Je viranga hawa wana wiki ngapi? Na husaidia nini kuwaweka hao kuku katika chanja au kuwaeka chini tu na kuwawekea maranda ya mbao katika kipindi cha udogo.
Mkuu naona shule hapo imetulia........!
Lakini mbona mnazungumzia haya makuku ya kisasa tu? Je, ufuguja wa kitaalam wa kuku wa KIENYEJI unakuwaje? Kumbuka hawa nao wana soko zuri sana..........!
wafugaji wenzangu, kwa wale wanaohitaji vifaranga vya kuku wa kisasa wa nyama Broilers wasiliana nami kwa kutuma private message (inbox me)
Karibu
NAFASI INAYOHITAJIKA KWA KUKU 1000 WENYE RIKA TOFAUTI (MABANDA YA KUKU)
[TABLE="class: grid, width: 500, align: center"]
[TR]
[TD]RIKA[/TD]
[TD]CHICKS
VIFARANGA[/TD]
[TD]
GROWERS
KUKU
WANAOKUWA
[/TD]
[TD]LAYERS
KUKU
WANAOTAGA[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]UMRI
KTK
WIKI
[/TD]
[TD]0-6[/TD]
[TD]7-20[/TD]
[TD]20-80[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]KUKU/ENEO LA
M[SUP]2 [/SUP]MOJA ZA MRABA
[/TD]
[TD]12[/TD]
[TD]9[/TD]
[TD]6[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]M[SUP]2 [/SUP]ZINAZOHITAJIKA
/KUKU 1000
[/TD]
[TD]83.7M[SUP]2[/SUP][/TD]
[TD]111.2M[SUP]2[/SUP][/TD]
[TD]166.6M[SUP]2[/SUP][/TD]
[/TR]
[TR]
[TD][/TD]
[TD][/TD]
[TD][/TD]
[TD][/TD]
[/TR]
[/TABLE]
Eneo watakaloshinda kuku 1000 wakati wa mchana, ambao hufugwa ktk mfumo wa nusu huria ni mita za mraba 10,000 .Hii inamaana kwamba ,kuku mmoja anahitaji eneo lenye mita za mraba 10.Kuhusu utagaji kuku wa kienji hana sifa ya utagaji wa mayai mengi.Kuku wa kienyeji hutaga kwa mzunguko.Kila mzunguko mmoja hutaga hutaga wastani wa mayai 15 na kuanza kuatamia,kutotoa na kulea vifaranga.Mzunguko huo huchukua wastani wa kipindi cha miezi 4 hadi 6 .Hali hiyo hiyo humfanya atage mayai machache kati ya mayai 30 hadi 60 kwa mwaka ukilinganisha na kuku wa kisasa ambao hutaga mayai 270 hadi 300.
Kuku wa kienyeji ukitaka watage mayai mengi wasiruhusiwa kuatamia,kila mayai yanayotagwa yaokotwe na kuhifadhiwa na kama mfugaji atahitaji kutotoresha, kama kuna kuku wengi ,ni vyema ikatumika machine ili kuzalisha vifaranga wengi zaidi.Kuku wa kienyeji anapokuwa kwenye mzunguko wa utagaji,kila siku hutaga yai moja.
Mawasiliano yangu nimekutumia kwenye private message yako ya jf,nenda kwenye notification yako fungua utaona.
naomba contacts zenu
Ndugu wana jamii forum, sasa ni wakati wa kuacha kulalamika, tunapaswa kujituma na kupiga kazi kwa bidii. Vijana graduates kutoka vyuo mbalimbali tuwaze zaidi kwenye kujiajiri kuliko kuajiriwa, kujiajiri kunatoa uhuru wa kufanya kazi na kutoa maamuzi binafsi tena kwa wakati. Kuajiriwa kimsingi hakuna tofauti na utumwa na kama utapiga hesabu vizuri utagundua kuwa kuajiriwa ni hasara na pia huzuia mtu kuitumia elimu yake ipasavyo hasa ukiajiriwa serikalini. Kwa wastaafu pia wana fursa ya kutumia mafao yao vyema kwenye miradi ya ufugaji.
Kwa kuanzia tu naruhusu kuulizwa maswali kutoka kwa wale wote wanaojihusisha na ufugaji wa kuku, kama kuna jambo lolote linasumbua na kutaka kupata ufafanuzi. Pia kwa wanaohitaji kuanzisha mradi wa ufugaji wa kuku,utotoreshaji wa vifaranga,biashara ya uchanganyaji na uuzaji wa vyakula vya kuku nk , kama watanzania tunaweza kusaidiana ili hatimae tuondokane na umasikini. Tukitaka kuyaona maendeleo ya kweli, kila mtu awe msaada kwa watu wengine kwa fani aliyesomea.
Karibuni kwa mjadala.
Yai likichafuliwa na kinyesi litafaa kutotolewa?na km ni chafu kuna njia mbadala ya kulisafisha likatotolewa?