Habari yako, sijajua unafuga kuku wa aina gani lakini sisi ni wazoefu zaidi ya miaka kumi sasa kwa maana ya kutotolesha na kufuga kuku wa kienyeji, na mwanzoni tulihangaika sana na hiyo chanjo Ya MAREK'S .Lakini baadae bada ya kufanya uchunguzi tukagundua kuwa huo ugonjwa (MAREK'S) ugonjwa ambao ukiufananisha na wa binadamau ni sawa na unaowapata wakina mama(kifafa cha uzazi) ambao kwa kuku ni MAREK'S , kwa kawaida kuku akiumwa MAREK'S hufa ile siku ya kwanza kabisa atakapoanza kutaga(kama atakua ameathirika na huo ugonjwa). na huo ugojwa huwashika kuku wale wa mayai(ambao wako kwa ajili ya mayai tu).