Asante mkuu kwa kuweka hii thread hapa jamvini. Naona unaendela kupata ushauri mzuri tu. Ila ingependeza sana mkuu kama ungejitahidi kuangalia dalili zote zinazoonekana. Kubandika tu picha haitoshi maana magonjwa yanayowafanya vifaranga wajikunyate yako mengi tu. Pengine ungetueleza kuhusu kinyesi chao (kina rangi gani?), kwenye pua zao kukoje, vichwa vyao vikoje, manyoya yao yamekaaje, tabia yao kwenye chanzo cha joto zikoje n.k. Hii itawasaidia hata madaktari wa mifugo waliopo hapa jamvini kukushauri vizuri zaidi.
Habari ya kukimbilia tu Antibiotics bila kujua tatizo ni nini siyo vizuri, ingawa hii watu wengi wanaipenda lakini huwa ni zima moto, yaani unafanya kwa vile tu Antibiotics zinatibu magonjwa mengi. Madhara ya kutumia antibiotics bila uhakika ni kuwafanya wanyama wawe sugu kwa dawa zingine, hii inaweza kusababisha mifugo kufa kutokana na ugonjwa umekosa dawa maana walishakuwa sugu.
Sitaki kuamini kwamba eneo ulilopo hakuna kabisa mtaalam wa mifugo, lakini mara nyingi wafugaji mnaogopa gharama za kumwita Mtaalam na mnajifanyia wenyewe bila kujua madhara yanayoweza kutokea. Kwa leo naweza kukuacha ukatumia hiyo dawa uliyoshauriwa na huyo mwenzetu lakini siku nyingine hebu jitahidi umwone mtaalam wa mifugo. Kwa vile umeamua kuingia kwenye hii shughuli hebu kubali gharama zozote zinazokuja kwa ajili ya kuboresha ufugaji wako.