Richard Mallya
Member
- Jul 20, 2016
- 36
- 33
Wazo nzuri sana ila kazi ipo apo kwenye kushirikiana inabidi kumtafuta mtu ulie nae karibu na ufahamu tabia zake kwa undani nae awe nakupata kwa ndani
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Karibu Honda XP, ushauri wa miradaji ya ufugaji ndiyo kazi yangu siwezi kuiacha, still niko hewani sema nimesimama kidogo kuendelea kuandika since naona karibu mambo mengi tumeyakava.Huu Uzi, ndo nauona Leo, nilipoangalia vizuri nikagundua ni wa tangu 2012. Nikawa na hofu, mleta Uzi tangu wakati huo atakuwa bado anatoa ushauri huu alioahidi hadi sasa?
Hivyo ikanilazimu kufuatilia hadi mwisho kujua aliishia mwaka gani? Nimefarijika kukuta kuna post hadi za sasa mleta Uzi bado anajibu changamoto za wafugaji na kutoa ushauri na Huduma mbalimbali.
Aman, hongera sana kwa Uzi huu! Nimejifunza mengi, lakini pia nakukumbuka kwa wema wako, niliwahi kukupigia simu juu ya Ufugaji wa mbuzi, kama miaka 3 hivi iliyopita, ulinishauri vizuri na kwa wema kabisa. Nina imani wewe bado ni MTU wa msaada.
Nitakutafuta kuhusiana na Ufugaji wa Kuku, maana nishaanza hatua za awali za kutafuta eneo nje ya mji, kwani nataka Ufugaji huria, mabanda na nyumba ya mfanyakazi, na kisima cha maji. Maana nimejipanga kufanya Ufugaji mkubwa wa kibiashara,
Nitakutafuta kwa simu/,email.
Asubuhi njema.
Slim5,
Ni matumaini yangu kuwa mzima. Nashukuru kwa maswali yako lkn naomba uniwie radhi kwa kuchelewa kukujibu. Banda lenye Square meta 140 kama ni kuku wa kienyeji unataka kufuga kwa ajili ya kuwafanya watagaji basi eneo hili litawatosha kuku 1120 maximum na Minimum Kuku 700. Lakini pia eneo hilo kama utamua kufuga kuku hao kwa ajili ya nyama kwa maana baada ya wiki miezi 3 au 4 unawauza basi utakuwa na uwezo wa kufuga kuku hadi 2100.
Kwa eneo la square mita 90 utafuga kuku 750 maximum na Minimum 500 kama utawafuga kwa ajili kuwafanya watagaji.
Ushauri wangu ni kuwa kama unataka kufanya Ufugaji wa Kibiashara fuga kuku chotara. unaweza kupata wale cross breed ya Pure line ya Rhode Island Red na Local wakwetu, au wale kuku weusi wa malawi nk, au Ukapata ile breed ya kenya na Uganda Kuroiler ukafuga hao utaiona faida ya ufugaji. Lakini kama utasema ufuge kuku pure wa kienyeji hawatakulipa kwakuwa ukuwaji wao pamoja uzalishaji wao ni mdogo ukilinganisha na gharama za uzalishaji.
Asante
Nategemea kufugakufugakama 300 aina yainaroilkuroileriilizniwauzeapasakani.maana maishamaishategekutegemeaamshaharamyanaumizakwakuwkwakuwaunitakuwa mgeniakatikajufugajiunitakuwaumbua sana kwa kuanzamaswali akuhusianagajiufugajiu
Upo Mkoa gani?Ndugu wana JF habari za majukumu ya kulijenga Taifa letu , mi ni mmoja wa wadau amabaye nilijikita sana kwenye kilimo cha umwagiliaji mpunga pale Dakawa kwa sasa nataka kupunzika na kuku wa kienyeji na Kisasa ...
ishu ipo kwenye kudizaini Banda lao ..
1. Naomba kuuliza Je naweza niakawachanganya kwa pamoja? au ni vizri nikawawekea partition?
2. Vipi nawezaje Kukamata soko,
3. Sokoni kuku wa kisasa shingapi na wa Kienyeji shingapi?
4 Ni mbegu gani ipo kwenye Trend?
5. Changamoto zake
Asanteni