Ufugaji wa Kuku wa Kisasa: Fahamu Mbinu, Faida, Changamoto na Masoko

Ufugaji wa Kuku wa Kisasa: Fahamu Mbinu, Faida, Changamoto na Masoko

Habari wandugu:
Nimejaribu kufuatilia mjadala toka mwanzo, lakini nikiri kwamba kuna uwezekano mkubwa kuna pages sijasoma.

Nimekuwa na hamu ya kuanza hii shughuli ya ufugaji wa kuku wa kisasa. Na kwa msaada wenu nimeweza kuchanganua kwa kadri niliyoweza na data nilizozipata humu na kwingineko kupata business plan. Huu chini ni mchanganuo wangu, kwa kifupi nimepiga hesabu ya kuku/vifaranga 200, halafu nikajaribu kuangalia kama unaongeza hadi 2000. Na pia nimejichukulia mimi kama muwekezaji kwa maana kwamba mimi nitaweka mtaji na kusimamia pesa lakini mtendaji/mtaalamu ni mwingine.

Kwa Ufupi:

Mahitaji:
[TABLE="width: 255"]
[TR]
[TD="colspan: 2"]Kuku (Vifaranga) 200[/TD]
[TD]TZS 260,000[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="colspan: 2"]Madawa na Chanjo[/TD]
[TD]TZS 30,000[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="colspan: 2"]Chakula jumla gunia 12[/TD]
[TD]TZS 456,000[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="colspan: 2"]Uendeshaji[/TD]
[TD]TZS 219,000[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD] [/TD]
[TD][/TD]
[TD] [/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="colspan: 2"]Total[/TD]
[TD]TZS 965,000[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
1. Gharama za kuwafuga/kuwatunza vifaranga 200 hadi unauza ni TZS 965,000
2. Ukiwauza tuseme kuku 200 kwa bei ya 5000 kwa kuku mmoja jumla unapata TZS 1,000,000.
3. Faida ni kiasi cha TZS 35,000.
4.Tuseme basi utafuga/watunza vifaranga 2000 hadi unauza basi gharama itakuwa TZS 905,000 x 10 + 200,000(mshahara) = 9,250,000
5. Faida ya kuku 2000 ni 2000x5000-9,250,000 = 750,000.

Hitimisho:
Maswali niliyonayo:
1. Gharama za madawa na chanjo kwa kuku 200 zinaweza kuzidishwa mara 10 ili kupata gharama ya kuku 2000?
2. Nimeona mshahara kwenye hii thread wa shilingi 100 kwa kuku mmoja kwa mwezi ina maana kuku 2000 kwa mwezi mshahara ni 200,000. je huu mshahara ina maana mfanyakazi anakaa kwake au anakaa na kula kwako? Je ratio ya mshahara na kazi ya kuku 2000 ipo sawa?
3. Kama unaajiri mfanyakazi kwa mwezi je ni kuku kiasi gani mfanyakazi mmoja anaweza kuwaudumia?
4.Kuhusu gaharama za banda au kupangisha banda: Nimeona kwenye hii thread kwamba banda la kuku 1000 kwa vipimo vya 15 x8 m linagharimu kama million 12 huko dodoma. Hizi gharama zipo sahii kweli?
5. Kama unapangisha ardhi ya mtu kujenga banda la size hilo la kuku 2000 inaweza kugharimu kiasi gani?
6. Kama unapangisha banda la size hiyo hapo juu linaweza kugharimu kiasi gani kwa mwezi?
7. Kuna maeneo gani mengine kwenye biashara ya kuku unaweza kupunguza gharama kama unafuga kuku wengi kama 2000 au zaidi?

Nitashukuru kwa msaada wa majibu yenu. Mchanganuo wangu wa hesabu ya kuku 200 upo hapa chini.

View attachment 180842

Mchanganuo wako ni wa kuku gani? Layers,Broiler Or Chotara?
 
Habari wandugu:
Nimejaribu kufuatilia mjadala toka mwanzo, lakini nikiri kwamba kuna uwezekano mkubwa kuna pages sijasoma.

Nimekuwa na hamu ya kuanza hii shughuli ya ufugaji wa kuku wa kisasa wa NYAMA. Na kwa msaada wenu nimeweza kuchanganua kwa kadri niliyoweza na data nilizozipata humu na kwingineko kupata business plan. Huu chini ni mchanganuo wangu, kwa kifupi nimepiga hesabu ya kuku/vifaranga 200, halafu nikajaribu kuangalia kama unaongeza hadi 2000. Na pia nimejichukulia mimi kama muwekezaji kwa maana kwamba mimi nitaweka mtaji na kusimamia pesa lakini mtendaji/mtaalamu ni mwingine.

Mkuu Ngoja nijitahidi kujibu hoja zako kwa kifupi tu;
1; Si kweli kuna gharama hubaki kama zilivyo na Zingine huongezeka lakini sio kwa Uwiano kama Unavyoonyesha...Kumbuka kuku wengi hupunguza gharama

2:Mfanyakazi ni Mapatano yenu tu na Uwezo wake binafsi.Mfanyakazi anaweza akafuga kuku kutokana na kujituma kwake tu..Sidhani kama kuna exactly figure..Kwa ufugaji wa kuku wa Nyama inategemea na mazingira ya ufugaji wako...Ila mfanyakazi ni lazima awepo Karibu na kuku muda wote.

3;Inatokana na Uwezo binafsi wa Mfanyakazi na Upatikanaji wa mahitaji mfano Maji nk

4;Hili siwezi kulijibu

5;Hapa Mtakubaliana na Mwenye Ardhi..Inategemea upo wapi..

6;Jibu linafanana na #6

7;Nafikiri maeneo yapo mengi..mfano Mshahara wa Mfanyakazi,Umeme,Maji nk..
 
Habari wandugu:
Nimejaribu kufuatilia mjadala toka mwanzo, lakini nikiri kwamba kuna uwezekano mkubwa kuna pages sijasoma.

Nimekuwa na hamu ya kuanza hii shughuli ya ufugaji wa kuku wa kisasa wa NYAMA. Na kwa msaada wenu nimeweza kuchanganua kwa kadri niliyoweza na data nilizozipata humu na kwingineko kupata business plan. Huu chini ni mchanganuo wangu, kwa kifupi nimepiga hesabu ya kuku/vifaranga 200, halafu nikajaribu kuangalia kama unaongeza hadi 2000. Na pia nimejichukulia mimi kama muwekezaji kwa maana kwamba mimi nitaweka mtaji na kusimamia pesa lakini mtendaji/mtaalamu ni mwingine.

Kwa Ufupi:

Mahitaji:
[TABLE="width: 255"]
[TR]
[TD="colspan: 2"]Kuku (Vifaranga) 200[/TD]
[TD]TZS 260,000[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="colspan: 2"]Madawa na Chanjo[/TD]
[TD]TZS 30,000[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="colspan: 2"]Chakula jumla gunia 12[/TD]
[TD]TZS 456,000[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="colspan: 2"]Uendeshaji[/TD]
[TD]TZS 219,000[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD][/TD]
[TD][/TD]
[TD][/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="colspan: 2"]Total[/TD]
[TD]TZS 965,000[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
1. Gharama za kuwafuga/kuwatunza vifaranga 200 hadi unauza ni TZS 965,000
2. Ukiwauza tuseme kuku 200 kwa bei ya 5000 kwa kuku mmoja jumla unapata TZS 1,000,000.
3. Faida ni kiasi cha TZS 35,000.
4.Tuseme basi utafuga/watunza vifaranga 2000 hadi unauza basi gharama itakuwa TZS 905,000 x 10 + 200,000(mshahara) = 9,250,000
5. Faida ya kuku 2000 ni 2000x5000-9,250,000 = 750,000.

Hitimisho:
Maswali niliyonayo:
1. Gharama za madawa na chanjo kwa kuku 200 zinaweza kuzidishwa mara 10 ili kupata gharama ya kuku 2000?
2. Nimeona mshahara kwenye hii thread wa shilingi 100 kwa kuku mmoja kwa mwezi ina maana kuku 2000 kwa mwezi mshahara ni 200,000. je huu mshahara ina maana mfanyakazi anakaa kwake au anakaa na kula kwako? Je ratio ya mshahara na kazi ya kuku 2000 ipo sawa?
3. Kama unaajiri mfanyakazi kwa mwezi je ni kuku kiasi gani mfanyakazi mmoja anaweza kuwaudumia?
4.Kuhusu gaharama za banda au kupangisha banda: Nimeona kwenye hii thread kwamba banda la kuku 1000 kwa vipimo vya 15 x8 m linagharimu kama million 12 huko dodoma. Hizi gharama zipo sahii kweli?
5. Kama unapangisha ardhi ya mtu kujenga banda la size hilo la kuku 2000 inaweza kugharimu kiasi gani?
6. Kama unapangisha banda la size hiyo hapo juu linaweza kugharimu kiasi gani kwa mwezi?
7. Kuna maeneo gani mengine kwenye biashara ya kuku unaweza kupunguza gharama kama unafuga kuku wengi kama 2000 au zaidi?

Nitashukuru kwa msaada wa majibu yenu. Mchanganuo wangu wa hesabu ya kuku 200 upo hapa chini.

View attachment 180842

Kuhusu Mchanganuo wako naona Haupo Sahihi Kabisa kwa kiwango kikubwa...Mfano Ndoo 5 za maji kila siku haiwezekani sababu kuku wakiwa wadogo hawanywi maji sawa na wakikua..
Pia madawa kwa 30,000 upo juu sana...Chakula Maximum ni Gunia 8-9 kama utawauza kuku wako wiki 4.5...
Uendeshaji wa 219,000 unalipa mtu wa Certificate/Diploma??
 
Mkuu Pachanya,
Hasante kwa mchango wako, hii inaongeza matumaini kwamba inawezekana kufanya hii biashara na ukapata faida.
Na kama ulivyosema kuhusu "Kumbuka kuku wengi hupunguza gharama". Katika hili la kuku wengi na kupunguza gharama ndio eneo ambalo linahitaji majaribio zaidi au michango zaidi kutoka kwa wengine.
 
Mkuu, Hasante sana kwa maangalizo yako.
hilo eneo la maji na gharama za umeme ni maeneo ambayo sijapata taharifa za kutosha.
Hayo yalikuwa makisio kutoka kwa watalaamu "kiboko.co.tz". Tena na wao walikosea kwenye bei ya ndoo moja ya maji. Beo yao waliweka ni TZS 50 wakati kuna mdau mwingine akanisahisha kwamba ni yeye yuko Mbezi na ananunua ndoo moja kwa TZS 500.
Kwa msingi huo basi nakubaliana na wewe kuhusu eneo la maji, nitaliangalia hili kwa upana wake labda wakati mradi umeanza.

Kuhusu madawa, pia nahisi kuna haja ya marekebisho. Lakini bado sijapata bei zitakazohakisi kuku 2000. Kwa niliowaulizia wanasema ni kati ya 18,000 hadi 25,000 inategemea. Na jamaa mmoja akaniambia idadi ya kuku mara nyingi haimaanishi kwamba uongeze manunuzi ya dawa. Alisema pale anaponunua dawa yeye huwa wanamuulizia za kuku wangapi. Na kwa mujibu wake yeye mara nyingi gharama huwa palepale iwe kuku 300 au 500.

Gharama za uendeshaji zilijumlisha pia umeme, kodi ya pango, na mengineyo. ndio maana ipo hivyo. Lakini hapo ndipo pana haja ya kuongeza umakini na udadisi wa hali ya biashara na kwa kwa jinsi gani wengine wanagharamia haya mambo.
 
dah! inatia moyo sana. Nami nataka kuingia kwenye biashara hii. Nataka nianze na kuku 400 wa nyama, kasha baadae nitaongeza. Ninayo maeneo ambayo nitaweza jenga mabanda. Bi mkubwa ana kiwanja kwa sasa kimekaa tu, hivyo nitakitumia kwa muda. Nimeongea na baadhi ya watu wanaofanya hii biashara, kwa kweli ukifuata misingi, unatoka kabisa. Nataka iwe ni full time job kwangu, sikusomea mambo ya ufugaji ila natumai nitapata tuition ya kutosha toka kwa wajuzi. Nimechoka kweli kuwa mtaani, nina shahada ya IT (Information systems management) ila kazi kupata imekuwa shughuli kwa kina sisi tusio na wahusika uko juu. Hivyo nimedhamiria kujikita huku, kuna ndugu yangu mpendwa kaniahidi msaada wa kapito ndani ya miezi kadhaa.
 
Wadau,

Poleni na majukumu ya kupambana na umasikini.Ile semina yetu ya Landmark Hotel imepelekwa mbele hadi mwezi wa kumi na mojatarehe 15/11/2014. Kwa mawasiliano zaidi mpigie mratibu wa semina hiyo kutoka shirika la Communication SolutionMadam Sekela MS kwa namba 0786427797.

Wakazi wa Songea tutakuwa na mafunzo kama hayoTarehe 11/10/2014, katika ukumbi wa Roman Catholic maeneo ya Bombambili, nyote mnakaribishwa. Kwa ajili ya kujiandikisha/kulipia fika mtaa wa Zanzibar jengo la CCM kwa Bwana Siphael Mgeni, wakala wa kusambaza vifaranga Bora Songea. Kiingilia ni tsh elfu kumi tu.

Tarehe 20/09/2014 na 21/09/2014 tutakuwa Singida katika wilaya ya mkalama, maeneo ya Iguguno katika ukumbi wa Amcoss. Pale tutatoa mafunzo kwa ajili ya project maalum ambayo watakao pata mafunzo watapewa vifaranga wa kuku wa kienyeji walioboreshwa watawafuga kisha ,kuku hao watakapokuwa wakubwa, shirika la Hisa Microfinance and Community Development Ltd lililofadhili mafunzo hayo watawanunua kuku wote kutoka kwa wafugaji hao na kwenda kuwauza huko walikotafuta masoko.
Mjadala uendelee na tuko pamoja.

KUKU WA KIENYEJI
Kuku wa kienyeji wamekuwa wakifugwa takribani na kila kaya hapa kwetu Tanzania. Kwa mujibu wa takwimu za mifugo zilizotolewa na wizara ya maendeleo ya mifugo na Uvuvi, Inakadiriwa kuwa Tanzania ina kuku wa asili wapatao milioni 34. Idadi hii ya kuku ni pungufu mara 1.3 ya idadi ya watu. Kwa mujibu wa Sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012, iliyoendeshwa na Idara ya takwimu Tanzania, inaonyesha kuwa Tanzania ina jumla ya watu 44,929,000/=. Hii inamaanisha kwamba idadi ya watu waliopo ni kubwa kuliko kuku wanaofugwa nchini kwetu na kama mfugaji atatazama kwa jicho la kijasiriamali na uchumi hii ni fursa, na fursa hii kama ikitumiwa vyema inaweza kuongeza kipato cha mfugaji na kuberesha kiwango chake cha maisha na kufanya ile kauli mbiu ya maisha bora kwa kila mtanzania itimie.

Kuku wa kienyeji wana soko kubwa hapa nchini kwetu Tanzania. Watu wengi huwapendelea kuku hao kutoka na kuwa na ladha nzuri wanapoliwa ukilinganisha na kuku wa kisasa. Ongezeko la hotel za kitalii, supamaketi, cafeteria, wapika chipsi mitaani nk kumeongeza Zaidi mahitaji ya kuku na hivyo kutoa soko la uhakika la kuku hao . Vile vile sherehe mbalimbali mfano, krismass, kipaimara, Idd el fitri, Idd al hajj, harusi, maafali nk kunawafanya kuku wa kienyeji wawe na thamani kubwa kutokana na mahitaji yake kuongezeka kila siku.

Sifa ya kuku wa kienyeji ni kuwa kwanza ni mstahimilivu dhidi ya magonjwa, ufugaji wake ni rahisi ukilinganisha na kuku wa kisasa, wanauwezo wa kula chakula cha kawaida kinachoweza kutengenezwa kwa malighafi zinazopatikana katika mazingira yetu tunayoishi.

Ufugaji wa kuku wa kienyeji, hatahivyo, unakabiliwa na changamoto kadhaa zikiwemo kukosekana kwa mfumo maalum masoko kwa ajili ya kuuzia kuku. Mara nyingi kuku hawa wanapokuwa tayari kuuzwa wafugaji huuziana kienyeji kitu ambacho hufanya mfugaji azidiwe nguvu ya ushawishi na mnunuzi hivyo kusababisha mnunuaji anunue kwa bei chini, bei ambayo kimsingi humkandamiza zaidi mfugaji na kumnufaisha mnunuaji. Changamoto nyingine ni uzalishaji mdogo wa kuku, kunakosababishwaa na kukithiri kwa vifo vinavyotokana na magonjwa, wezi pamoja na wanyama wakali hasa kama ufugaji huo ukifanywa huria. Chakula c duni pamoja na ukosefu wa maarifa ya utunzaji bora wa kuku, kukosekana kwa mtandao wa taarifa, umoja miongoni mwa wafugaji wa kuku, vyama vya wafugaji wa kuku vilivyopo havina nguvu wala ushawishi katika kufanya maamuzi huzidisha changamoto katika ufugaji wa kuku hao wa kienyeji. Changamoto zote hizo kwa pamoja hupunguza ari ya wafugaji kufuga kuku wengi.

Ili kukabiliana na changamoto hizi, ni muhimu kwa serikali, masharika yasiyo ya kiserikali, taasisi pamoja na wadau mbalimbali katika tasnia ya ufugaji wa kuku wa kienyeji, kutafuta njia mbadala za pamoja za kuwaongezea wafugaji maarifa ya ufugaji bora wa kuku, namna ya kuongeza uwingi na ubora wa kuku na mazao yake na pia kuchangia kuendeleza mnyoro wa thamani katika tasnia ya kuku Tanzania.

Kwa ajili ya kuboresha kosaafu ya kuku wa kienyeji wafugaji wanashauriwa kufuga kuku walioboreshwa na hivyo kuwa na kuku wazuri machotara wenye kukua haraka na utagaji wenye tija.
 
mie.nina mpango wa kujiajir..na napenda ufugaji..huo wa kuku...haswa wa kienyeji na wanyama....ila nahitaji mafunzo kwanza..je wapi unanishauri nianzie?kwasasa nipo zanzibar...
 
Aman Ng'oma ili kuku wawe vizuri kuku 50 wanahitaji banda la ukubwa gani kuku wa kinyeji.
 
Last edited by a moderator:
Kutokana na sebabu zilizo nje ya uwezo wetu, ile Semina ya ufugaji bora wa kuku sasa kufanyika tarehe 01/11/2014 badala ya kuhairishwa tarehe 27/09/2014, tunaomba radhi kwa usumbu uliojitokeza.

Kwa taarifa kamali pitia tangazo hilo hapo chini au piga 0767989713/0715989713 au kwa mratibu wa semina hiyo kwa namba 0655663900

IMG-20140926-WA0000.jpg

Tarehe 11/10/2014, kutakuwa na semina kama hiyo Songea katika ukumbi wa Familia Takatifu Bombambili, tiketi zinapatikana kwa bwana Siphael Mgeni, wakala maarufu wa kusambaza vifaranga wa kuku mkoani Ruvuma anapatikana mtaa wa Zanzibar jengo la CCM, au waweza mpigia kwa simu namba 0717705614 au 0684812938.

Kwa ufugaji wenye tija, unakaribishwa katika semina .

SONGEA.jpg
 
Mkuu, naomba mawasiliano yako, au kama vipi nitumie text kwa 0652590519 will call you. thanx.

Ndugu wana jamii forum, sasa ni wakati wa kuacha kulalamika, tunapaswa kujituma na kupiga kazi kwa bidii. Vijana graduates kutoka vyuo mbalimbali tuwaze zaidi kwenye kujiajiri kuliko kuajiriwa, kujiajiri kunatoa uhuru wa kufanya kazi na kutoa maamuzi binafsi tena kwa wakati. Kuajiriwa kimsingi hakuna tofauti na utumwa na kama utapiga hesabu vizuri utagundua kuwa kuajiriwa ni hasara na pia huzuia mtu kuitumia elimu yake ipasavyo hasa ukiajiriwa serikalini. Kwa wastaafu pia wana fursa ya kutumia mafao yao vyema kwenye miradi ya ufugaji.

Kwa kuanzia tu naruhusu kuulizwa maswali kutoka kwa wale wote wanaojihusisha na ufugaji wa kuku, kama kuna jambo lolote linasumbua na kutaka kupata ufafanuzi. Pia kwa wanaohitaji kuanzisha mradi wa ufugaji wa kuku,utotoreshaji wa vifaranga,biashara ya uchanganyaji na uuzaji wa vyakula vya kuku nk , kama watanzania tunaweza kusaidiana ili hatimae tuondokane na umasikini. Kila mtu awe msaada kwa watu wengine kwa fani aliyesomea.

Karibuni kwa mjadala.
 
Wadau wangu katika hii mada msione kimya niko kijijini mara moja kama ambavyo mnajua miundominu yetu vijijini ni shida hasa kwenye upande wa umeme.
 
Back
Top Bottom