Ufugaji wa Kuku wa Kisasa: Fahamu Mbinu, Faida, Changamoto na Masoko

Ufugaji wa Kuku wa Kisasa: Fahamu Mbinu, Faida, Changamoto na Masoko

NAFASI INAYOHITAJIKA KWA KUKU 1000 WENYE RIKA TOFAUTI (MABANDA YA KUKU)

[TABLE="class: grid, width: 500, align: center"]
[TR]
[TD]RIKA[/TD]
[TD]CHICKS

VIFARANGA[/TD]
[TD]
GROWERS

KUKU
WANAOKUWA
[/TD]
[TD]LAYERS

KUKU
WANAOTAGA[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]UMRI
KTK
WIKI
[/TD]
[TD]0-6[/TD]
[TD]7-20[/TD]
[TD]20-80[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]KUKU/ENEO LA
M[SUP]2 [/SUP]MOJA ZA MRABA

[/TD]
[TD]12[/TD]
[TD]9[/TD]
[TD]6[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]M[SUP]2 [/SUP]ZINAZOHITAJIKA
/KUKU 1000


[/TD]
[TD]83.7M[SUP]2[/SUP][/TD]
[TD]111.2M[SUP]2[/SUP][/TD]
[TD]166.6M[SUP]2[/SUP][/TD]
[/TR]
[TR]
[TD][/TD]
[TD][/TD]
[TD][/TD]
[TD][/TD]
[/TR]
[/TABLE]


Eneo watakaloshinda kuku 1000 wakati wa mchana, ambao hufugwa ktk mfumo wa nusu huria ni mita za mraba 10,000 .Hii inamaana kwamba ,kuku mmoja anahitaji eneo lenye mita za mraba 10.Kuhusu utagaji kuku wa kienji hana sifa ya utagaji wa mayai mengi.Kuku wa kienyeji hutaga kwa mzunguko.Kila mzunguko mmoja hutaga hutaga wastani wa mayai 15 na kuanza kuatamia,kutotoa na kulea vifaranga.Mzunguko huo huchukua wastani wa kipindi cha miezi 4 hadi 6 .Hali hiyo hiyo humfanya atage mayai machache kati ya mayai 30 hadi 60 kwa mwaka ukilinganisha na kuku wa kisasa ambao hutaga mayai 270 hadi 300.

Kuku wa kienyeji ukitaka watage mayai mengi wasiruhusiwa kuatamia,kila mayai yanayotagwa yaokotwe na kuhifadhiwa na kama mfugaji atahitaji kutotoresha, kama kuna kuku wengi ,ni vyema ikatumika machine ili kuzalisha vifaranga wengi zaidi.Kuku wa kienyeji anapokuwa kwenye mzunguko wa utagaji,kila siku hutaga yai moja.

Mawasiliano yangu nimekutumia kwenye private message yako ya jf,nenda kwenye notification yako fungua utaona.

na mimh naomba mawasiliano yako mkuu.
 
Wapi naweza kupata chotara aliekaribu kutaga na jogoo wake na bei zikoje
Hukuk Dodoma unaweza ukapata kirahisi kwa sababu nasimamia vikundi vya wafugaji wa chotara ambao wanafuga kuku hao kwa ajili kupata mayai ya kutolesha. Hivyo kuna ambao wanafuga wakifikia miezi mitatu wanawauza. kwahiyo ukihitaji tuwasiliane utapata.
 
Mkuu ahsante sana

Naomba msaada wako hapa. Nataka kujenga mabanda mawili, ili kufuga kuku wa kienyeji.

Lengo niwe ni muuza mayai na kuku kwa biashara.

Banda la kwanza litakuwa na ukubwa wa square meters 140 na lingine litakuwa na square meters 90.

naomba kujua kama, ni kuku wangapi naweza kufuga hapo, ikiwa ni ufugaji wa nusu huria.

Pia naomba unishauri ni mbegu gani au aina gani ya kuku wa kienyeji itanifaa.

Slim5,
Ni matumaini yangu kuwa mzima. Nashukuru kwa maswali yako lkn naomba uniwie radhi kwa kuchelewa kukujibu. Banda lenye Square meta 140 kama ni kuku wa kienyeji unataka kufuga kwa ajili ya kuwafanya watagaji basi eneo hili litawatosha kuku 1120 maximum na Minimum Kuku 700. Lakini pia eneo hilo kama utamua kufuga kuku hao kwa ajili ya nyama kwa maana baada ya wiki miezi 3 au 4 unawauza basi utakuwa na uwezo wa kufuga kuku hadi 2100.

Kwa eneo la square mita 90 utafuga kuku 750 maximum na Minimum 500 kama utawafuga kwa ajili kuwafanya watagaji.

Ushauri wangu ni kuwa kama unataka kufanya Ufugaji wa Kibiashara fuga kuku chotara. unaweza kupata wale cross breed ya Pure line ya Rhode Island Red na Local wakwetu, au wale kuku weusi wa malawi nk, au Ukapata ile breed ya kenya na Uganda Kuroiler ukafuga hao utaiona faida ya ufugaji. Lakini kama utasema ufuge kuku pure wa kienyeji hawatakulipa kwakuwa ukuwaji wao pamoja uzalishaji wao ni mdogo ukilinganisha na gharama za uzalishaji.
Asante
 
Slim5,
Ni matumaini yangu kuwa mzima. Nashukuru kwa maswali yako lkn naomba uniwie radhi kwa kuchelewa kukujibu. Banda lenye Square meta 140 kama ni kuku wa kienyeji unataka kufuga kwa ajili ya kuwafanya watagaji basi eneo hili litawatosha kuku 1120 maximum na Minimum Kuku 700. Lakini pia eneo hilo kama utamua kufuga kuku hao kwa ajili ya nyama kwa maana baada ya wiki miezi 3 au 4 unawauza basi utakuwa na uwezo wa kufuga kuku hadi 2100.

Kwa eneo la square mita 90 utafuga kuku 750 maximum na Minimum 500 kama utawafuga kwa ajili kuwafanya watagaji.

Ushauri wangu ni kuwa kama unataka kufanya Ufugaji wa Kibiashara fuga kuku chotara. unaweza kupata wale cross breed ya Pure line ya Rhode Island Red na Local wakwetu, au wale kuku weusi wa malawi nk, au Ukapata ile breed ya kenya na Uganda Kuroiler ukafuga hao utaiona faida ya ufugaji. Lakini kama utasema ufuge kuku pure wa kienyeji hawatakulipa kwakuwa ukuwaji wao pamoja uzalishaji wao ni mdogo ukilinganisha na gharama za uzalishaji.
Asante

Ahsante sana mkuu, ntakutafuta. Shukrani.
 
Naomba kufahamu...

1.Kuku mmoja (layer)aliyeanza kutaga anapaswa kula chakula chenye ujazo gani?

2. Kuku kukosa madini ya calcium (kudonoana na kula mayai) nini kifanyike?

3. Kuku kuacha chakula (kutokula) nini sababu na solution

4. Idadi ya vyombo vya kulishia (feeders na drinkers) unatakiwa uweje kulingana na idadi ya kuku?

Ukifuatilia toka mwanzo wa thread kuna majibu ya maswali yote uliyouliza kwa kina..

1; Hula kg 0.12-0.13 kwa siku.So kuku 100 hula kg 12-13

2; Kuku gani hasa wa mayai au chotara?

3; Mara nyingi huwa ni ugonjwa na solution ni kwenda kwa mtaalamu ili akusaidie zaidi

4;Drinkers za litre 10 moja hufaa kwa kuku 50..feeders jaribu kuangalia pindi unapolisha uwiano wa kuku kwa feeder moja..Kama hazitoshi unaongeza.
 
Naomba kufahamu...

1.Kuku mmoja (layer)aliyeanza kutaga anapaswa kula chakula chenye ujazo gani?

2. Kuku kukosa madini ya calcium (kudonoana na kula mayai) nini kifanyike?

3. Kuku kuacha chakula (kutokula) nini sababu na solution

4. Idadi ya vyombo vya kulishia (feeders na drinkers) unatakiwa uweje kulingana na idadi ya kuku?

Ariella A.K,
Kuku anayetaga mmoja kwa siku anakula wastani wa gram 123. Kwahiyo kwa mafano ukiwa na kuku 1000 kwa siku utahitaji kilo 123 ambazo ni karibia ssawa na mifuko 2.5 wa kilo 50 kila mmoja. Na kama utakuwa na kuku 100 watahitaji kilo 12.3 kwa siku.

Wastani kilo moja kwa sasa kwa chakula Super ambacho kinauzwa tsh 55 kwa mfuko ni tsh 1100 kwa kilo moja kwahiyo kwa kuku 1000 ambao wanakula kilo 123 kwa siku utahitaji sh 135,300 kwa siku. Kwa hiyo ili uweze kupata faida inatakiwa kuku waka utagaji uanzie 60% ambapo utakuwa na faida kama 34700 kwa siku. Kama utakuji utakuwa zaidi ya 80% faida itakuwa kubwa zaidi. Bei ya mayai sasa hivi kwa jumla ni 8500 hadi 9000.

Kuku kusoma madini ya chuma Calciumhuwafanya kuku wako wadonoane wao kwa wao na wakati mwingine kula mayai yao. Lakini sababu nyingine za kudonoana ni pamoja na mrundikano wa kuku katika nafasi ndogo ya banda, vilevile mwanga mkali, upungufu wa madini kama hayo ya chuma,na pia kukosekana kwa mabox ya kutagia ambako hufanya kuku watage chini na kusababisha wenzao wawadonee pale wanapotaga.

Nini kifanyike, hakikisha kuku wanakaa kwa nafasi iliyoshauriwa kitaalam, pia wawekewe bembea zitakazikuwa zikiwashughulisha na michezi, pia wakati wa mchana wawekewe mboga mboga za majani mfano mchicha, chinese au majani yoyote yayopendelewa na kuku hao kuyatumia mfano Lusina nk. Vile vile chakula kiwe na chokaa pamoja na dcp ya kutosha. Lakini njia zote hizo zikishindikana basi kuku wakatwe midomo mara moja. Na mdomo tunaokata ni ule wa juu kwababu ndiyo unaotumkika kwa ajili kudonolea wenzake. Mdomo wa chini hutumika kwa ajili ya kulia chakula hivyo ukikata yote miwili utamuathiri katika ulaji wake kitu ambacho kitampa mshituko na kama ni watakaji watashusha ghafla utagaji wao.

Tunashauri ukataji wa midomo ufanyike wiki 15 kbla ya kuku hawajaanza kutaga lakini ikiwa wataanza mapema zaidi kudonoana basi hapo hapo wakatwe midomo yao.

Kuku kushindwa kula vizuri sababu kubwa ninayoiona mimi mara nyingi ni Ugonjwa, huenda kuku wako wanaumwa au kama watakuwa wamebadilishiwa chakula kutoka kile walichokizoea. Vile vile joto kali linapunguza ulaji wa kuku pia kama kuna makelele kuku hushituka na kuwafanya wapunguze ulaji wao. Kuku wakiwa sawa chakula chote wanachowekewa kwa siku kama share yao huwa ni lazima wamalize vinginevyo kuna kitu kinakuwa hakijaenda sawasawa na hivyo lazima mfugaji ufuatilie ili uweze kujua sababu hasa kama wanaumwa au la.

Idadi ya vyombo vya maji na chakula inategemea na idadi ya kuku ulionao lakini kwa mfano ukiwa na kuku 1000 hapo utahitaji drinkers 22 na feeders 43. Hapo kuku wote watapata nafasi ya kula wanapowekewa chakula. Faida ya kuwa na vyombo vya chakula vyenye uwiano sawa na kuku huwafanya kuku wako wasiwe wanapishana katika ukuaji wao na hivyo kama ni kuku wa mayai itawasaidia wasipishane katika kuanza utagaji wao na kama ni kuku wanyama itakufanya wewe mfugaji uwauze kwa makati mmoja kwa kuwa ule uzito wa kuwauzia yaani market weight watakuwa wamefikia kwa wakati mmoja.
Asante.
 
Kwa wale wanaohitaji mchanganuo wa mahesabu (Business Plan) kwa ajili ya kilimo au kwa shughuli nyingine yoyote ile basi tuwasiliane. Natengeneza michanganuo ya uhakika itakayokuhakikishia upatikanaji wa mikopo kutoka kwenye mabenki ili mradi uweze kutimiza masharti mengine yanayohitajika na benki husika zaidi ya mchanganuo wa mahesabu kwa bei nafuu ya 1% ya mtaji unaohitajika kwa ajili ya biashara yako na maongezi yapo kama 1% inakuwa ni kubwa.

Mara baada ya kupata data husika za biashara yako, haitazidi wiki mbili kupata business plan yako tofauti na watengenezaji wengi wengine ambao wanachukua mda mrefu lakini pia output zao ni za kiwango cha chini.

Nina uzoefu wa miaka 12 ndani ya sekta ya benki kama mtaalam wa maswala ya uhasibu katika masuala ya utengenezaji wa business plans.

Nimejikita kwenye shughuli hizi tangu October 2010 chini ya Sole Proprietership yangu inayoitwa Biznocrats Consulting Enterprise na nimeshatengeneza business plans nyingi katika maeneo tofauti na hakuna hata business plan moja iliyorudishwa na benki kwa kuwa chini ya kiwango.

Ofisi yangu ipo Makumbusho Bus Terminal & Shopping Complex, Block A, Ghorofa ya kwanza, chumba No. FF-04.

Tuwasiliane kwa namba yoyote kati ya hizi 0658 au 0772 977330
 
Habari zenu wadau wa ufugaji, Mimi najihusisha na ufugaji wa kuku wa kisassa wa mayai na wameshaanza kutaga kama miezi miwili imepita lakini wanataga mayai yenye size ndogo kama mayai ya kuku wa kienyeji, Je hii ni kawaida? maana mayai madogo ya kisasa hayana soko, Je nifanyeje ili waweze kutaga mayai yenye umbo kubwa? naomba ushauri wenu wadau.
hey wataalam tupeni majibu basi maana hata mimi nina tatizo kama hili.......ushauri tafadhali sio namba za simu
 
ufugaji wa broilers unaweza pata ugonjwa wa moyo coz hawastahimili magonjw'
ukiwa na mawazo haya kupiga hatua inakuwa ngumu...hakuna biashara au kazi isiyo pasua kichwa....tembea ukutane na wakulima waliolima mahindi then wafugaji wakaingiza ng`ombe ndio utajua bora kuku.....
 
KUKU WA KIENYEJI - UFUGAJI BORA





Kuku hutoka kwenye kizazi kinachojulikana kitaalam kama gallus gallus, Ufugaji huu nitaoelezea ni wa kienyeji kabisa ila huu umeboreshwa kidogo ili kuleta faida zaidi, kwanza itabidi uwe na eneo lakutosha kama ekari mbili (70m *140m) banda la kuku liwe linalohamishika na liwe limejengwa juu juu, hii husaidia kupunguza maambukizi ya magonjwa kwa sababu kinyesi cha kuku kikilundikana huweza kubeba vimelea vya magonjwa

BANDA BORA LINALOHAMISHIKA


Banda liwekewe viota vya kutagia na unaweza kuwafundisha kuku kuvitumia mapema kabla ya kuanza kutaga kwa kuchelewa kuwafungulia asubuhi. Kwa kawaida kuku hupenda kulala bandani wakiwa juu juu kwa hiyo uweke baadhi ya fito au mbao nyembamba zikining'inia pia kuwe na vyombo vya chakula nje ya banda

Hakikisha banda halivuji na wanyama wakali hawaingii lakini liwe na hewa ya kutosha na lisiwe na joto wala baridi kali, ni vizuri ukiliweka chini ya miti
Ili kuboresha ufugaji huu inashauriwa kutumia majogoo ya kisasa ambayo yana patika kwa mazalishaji wa kuku kote nchini, pia unaweza kutumia majogoo ya kuku aina ya KUCHI wanaopatikana zaidi miko ya Singida na Shinyanga. Majogoo ya kisasa huweza kuhudumia wastani wa majike 20-25 na kuchi huweza kuhudumia majike 10 -15 kwa sababu ni wavivu kidogo

MAJOGOO YA KISASA INA YA CORNISH


Andaa na banda la kukuziA watoto ambalo litawakinga na wanyama wakali na mwewe, banda linakuwa wazi juu hukulikizuiwa na waya kwa 75% na 25% iwe imezibwa kwa mbao ili kuwapatia kivuli wanapohitaji, banda hili lina hitaji kuhamishwa hamisha angalau mara 5 kwa siku kutika mahali pamoja hadi pengine, hakikisha banda la watoto lina maji na chakula muda wote, pia kumbuka kuwawekea mabaki ya mboga za majani kama mchicha, kunde, kisamvu n.k




FAIDA
(A)
Mfumo hauhitaji chakula maalum kama kuku wa ndani
(B) Wadudu kama utitiri na virobot hushambulia kuku mara chache
(C) Kuku hupata muda wa mazoezi kwa kutembea tembea
(D) Gharama za uendeshaji ni kidogo
(E) Hautumii muda mwingi
(F) Kiasi cha uchafu ni kidogo

HASARA
(A)
Vifaranga huweza kuliwa na mwewe au wanyama
(B) Mayai huweza kupotea yakitagwa nje ya banda
(C)Kuku huweza kula mbegu zilizopandwa mashambani
(D)Vifo vya kuku ni vingi

CHANJO
Kuku wapewe chanjo ya kideri/mdondo kila baada ya miezi mitatu chanjo hii hupatikana nchini kote ukifika dukani ulizia chanjo ya newcastle, utapata maelekezo ya jinsi ya kuwawekea kuku kwenye maji ya kunywa, chanjo hii wapewe kuku wazima tu na wagonjwa watengwe mbali

MINYOO
Kuku hunyweshwa dawa ya minyoo kila baada ya miezi mitatu, kuna dawa kama piperazine na nyinginezo ambazo huwekwa kwenye maji

CHAWA NA UTITIRI
Unaweza kutumia dawa za kuogeshea mifugo kama ecotix au dawa ya unga unga ya kunyunyuzia kama akheri powder, dawa ya akheri unaweza kuimwaga bandani na kisha kumnyunyuzia kuku mwilini ukiwa umemning'iniza kichwa chini miguu juu ili mayoya yaacha nafasi ya dawa kuingia

MAGONJWA YA MAPAFU
Kuna magonjwa mengi yanayoshambulia mfumo wa hewa, dawa ya tylosin inauwezo mkubwa wa kupambana na magonjwa karibu yote, wape dawa hii mara tu unapoanza kuona dalili za mafua

Source: Mitiki.blogspot.com
Mama shikamoo!!
Naomba msaada nataka kufuga kuku wa mayai 600 au 500 nataka kujua banda linatakiwa ukubwa gani Tafadhali sana nissidie
 
naomba unitumie meseji ya neno "kuku" kwenda +255 752 693 692

Mama shikamoo!!
Naomba msaada nataka kufuga kuku wa mayai 600 au 500 nataka kujua banda linatakiwa ukubwa gani Tafadhali sana nissidie
 
Habari zenu wadau wa ufugaji, Mimi najihusisha na ufugaji wa kuku wa kisassa wa mayai na wameshaanza kutaga kama miezi miwili imepita lakini wanataga mayai yenye size ndogo kama mayai ya kuku wa kienyeji, Je hii ni kawaida? maana mayai madogo ya kisasa hayana soko, Je nifanyeje ili waweze kutaga mayai yenye umbo kubwa? naomba ushauri wenu wadau.
Mara nyingi kuku wanapoanza kutaga hutoa Mayai Madogo. Na hii Ni kwasababu mfumo wa utengenezaji Mayai bado unakua. Kwa hiyo Kama chakula Ni kizuri basi ondoa Shaka maana baada ya muda si mrefu utaanza kuona Mayai yanaongezeka ukubwa
 
Ankojei ="ANKOJEI, post: 15364066, member: 31431"]naomba unitumie meseji ya neno "kuku" kwenda +255 752 693 692[/QUOTE]
Ankojei nimekutumia bana kange ndomile leleno
 
Ankojei ="ANKOJEI, post: 15364066, member: 31431"]naomba unitumie meseji ya neno "kuku" kwenda +255 752 693 692
Ankojei nimekutumia bana kange ndomile leleno[/QUOTE]


DU WE NOMA LUGHA GANI HIYO?
 
Back
Top Bottom