Habarini wadau,
Still niko humu jamvini.
Leo nina habari njema kwa wakazi wa Dar es salaam. Kuna semina kabambe inaratibiwa, soon nitawapa habari kamili. Mimi pia nitakuwa mjengoni siku hiyo. Nitakuwepo katika wale watakao wasilisha mada. Kaeni mkao wa kula ni semina ya siku moja kiingilio ni tsh 20000/=
Kama kweli wewe ni mfugaji ama unakusudia kuanza ufugaji basi tafadhali usikose siku hiyo. Ukikosa utakuwa umepitwa na mengi.
Wadau mbalimbali wa kuku watakuwepo siku hiyo, mabenki yanayotoa mikopo kwa wafugaji, wafugaji wakuliofanikiwa katika ufugaji watatoa ushuhuda wao siku hiyo, wanunuzi wa mazao ya kuku, watu wa mahoteli mbalimbali, supermarkets,nk madaktari na watu mbailmbali waliobobea katika tasnia ya kuku nk. Watakuwepo pia wazalishaji wa vifaranga, watengenezaji wa vyakula mbalimbali vya kuku, watengenezaji wa Incubator wa ndani ya nchi na wawakilishi wa watengenezaji wa mashine za nje.
Kila kitu utakachohitaji kukifahamu siku hiyo utafahamu. Je wajua ukitaka kuanzisha hatchery hatua gani muhimu za kufuata, nini kinahitajika na wapi uanzie, siku hiyo ni siku muafaka. Je wajua watawezaje kupunguza gharama katika ufugaji wa kuku?
Mambo yakikaa sawa tutawajulisha, lini na ukumbi gani semina hiyo itafanyika. Kwa wale watakaohitaji basi tuwasiliane kupitia namba zangu 0767989713, 0715989713 na 0786989713
Kwa pamoja tunaweza kuutokomeza umasikini.