Mradi wa ufugaji wa kuku una utajiri mkubwa ukifanyika kwa ufanisi. Huhitaji elimu kiasi katika utekelezaji wake, nguvu kiasi na muda wa kutosha. Ni rahisi, unaoweza kufanywa na mtu yeyote. Ufugaji wa kuku ni nyenzo muhimu katika kupambana na wimbi la umaskini. Pamoja na soko la uhakika, bado ufugaji kuku haujatumika ipasavyo kupambana na umaskini unao wakabili Watanzania wengi. Kuku wa kienyeji ambao hufugwa na watu wengi wamekuwa wakifugwa bila kupatiwa mahitaji muhimu kama chakula cha ziada, makazi bora, kinga na tiba za magonjwa pamoja na uangalizi! Hali inayo pelekea wafugaji kunufaika na kitoweo tu pamoja na kipato kidogo katika kazi yao ya ufugaji.
MIFUMO YA UFUGAJI WA KUKU WA ASILI
Ufugaji upo wa aina mbalimbali. Mifumo ya ufugaji inayo tumika sana hapa Tanzania ni;
- Ufugaji huria; unaweza kuuita ufugaji usio jali. Katika ufugaji hurua kuku huachwa kujitafutia mwenyewe chakula na maji na mfugaji hawajibiki kuwapatia chakula cha ziada na ikitokea ni mara chache sana. Kuku hulala eneo lisilo rasmi, kulala jikoni, kwenye kibanda au ndani kwa mfugaji n.k njia hii ni njia rahisi ambayo hutumika sana kufuga kuku wa kienyeji na huhitaji eneo kubwa litakalo tosha kuku kutembea ili kujitafutia chakula.
Faida zake;
- Kuku hupata chakula mchanganyiko ambacho kinawafaa kiafya.
- Kuku hupata hewa, joto na mwanga wa jua wa kutosha.
- Ni njia rahisi ya kufuga.
- Hutumia gharama ndogo katika kufuga, n.k
Hasara zake;
- Usalama wa kuku siyo wa uhakika hivyo wanaweza kuibiwa ana kudhuliwa na wanyama au kukumbwa na tatizo kwa namana yoyote.
- Ukuaji wa kuku ni hafifu.
- Huharibu mazingira kama kula na mimea ya bustanini mazao kama nafaka, n.k.
- Matunda yake ni madogo kiasi kwamba hawamnufaishi vizuri mfugaji.
- Ni rahisi kuambukizwa magonjwa.
Zingatia;
- Mfumo huu wa ufugaji ni rahisi lakini siyo rafiki kwa mfugaji mwenye malengo ya kufanikiwa.
- Nusu huria; Katika mfumo huu kuku hujengewa banda na kuzungushiwa wigo (uzio) kuzunguka banda. Kuku hulala kwenye banda nyakati za usiku na kushinda ndani ya uzio wakati wa mchana wakila chakula na maji humo. Nusu huria ni ufumo ambao huonesha sehemu kubwa ya mafanikio kwa mfugaji.
Faida zake;
-
- Utunzaji wa kuku ni rahisi ukilinganisha ufugaji huria.
- Kuku wanakuwa salama ukilinganisha na nfumo huria.
- Ni rahisi kudhibiti ukusanyaji wa mayai.
- Ukuaji wa kuku ni mzuri maana hupata chakula cha ziada.
- Ufugaji wa nusu huria huhitaji sehemu ndogo ya kufugia ukilinganisha na huria.
- Ni rahisi kuweka kumbukumbu.
Hasara zake;
-
- Gharama kiasi huongezeka katika ufugaji ukiliganisha na mfumo huria.
- Ugonjwa ukiingia, ni rahisi kuenea haraka.
- Matumizi ya muda mrefu ya eneo husika laweza kuwa na minyoo au vimelea vingine vya magonjwa.
Zingatia;
-
- Mfumo huu ni mzuri kwa ufugaji ila huhitaji usafi. Eneo husika lifanyiwe usafi kila siku na ikiwezekana kuwa na mzunguko wa kubadilisha eneo la kufugia angalau kila mwaka iwapo inawezekana.
-
- Shadidi; Shadidi ni mfumo wa kufugia ndani ya banda tu. Katika mfumo huu kuku hujengewa banda rasmi na hufugwa wakiwa ndani ya bada huku wakipatiwa chakula, maji na kupewa huduma zingine zote muhimu humohumo badani maisha yao yote. Mara nyingi mfumo huu hutumika kufugia kuku wa kisasa lakini ni mzuri pia katika ufugaji wa kuku wa asili. Sakafu ya banda la kutumia katika ufugaji shadidi ifunikwe kwa landa za mbao, makapi ya mpunga, majani makavu au maganda ya karanga.
Faida za ufugaji shadidi;
-
- Usalama wa kuku ni kamili.
- Huduma ya kuku ni nzuri na rahisi.
- Ni mfumo mzuri kwenye maeneo yenye uhaba wa ardi kwasababu huhitaji eneo dogo la kufugia.
- Ni rahisi kutibu maradhi ya kuku.
- Ni rahisi kudhibiti utagaji na ukusanyaji wa mayai.
- Japo usafi ni muhmu lakini hakuna haja ya kufagia kinyesi cha kuku kila siku.
- Faida ni ya uhakika.
- Ni rahisi kuweka kumbukumbu.
Hasara zake;
-
- Mfumo huu huhitaji gharama katika ujenzi wa banda, ulishaji wa kuku na huduma zingine za kuku.
- Hutumia muda mwingi kuhudumia kuku zaidi ya ufugaji huria na nusu huria.
- Kuna uwezekano kwa kuku kuatamia mayai bila mpangilio kama usimamizi hautoshi.
- Kuna uwezekano wa kuku kudonoana na kula mayai wasipokuwa na huduma na uangalizi mzuri.
- Ugonjwa ukiingia, ni rahisi kuenea haraka.
- Kuku watakosa mionzi ya jua ambayo ni muhimu kwa vitamin D.
Zingatia;
-
- Kuku wawiane na ukubwa wa banda. Wasizidi 6 kwa kila mita moja ya mraba.
- Bada liwe bora ambalo haliluhusu unyevunyevu na athali zingine za hari ya hewa kwa kuku.
- Chanjo ni muhimu.
- Usafi wa vyombo vya kulishia unahitajika.
KULEA VIFARANGA
Malezi ya vifaranga hufanywa na kuku hivyo ili kulea vifaranga vizuri inabidi kuiga mfano wa kuku anavyo lea. Vifaranga huhitaji joto, chakula, maji, uangalizi na huduma zingine ili wakue vizuri. Usalama wa vifaranga huhitajika ikiwa ni pamoja na kuhakikisha hawadhuliwi na mabadiliko ya hari ya hewa, wanyama hatari kama mwewe, kunguru, kenge, vicheche n.k
Vifaranga wa asili wanaweza kulelewa na kuku au kulelewa kisasa. Iwapo umetotolesha vifaranga wengi kwa wakati mmoja, unaweza kuwaweka walelewe na kuku mmoja kati ya walio totoa, mwenye upendo kwa vifaranga, asiye na ubaguzi au ukawalea kisasa na mama zao ukawaacha huru bila vifaranga ili wawahi kutaga tena.
Kulea vifaranga wa asili kwa kuku (mama zao);
Baada ya vifaranga kutotolewa waache na mama mahali penye usalama kwa muda wa mwezi mmoja, hakikisha wanapata maji na chakula cha kutosha kila siku. Unaweza kuandaa sehemu yenye usalama kwa ajili ya kulelea vifaranga kwa kujenga banda maalumu kwa ajili ya vifaranga au kuwafunika na tenga iwapo ni wachache kwa ajili ya usalama. Vifaranga wasipigwe jua wala kunyeshewa mvua. Kama unawafunika vifaranga kwenye tenga bila mama yao, hakikisha jioni unawarejesha kwa mama yao ili wapate kukingwa na baridi. Kwa kufanya hivi vifaranga wakifikisha umri wa mwezi mmoja watenge rasmi na mama yao.
Kulea vifaranga wa asili kwa njia ya kisasa (kwa kutumia kitalu);
Kitalu kinacho zungumziwa hapa ni sehemu maalumu ya kulelea vifaranga. Andaa kitalu cha kulelea vifaranga chenye ukubwa unao wiana na idadi ya vifaranga ulio nao. Kitalu kinaweza kuandaliwa ndani au nje ya banda ila kinatakiwa kuwa sehemu salama yenye kivuli, mwanga wa jua na hewa ya kutosha.
Kwa ufugaji mdogo hasa katika maeneo ya kijijini unaweza kuandaa kitalu kwa kutumia mifuko ya magunia; zungusha kuta mbili za magunia zinazo achiana nafasi ya nchi tatu katikati kisha hiyo nafasii iliyo wazi ijaze maranda ya mbao tayai utakuwa umepeta kitalu cha kulelea vifaranga.
Katika ufugaji mkubwa andaa kitalu/vitalu vya kudumu kwa ajili ya kulelea vifaramga. Vijengewe ukuta imara kwa kutumia tofari.
Weka taa ya chemli katikati ya kitalu ambayo itatumika kutoa joto linalo hitajika kwa ajili ya vifaranga. Pia unaweza kutumia taa ya umeme badala ya chemli. Njia nzuri na rahisi ya kulea vifaranga ni kwa kutumia taa kubwa nyekundu za umeme (wati 200 au 275) au tumia kipasha joto (Heater) Taa moja ya umeme inatosha kulea vifaranga mia moja thelathini katika sehemu za joto na vifaranga mia moja katika sehemu za baridi. Mwanzoni taa iwekwe umbali wa kati ya kitaru. Taa iendelee kushushwa karibu na vifaranga kadri bari inavyoongezeka.
Vifaranga wakisogelea sana taa jua joto halitoshi, ongeza joto kwa kupandisha utambi wa chemli au kama ni taa ya umeme, ishushe karibu na vifaranga ili wapate joto zaidi. Pia ukiona vifaranga wanasogea mbali na chemli/taa ya umeme, jua joto limezidi, punguza. Usizime chemli/taa hadi utakapoona vifaranga wametawanyika wote kwenye kitalu na kuonesha hali ya kuchangamka.
Kuku walio nyang’anywa vifaranga warudishwe kwenye kundi lenye jogoo ili wawahi kupandwa na kutaga tena. Kulea vifaranga wa asili kwa kutumia kitalu hufanya kuku waongezeke haraka.
Ili kudhibiti magongwa vifaranga wapewe chanjo dhidi ya magonjwa yafuatayo;
-
-
- Kideri (new castle) siku ya 3 baada ya kuanguliwa, rudia baada ya wiki tatu kisha uchanje kila baada ya miezi mitatu.
-
- Kuhara damu au rangi ya ugoro (Coccidiosis) : Wapewe kinga kwa dawa ya Amprolium kwa siku 3 mfululizo mara tu wanapofikisha umri wasiku 7 baada ya kuanguliwa.
- Gumboro; Kuku wanashusha mbawa na kujikusanya pamoja kwa baridi, pia wanaharisha kinyesi chenye rangi nyeupe. Hutokea kuanzia wiki ya 2 hadi ya 18. Wapewe chanjo siku ya 10 hadi ya 14 baada ya kuanguliwa na rudia baada ya siku 28 na 42. Na zingine utakazo shauriwa na mtaalamu wa mifugo wa eneo ulilopo.
Vifaranga wapewe chakula stahiki kwa umri wao na maji safi ya kutosha wakati wote kwa muda wa miezi miwili. Baada ya hapo wanapewa chakula cha kuku wanaokua.
Kuku wakikaribia kupevuka wakiwa na miezi mitatu hadi mine, tenganisha temba na majogoo ili kudhibiti kuku wenye uhusiano wa damu wasipandane wao kwa wao. Wakipandana na mayai yao yakianguliwa hawatatoka vifaranga wenye sifa nzuri.
mfano: Ukuaji wao utakuwa hafifu kuliko wazazi wao, uwezo mdogo kuhimili magonjwa na wengine wanaweza kuwa na ulemavu. Pia zingatia matemba hao wasipandwe na baba yao. Vilevile majogoo hao wasimpande mama yao, kwa masaada zaidi wa kitaalamu kuhusu mbinu bora za ufugaji wa kuku karibu
NaGA Media.