Ufugaji wa Kuku wa Kisasa: Fahamu Mbinu, Faida, Changamoto na Masoko


Mkuu nimewasoma hapa na nimevutika sana! Maana leo nilikuwa shambani kwangu Miye ndo kwanza najiandaa kuanza ufugaji! Namiliki shamba kama eka 20 kijiji cha Kilimahewa kata ya Mkwechembe, tarafa ya Kimanzichana, wilaya ya Mkuranga mkoa wa Pwani. Kwa kuanza nimepanda mipapai ekari moja na robo. Shamba lina michungwa ya asili ilipandwa zamani bado inatoa machungwa ya kutosha.

Ninafikiria sana kuanza ufugaji wa kuku wa mayai, lakini kwa kuanza naanza na kuku wa kienyeji .
Natafuta wadau/washirika tusaidiane kupambana na umasikini.
Tafadhali nisaidie mawazo/maoni yako, napambanaje hapa!
Nipo kwa moddyguyz@yahoo.com ama 0787519910.
Natanguliza shukurani!!
 
Vp kwa kuku wanaopenda kutaga nje ya banda
Safre,
Tafadhali rejea tena sijakuelewa vuzuri swali lako, wanapenda kutaga nje ya banda au nje ya mabox ya kutagia? ni ain gani ya kuku, nadhani itakuwa ni kuku wa kienyeji na unawafuga katika mfumo wa kuwaacha huru wakijitafutia chakula wenyewe. Kama ndiyo kitu ninachokushauri ni kwamba, tengeneza box za kutagia kisha ziweze ukutani na baada hapo tengeneza kitu kama panzia vile kuyaficha yale mabox ya kutagia.

Kuku wa kienyeji ana haibu sana mara nyingi hupenda kutaga kwa kujificha. Huwa hapendi kuonwa wakati akiwa anataga.
Hii ni karibu kwa aina zote za kuku na ndio maana huwa tunashauri kwa kuku yeyeto anayetaga ni lazima wawekewa nest box na si kuwaacha tu wakiwa wanataga chini kwa huathiri hutagaji wao. Hapo ndio maana unaweza ukakuta una kuku wengi lakini wanaotaga ni wachache.
 

Suzuki Every,
Ili niweze kukusaidia lazima useme kwanza una shilingi ngapi ili tujue namna ya kukushauri maana ufugaji wa kuku unahitaji mtaji kwa ajili ya ujenzi wa mabanda, kukunulia vifaranga, nk au kama huna mtaji unaweza ukauza sehemu ya shamba lako kuna wateja ili upate pesa kwa ajili ya kutumia kama mtaji anza wa mradi wako wa ufugaji wa kuku, kama vipi naweza ukanipigia kwa ushauri zaidi.
 


Kumekuchaaa Dar es salaam. Ni tarehe 20/09/2014 ndani ya Landmark Hotel, ni semina ya aina yake kuwahi kufanyika. Nitakuwemo katika wale watakao toa mada siku hiyo. Ni fursa pekee kwa wale ambao wanaofuga na wanaohitaji kuanza kufuga nk. Karibu tukutane tuonyeshane utajiri uliojificha katika ufugaji wa kuku, hakuna haja ya kulalamika. Anza sasa kufuga kuku unufaike Kiuchumi.

Ni semina ya aina yake kwasababu mambo mengi yatahusika siku hiyo kama ambavyo yamebainishwa kwenye hilo tangazo hapo juu.

Siyo siku ya kukosa siku hiyo. Karibu nyote.
 
Wanajukwaa,
Leo nawaletea Gharama za ujenzi wa Banda lenye uwezo wa kuchukua kuku 1000 wa mayai

Ujenzi huu umetumia tofari za block, na nyumba yenyewe iko Dodoma mjini. Ina vyumba 4, store moja, Brooder ya kulelea vifaranga moja pamoja na choo.

Ukubwa wa vyumba.
1. 6.5 x 7M Chumba cha kulala kuku
2. 6.5 X 7M chumba cha kulala kuku
3. 6.5 X 7M Chumba cha kulala kuku
3. 6.5 X 7.5M Chumba cha kulala kuku
4. 3 x 5 m Stoo
5. 3x 3 m Choo

Gharama.
Gharama ya ujenzi wa banda hilo ni tshs. 12483000/=
Nikipata camera nzuri nitapiga picha kisha nitawawekea humu ndani
 
kama kweli mnania ya kuwa saidia watanzania msinge weza kuweka kiingilio tsh 20,000 mnaonekana mko kibiashara zaidi ,nini msaada wenu kwa watu wa hali ya chini ,jf ni jamvi la kuelimishana na kupeana mikakati ya jinsi ya kuondokana na umaskini pia vijana kuacha akiri potofu ya kutegemea kuajiriwa badala ya kujia jiri.
 
Kakota,
Hujalazimishwa kushiriki semina hiyo. Ni semina ya hiari kwa watu wanaoona umuhimu wake. Ukitaka msaada humu jamii forum unapatikana kitu cha msingi wewe ni kusoma hata usiogope kaka, ndio maana tuko hapa kwa ajili ya kujibu maswali mbalimbali ya wafugaji na wadau wengine wa kuku.

Kumbuka kuna gharama za ukumbi, chakula nk.
 
Mkuu tarehe 20 September naona kama ni mbali sana. Ikiwezekana ifanyike hata August. Ni mtazamo wangu tu.
 
Mkuu tarehe 20 September naona kama ni mbali sana. Ikiwezekana ifanyike hata August. Ni mtazamo wangu tu.

Urban,
Tumepanga huko ili kuwapa fursa watu waweze kujiandaa isiwe kama wameshitukizwa. Lengo yeyote anayehitaji kushiriki isionekane kama taarifa imekuwa ya ghafla. Muhimu kama mtu atahitaji kushiriki siku hiyo basi awahi kujisajiri kwani kuna hatari kama mtu atachelewa atakosa nafasi.

Kujisajili piga namba iliyo kwenye tangazo.
 
Mkuu nimefurahishwa na maelezo unayoyatoa,nimeanza ujenzi toka last month.Nimekutumia contacts zangu nategemea utanipa zako tuweze kuwasiliana zaidi kwa ajili ya mradi wangu
 
Duuh mkuu hii plan nilikuwa nayo muda mrefu mkuu .naomba tuwacliane mkuu.ili utupe shule zaidi
 
mkuu mimi ninapenda ufugaji wa kuku na ninategemea kufanya hivyo,ila naomba mawazo yako nitaanza vipi kufuga maana bado nipo chuo nasoma
 
Duuh mkuu hii plan nilikuwa nayo muda mrefu mkuu .naomba tuwacliane mkuu.ili utupe shule zaidi

Josss,
Katika lile Tangazo kuna namba za simu pale chini unaweza ukampigie mratibu wa semina hiyo kutoka shirika la Communication Solution(CoSo) atakupa habari zaidi
 
mkuu mimi ninapenda ufugaji wa kuku na ninategemea kufanya hivyo,ila naomba mawazo yako nitaanza vipi kufuga maana bado nipo chuo nasoma

de Marco,
Mimi binafsi nilikuwa nakushauri hebu concentrate kwanza kwenye kitabu ufugaji ufuate kwa sasa wewe endelea tu kujifunza zaidi kuhusu kuku ili utakapoanza ufugaji utakuwa na elimu ya kutosha kukuwezesha ufuge kwa ustadi.
 
de Marco,
Mimi binafsi nilikuwa nakushauri hebu concentrate kwanza kwenye kitabu ufugaji ufuate kwa sasa wewe endelea tu kujifunza zaidi kuhusu kuku ili utakapoanza ufugaji utakuwa na elimu ya kutosha kukuwezesha ufuge kwa ustadi.

Asante mkuu ngoja niendeleze shule kwanza pia nimefurahishwa sana na darasa hili na ningependa nijifunze zaidi
 
Kwa kuku wa kienyeji kabisa ambao siyo chotara na ambao wanafugwa kienyeji kama vile ambavyo wananchi wengi na hasa wa kijijini wanavyo wafuga kwa kuwaachia wakijitafutia chakula wenyewe.Je ni mtiririko gani wa kimatibabu unatakiwa ufuatwe ili kuwa kinga kuku na magonjwa tangu wakiwa vifaranga?.Je ufugaji wa aina hii unaweza ukatumika kwa kuku wa kienyeji ambao ni chotara endapo taratibu zote za kimatibabu zitafuatwa?.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…