incubators za kutotoleshea mayai 48. Ni nzuri za umeme na zatumia Watts 80. Piga simu 0783503864. Bei 400,000/=. Kila la heri katika kujikwamua kiuchumi.
 
Swali langu leo ni kuhusu chakula cha kuku

Naomba msaada kuhusu fomula ya,chakula cha kuku , kuku wangu wana miezi 6 naomba fomula ya kuchanganya chakula ili niweze fanikiwa zaidi maana kununua kilichachanganywa sioni faida wakati,mwingine,kiko na uchafu mwingi
 
Asante kwa kutoa nafasi ya kuuliza maswali mkuu.....mimi niliamua kuanza kufuga kuku wa kisasa wa mayai. Nina miliki kuku 199. Kwa sasa wako na umri wa wiki 27. Ni mgeni kabisa wa biashara hii. Katika mwongozo wangu inaonyesha wanatakiwa kutaga kwa 90% to 95 kwa sasa. Yaani mayai 179 mpaka 189 kwa siku. Lakini nazalisha wastani wa mayai 120 mpaka 130....nahisi kuna tatizo ingawa sijui nini shida..je nifanyeje niweze kuzidisha uzalishaji?

Mkuu pia hakikisha Hauna Mazoea ya kuwabadilishia kuku Aina ya chakula mara kwa mara,mfano wiki hii kampuni X Next week kampuni Y..

2) Hakikisha unawapa kuku wako Vitamin angalau siku 5 kwa mwezi pamoja na dawa ya minyoo mara 1 kwa miezi mitatu...

By the way mayai 130 kwa kuku 199 ni kama 65% je utagaji.Je waliwahi kutaga kwa kiwango cha juu cha asilimia ngapi?
 
Hapo kwenye chakula sijawahi kubadirisha, dawa nawapa. Ila vitamins huwa nawapa nikifanya chanjo na nikiwapa dawa. Kuhusu kiwango cha juu ni kwamba wamewahi kufika kiwango cha juu cha 78% yaani mayai 156 ambayo ni jana tu.
 
Mkuu 78% sio mbaya sana..Muone Dr wetu Zantan kwa dawa ya kupandisha utagaji
 
Hapo kwenye chakula sijawahi kubadirisha, dawa nawapa. Ila vitamins huwa nawapa nikifanya chanjo na nikiwapa dawa. Kuhusu kiwango cha juu ni kwamba wamewahi kufika kiwango cha juu cha 78% yaani mayai 156 ambayo ni jana tu.
Nitafute kwenye namba zangu nitakushauri kuhusu formula za kutengeneza chakula na dawa ya kuwaongezea utagaji
 
Ndugu ELNIN0 hongera sana kwa biashara yako ya ufugaji wa kuku, mimi ndio nimeanza maandalizi kwa ajili ya ufugaji wa kuku, nimeweka uzio wa seng'enge kuzunguka eneo la nyumba, nimejenga mabanda mawili, moja ni futi 26x13 jingine ni futi 10x15, nimechimba kisima kirefu cha maji, pia natarajia kuongeza banda jingine la ukubwa wa futi 14x20, changamoto niliyonayo ni eneo bado halina umeme. wadau wa JF naomba ushauri wenu
 
Wanajf, Kwasasa niko mkoani Dodoma,kwa wale wafugaji wa dodoma mnaweza kunitafuta kwa msaada zaidi. Tuko pamoja kwenye ujenzi wa Taifa na kijikwamua binafsi.Ujasiriamali unalipa.
 
Back
Top Bottom