Mtaji sio tatizo, sehem sio tatizo, tatizo ni mtu wa kumkabidhi shughuli hy mnk sina muda wa kukaa huko shamba, unao vijana wazuri?
Ngosha,
Kwa kushirikiana na shirika la Ndurumo, tunaendesha mafunzo kwa vijana wa kitanzania wenye ari ya kufanya kazi kwa weredi na kujituma. Hawahitaji kusukumwa katika kutekeleza majukumu yao, ni waaminifu, wachapakazi na wanaojua wajibu wao. Tunawafundisha namna ya kuwahudumia kuku hatua kwa hatua, udhibiti wa magonjwa na kuyajua magonjwa hatari ya kuku dalili zake, kuenea kwake na namna ya kuyazuia. Pia huwa tunawapeleka kwenye mafunzo kwa vitendo katika mashamba mbalimbali ya watu ambao tunawasimamia miradi yao kwa ajili ya kupata uzoefu zaidi.
Vijana hawa kwakweli wanaopenda kazi, siyo wavivu, wapo wanaotoka kigoma, ambao huwa wao hupenda kufanya kazi kwa mkataba, kwamba wanaweza wakakufanyia kazi kwa muda wa mwaka mzima bila kudai malipo yoyote kisha mwisho wa mwaka ukawlipa mishahara yao yote kama lump sum. Wengine kutoka Songea, Iringa na dodoma nk.
Kwa kuwa tunawafanyia training, kila ambaye atawahitaji atawalipia laki 2.5 kwa kila kijana mmoja kama gharama za mafunzo.
Ikiwa una kijana/vijana wako, na ungependa wawe weredi katika kusimamia na kuhudumia kuku unaweza kumlete/kuwaleta kwetu na tukawapatia mafunzo ya ufugaji bora wa kuku, mafunzo hayo hufanyika kwa muda wa wiki 4, wiki moja darasani na wiki tatu nyingine wanakuwa field/ mafunzo kwa vitendo.
Kijana mmoja anauwezo wa kuwahudumia kuku 1000 kwa umakini na uangalifu wa hali ya juu ikiwa ni pamoja na kudhibiti. Wako tayari kufanya kazi kwa mshahara wa laki moja wa kuanzia
Kama utahitaji pia vijana wenye certificate za afya ya wanyama na uzalishaji unaweza ukawasiliana nami na utawapata vijana hao ambao ni weledi katika tasnia ya mifugo. Siku zote rahisi ni ya ghali.