Ufugaji wa Kuku wa Kisasa: Fahamu Mbinu, Faida, Changamoto na Masoko

Ufugaji wa Kuku wa Kisasa: Fahamu Mbinu, Faida, Changamoto na Masoko

nitafuteni
 

Attachments

  • 1443704157797.jpg
    1443704157797.jpg
    45.3 KB · Views: 650
Mkuu Amani nami nimeanza kufuga lkn Kuku wanakula sana mayai, pia nilipoongeza Kuku waliokuwepo wanafukuza wageni,msaada wako plz ,ni Mgeni kabisa kwenye fani hii
 
Niliingiza vifaranga 1,000 vya nyama - vikadumaa vyote - nusu vikafa- badala ya kupata hardly 3200*1000= 3.2m. nikajikuta napata laki Sita. kwa hiyo wageni wa ufugaji this business is so risk - usije kopa pesa ukaingia kwenye biashara hii utahama nyumba kukwepa deni la watu.

Anza na mtaji wako mwenyewe ili uwe kwenye safe side.

This is the best advice ELNINO
 
Pole sana mdau.
Yawezekana nimechelewa kidogo lakini ushauri wangu juu ya tatizo lako ni kwamba watenge hao kuku wagonjwa kutoka kwa wazima ambao hawana dalili ya ugonjwa.
Hakikisha hawachangii maji wala sehemu ya chakula.
 
Katika Mtizamo wa kibiashara wenye faida nzuri kufuga kuku wa Mayai na kufuga kuku Chotara ni aina gani ndiyo nzuri.

shukrani sana
 
Katika Mtizamo wa kibiashara wenye faida nzuri kufuga kuku wa Mayai na kufuga kuku Chotara ni aina gani ndiyo nzuri.

shukrani sana
Umeuliza swali ambalo kinanisumbua sana, wakuu tusaidie majibu kwa wenye ujuvi
 
naomba kujua nahitaji chakula kiasi gani kulisha kuku (broiler) 200 hadi kufikia kuwauza
pili je faidA naweza pata japokuwa itakuwa ni kidogo???
 
Habari zenu wadau wa ufugaji, Mimi najihusisha na ufugaji wa kuku wa kisassa wa mayai na wameshaanza kutaga kama miezi miwili imepita lakini wanataga mayai yenye size ndogo kama mayai ya kuku wa kienyeji, Je hii ni kawaida? maana mayai madogo ya kisasa hayana soko, Je nifanyeje ili waweze kutaga mayai yenye umbo kubwa? naomba ushauri wenu wadau.
 
attachment.php
attachment.php
Katika ujenzi wa mabanda ni muhimu sana kuzingita kuwa hewa ya kutosha inazunguka katika mabanda yako kwa kuweka madirisha makubwa hasa kwenye maeneo ya joto
 

Attachments

  • banda la kuku 2.jpg
    banda la kuku 2.jpg
    42.6 KB · Views: 1,265
  • Banda la Kuku.jpg
    Banda la Kuku.jpg
    39.9 KB · Views: 1,012
Mkuu ahsante sana

Naomba msaada wako hapa. Nataka kujenga mabanda mawili, ili kufuga kuku wa kienyeji.

Lengo niwe ni muuza mayai na kuku kwa biashara.

Banda la kwanza litakuwa na ukubwa wa square meters 140 na lingine litakuwa na square meters 90.

naomba kujua kama, ni kuku wangapi naweza kufuga hapo, ikiwa ni ufugaji wa nusu huria.

Pia naomba unishauri ni mbegu gani au aina gani ya kuku wa kienyeji itanifaa.
 
Naomba kufahamu...

1.Kuku mmoja (layer)aliyeanza kutaga anapaswa kula chakula chenye ujazo gani?

2. Kuku kukosa madini ya calcium (kudonoana na kula mayai) nini kifanyike?

3. Kuku kuacha chakula (kutokula) nini sababu na solution

4. Idadi ya vyombo vya kulishia (feeders na drinkers) unatakiwa uweje kulingana na idadi ya kuku?
 
Back
Top Bottom