Ufugaji wa Kuku wa Kisasa: Fahamu Mbinu, Faida, Changamoto na Masoko

Ufugaji wa Kuku wa Kisasa: Fahamu Mbinu, Faida, Changamoto na Masoko

Kuku wa kienyeji kama wanafugwa huria wanatumia gharama ndogo sana. Cha msingi anapototoa unamnyang'anya vifaranga ndani ya wiki mbili ili aanze kutaga tena. Kuku wa kisasa wana gharama kubwa.
 
Mtaalamu wa huduma za mifugo (veterinary services) anapatikana hapa. Huduma nitoazoni ushauri wa ufugaji bora, kutibu mifugo inayoumwa, kuchanja mifugo ili kuzuia magonjwa, kuchunguza na kugundua ugonjwa uliomuua mfugo wako kama wewe hufahamu ili utibu waliobaki, kupandisha kwa chupa (A.I) kwa wale wafugaji wa ng'ombe, kuhasi vidume vya mifugo kama vile nguruwe, ng'ombe, mbuzi, kondoo pamoja na huduma nyingine nyingi. Kama umegundua unahitaji huduma yangu usisite kunitafuta kwa namba 0786909993, makazi yangu ni morogoro na Dodoma. Kauli mbiu yangu ni "Uliza, Utajibiwa, Utahudumiwa" Karibuni sana.
 
Wanabodi, nauza mayai ya kuku wa kisasa tray moja ni Tshs elfu sita tu kwa bei ya jumla na reja reja ni elfu saba kwa tray, kwa anaehitaji ni PM namba yako tuwasiliane. Angalizo mi nipo Dar es salaam
 
Je viranga hawa wana wiki ngapi? Na husaidia nini kuwaweka hao kuku katika chanja au kuwaeka chini tu na kuwawekea maranda ya mbao katika kipindi cha udogo.
 
Mkuu naona shule hapo imetulia........!

Lakini mbona mnazungumzia haya makuku ya kisasa tu? Je, ufuguja wa kitaalam wa kuku wa KIENYEJI unakuwaje? Kumbuka hawa nao wana soko zuri sana..........!

Mkuu kuna thread moja humu ndani ilirushwa mwaka jana ina nondo za kufa mtu kuhusiana na ufugaji wa kuku wa kienyeji, mimi nilikopi hizo nondo nilizi-save kwenye pc yangu nazitumia kama msahafu kwenye shamba langu la kuku wa kienyeji, nikiipata hiyo thread nakupa link
 
wafugaji wenzangu, kwa wale wanaohitaji vifaranga vya kuku wa kisasa wa nyama Broilers wasiliana nami kwa kutuma private message (inbox me)
Karibu

Mkuu hizo bei za vifaranga zikoje kwa sasa? ?
 
NAFASI INAYOHITAJIKA KWA KUKU 1000 WENYE RIKA TOFAUTI (MABANDA YA KUKU)

[TABLE="class: grid, width: 500, align: center"]
[TR]
[TD]RIKA[/TD]
[TD]CHICKS

VIFARANGA[/TD]
[TD]
GROWERS

KUKU
WANAOKUWA
[/TD]
[TD]LAYERS

KUKU
WANAOTAGA[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]UMRI
KTK
WIKI
[/TD]
[TD]0-6[/TD]
[TD]7-20[/TD]
[TD]20-80[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]KUKU/ENEO LA
M[SUP]2 [/SUP]MOJA ZA MRABA

[/TD]
[TD]12[/TD]
[TD]9[/TD]
[TD]6[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]M[SUP]2 [/SUP]ZINAZOHITAJIKA
/KUKU 1000

[/TD]
[TD]83.7M[SUP]2[/SUP][/TD]
[TD]111.2M[SUP]2[/SUP][/TD]
[TD]166.6M[SUP]2[/SUP][/TD]
[/TR]
[TR]
[TD][/TD]
[TD][/TD]
[TD][/TD]
[TD][/TD]
[/TR]
[/TABLE]

Eneo watakaloshinda kuku 1000 wakati wa mchana, ambao hufugwa ktk mfumo wa nusu huria ni mita za mraba 10,000 .Hii inamaana kwamba ,kuku mmoja anahitaji eneo lenye mita za mraba 10.Kuhusu utagaji kuku wa kienji hana sifa ya utagaji wa mayai mengi.Kuku wa kienyeji hutaga kwa mzunguko.Kila mzunguko mmoja hutaga hutaga wastani wa mayai 15 na kuanza kuatamia,kutotoa na kulea vifaranga.Mzunguko huo huchukua wastani wa kipindi cha miezi 4 hadi 6 .Hali hiyo hiyo humfanya atage mayai machache kati ya mayai 30 hadi 60 kwa mwaka ukilinganisha na kuku wa kisasa ambao hutaga mayai 270 hadi 300.

Kuku wa kienyeji ukitaka watage mayai mengi wasiruhusiwa kuatamia,kila mayai yanayotagwa yaokotwe na kuhifadhiwa na kama mfugaji atahitaji kutotoresha, kama kuna kuku wengi ,ni vyema ikatumika machine ili kuzalisha vifaranga wengi zaidi.Kuku wa kienyeji anapokuwa kwenye mzunguko wa utagaji,kila siku hutaga yai moja.

Mawasiliano yangu nimekutumia kwenye private message yako ya jf,nenda kwenye notification yako fungua utaona.

naomba contacts zenu
 
Ufugaji wa kuku wa mayai unachangamoto kidogo hasa kama utawalisha chakula chenye upungufu wa virutubisho. Mara nyingi kuku wa mayai wakika chakula chenye upungufu wa virutubisho hisababisha utagaji kushuka au ambao hawajaanza kutaga huwafanya wachelewwe kutaga, huwafanya wadonoane, lakini wakati mwingine kuku hufa wakati wa utagaji kutokana na kupasukia mayai tumboni.

Mayai hupasukia tumboni kutokana na kuku kula chakula vhenye upungu wa madini ya calcium na hivyo kulifanya yai liwe tepetepe na wakati wa kutaga yai hilo hupasuka kabla ya kutoka nje.

JE UNACHANGAMOTO YOYOTE INAKUKABILI, HEBU ILETE TUIJADILIBKWA PAMOJA
 
Sababu zinazowafanya kuku ashushe utagaji ni pamoja na zifuatazo
Kwanza ugojwa. Kuku akiwa mgonjwa dalili ya kwanza kushusha utagaji mfano wa wagonjwa yanayosababisha ushukaji wa utagaji ni pamoja na Typhoid, minyoo, Utitiri, Chawa, Mafua nk.

Pili Chakula. Chakula kina mchango mkubwa katika utagaji wa kuku. Kuku wakilishwa chakula kizuri husaidia kuongeza utagaji.

Mndikano wa kuku. Kuku wanatakiwa wakae kulingana na ukubwa wabanda. Kuku wakiwa wengi kuliko nafasi inayotakiwa. Kwa kuku wa mayai mita square 1 ni kwa kuku 5-6.

Kumlisha kuku bila kumpimia chakula. Kuku wa mayai anatakiwa apimiwe chakula ili asiwe mnene kupita kiasi. Kuku mnene sana si mtagaji kwakuwa anakuwa amejaza mafuta mengi mwilini kwake na hata sehemu utagaji wake.
 
Ndugu wana jamii forum, sasa ni wakati wa kuacha kulalamika, tunapaswa kujituma na kupiga kazi kwa bidii. Vijana graduates kutoka vyuo mbalimbali tuwaze zaidi kwenye kujiajiri kuliko kuajiriwa, kujiajiri kunatoa uhuru wa kufanya kazi na kutoa maamuzi binafsi tena kwa wakati. Kuajiriwa kimsingi hakuna tofauti na utumwa na kama utapiga hesabu vizuri utagundua kuwa kuajiriwa ni hasara na pia huzuia mtu kuitumia elimu yake ipasavyo hasa ukiajiriwa serikalini. Kwa wastaafu pia wana fursa ya kutumia mafao yao vyema kwenye miradi ya ufugaji.

Kwa kuanzia tu naruhusu kuulizwa maswali kutoka kwa wale wote wanaojihusisha na ufugaji wa kuku, kama kuna jambo lolote linasumbua na kutaka kupata ufafanuzi. Pia kwa wanaohitaji kuanzisha mradi wa ufugaji wa kuku,utotoreshaji wa vifaranga,biashara ya uchanganyaji na uuzaji wa vyakula vya kuku nk , kama watanzania tunaweza kusaidiana ili hatimae tuondokane na umasikini. Tukitaka kuyaona maendeleo ya kweli, kila mtu awe msaada kwa watu wengine kwa fani aliyesomea.

Karibuni kwa mjadala.

Yai likichafuliwa na kinyesi litafaa kutotolewa?na km ni chafu kuna njia mbadala ya kulisafisha likatotolewa?
 
Yai likichafuliwa na kinyesi litafaa kutotolewa?na km ni chafu kuna njia mbadala ya kulisafisha likatotolewa?

Kuku wa Kabanga, yali likichafuliwa kwa kinyesi wakati wa utagaji ili liweze kutotolewa vyema kwanza linahitaji lisafishwa kwa kitambaa kisafi na kikavu kama litakuwa limelowa kenyesi na kama kenyesi ni kikavu kimegandamana kwenye yai itabidi utafutwe mti uchongwe kisha yai liparazwe kuondoa kenyesi kisha liatamishwe.

Unyevunyevu husababisha yai livamiwe na wadudu.

Hakikisha yai la kutotolewa halikutani na maji.

Ni muhimu mayai kutibiwa kabla ya kuingizwa katika mashine kwa ajili ya kuua wadudu.
 
Ndugu wana jamii forum, sasa ni wakati wa kuacha kulalamika, tunapaswa kujituma na kupiga kazi kwa bidii. Vijana graduates kutoka vyuo mbalimbali tuwaze zaidi kwenye kujiajiri kuliko kuajiriwa, kujiajiri kunatoa uhuru wa kufanya kazi na kutoa maamuzi binafsi tena kwa wakati. Kuajiriwa kimsingi hakuna tofauti na utumwa na kama utapiga hesabu vizuri utagundua kuwa kuajiriwa ni hasara na pia huzuia mtu kuitumia elimu yake ipasavyo hasa ukiajiriwa serikalini. Kwa wastaafu pia wana fursa ya kutumia mafao yao vyema kwenye miradi ya ufugaji.

Kwa kuanzia tu naruhusu kuulizwa maswali kutoka kwa wale wote wanaojihusisha na ufugaji wa kuku, kama kuna jambo lolote linasumbua na kutaka kupata ufafanuzi. Pia kwa wanaohitaji kuanzisha mradi wa ufugaji wa kuku,utotoreshaji wa vifaranga,biashara ya uchanganyaji na uuzaji wa vyakula vya kuku nk , kama watanzania tunaweza kusaidiana ili hatimae tuondokane na umasikini. Tukitaka kuyaona maendeleo ya kweli, kila mtu awe msaada kwa watu wengine kwa fani aliyesomea.

Karibuni kwa mjadala.

nielezee kuhusu battery farming system
 
Back
Top Bottom