Ufugaji wa Kuku wa Kisasa: Fahamu Mbinu, Faida, Changamoto na Masoko

Nikweli mkuu
Upo sahihi, tatizo la wafugaji wengi wa broiler...hasa wanaojifunza wanasubiri mpaka kuku afike muda wa kuuzwa ndio wanatafuta soko, sasa wanunuzi wakichelewa siku moja tuu....unajikuta kuku wanaanza kula faida...na baadae hadi mtaji hasa kama siku zitaongezeka zaidi.
Mimi hutangaza soko siku kumi kabla ya muda wa kuuza, mnunuzi anakuja anawaona na ku make appointment .mapema...
Nikweli mkuu ifike mahala sasa wafugaji tubadilike. Tunafuga kwa mazoea sana.
 
Mradi wa ufugaji wa kuku una utajiri mkubwa ukifanyika kwa ufanisi. Huhitaji elimu kiasi katika utekelezaji wake, nguvu kiasi na muda wa kutosha. Ni rahisi, unaoweza kufanywa na mtu yeyote. Ufugaji wa kuku ni nyenzo muhimu katika kupambana na wimbi la umaskini. Pamoja na soko la uhakika, bado ufugaji kuku haujatumika ipasavyo kupambana na umaskini unao wakabili Watanzania wengi. Kuku wa kienyeji ambao hufugwa na watu wengi wamekuwa wakifugwa bila kupatiwa mahitaji muhimu kama chakula cha ziada, makazi bora, kinga na tiba za magonjwa pamoja na uangalizi! Hali inayo pelekea wafugaji kunufaika na kitoweo tu pamoja na kipato kidogo katika kazi yao ya ufugaji.

MIFUMO YA UFUGAJI WA KUKU WA ASILI​

Ufugaji upo wa aina mbalimbali. Mifumo ya ufugaji inayo tumika sana hapa Tanzania ni;

  1. Ufugaji huria; unaweza kuuita ufugaji usio jali. Katika ufugaji hurua kuku huachwa kujitafutia mwenyewe chakula na maji na mfugaji hawajibiki kuwapatia chakula cha ziada na ikitokea ni mara chache sana. Kuku hulala eneo lisilo rasmi, kulala jikoni, kwenye kibanda au ndani kwa mfugaji n.k njia hii ni njia rahisi ambayo hutumika sana kufuga kuku wa kienyeji na huhitaji eneo kubwa litakalo tosha kuku kutembea ili kujitafutia chakula.
Faida zake;
  • Kuku hupata chakula mchanganyiko ambacho kinawafaa kiafya.
  • Kuku hupata hewa, joto na mwanga wa jua wa kutosha.
  • Ni njia rahisi ya kufuga.
  • Hutumia gharama ndogo katika kufuga, n.k
Hasara zake;
  • Usalama wa kuku siyo wa uhakika hivyo wanaweza kuibiwa ana kudhuliwa na wanyama au kukumbwa na tatizo kwa namana yoyote.
  • Ukuaji wa kuku ni hafifu.
  • Huharibu mazingira kama kula na mimea ya bustanini mazao kama nafaka, n.k.
  • Matunda yake ni madogo kiasi kwamba hawamnufaishi vizuri mfugaji.
  • Ni rahisi kuambukizwa magonjwa.
Zingatia;
  • Mfumo huu wa ufugaji ni rahisi lakini siyo rafiki kwa mfugaji mwenye malengo ya kufanikiwa.
  1. Nusu huria; Katika mfumo huu kuku hujengewa banda na kuzungushiwa wigo (uzio) kuzunguka banda. Kuku hulala kwenye banda nyakati za usiku na kushinda ndani ya uzio wakati wa mchana wakila chakula na maji humo. Nusu huria ni ufumo ambao huonesha sehemu kubwa ya mafanikio kwa mfugaji.

Faida zake;
  • Utunzaji wa kuku ni rahisi ukilinganisha ufugaji huria.
  • Kuku wanakuwa salama ukilinganisha na nfumo huria.
  • Ni rahisi kudhibiti ukusanyaji wa mayai.
  • Ukuaji wa kuku ni mzuri maana hupata chakula cha ziada.
  • Ufugaji wa nusu huria huhitaji sehemu ndogo ya kufugia ukilinganisha na huria.
  • Ni rahisi kuweka kumbukumbu.

Hasara zake;
  • Gharama kiasi huongezeka katika ufugaji ukiliganisha na mfumo huria.
  • Ugonjwa ukiingia, ni rahisi kuenea haraka.
  • Matumizi ya muda mrefu ya eneo husika laweza kuwa na minyoo au vimelea vingine vya magonjwa.

Zingatia;
  • Mfumo huu ni mzuri kwa ufugaji ila huhitaji usafi. Eneo husika lifanyiwe usafi kila siku na ikiwezekana kuwa na mzunguko wa kubadilisha eneo la kufugia angalau kila mwaka iwapo inawezekana.
  1. Shadidi; Shadidi ni mfumo wa kufugia ndani ya banda tu. Katika mfumo huu kuku hujengewa banda rasmi na hufugwa wakiwa ndani ya bada huku wakipatiwa chakula, maji na kupewa huduma zingine zote muhimu humohumo badani maisha yao yote. Mara nyingi mfumo huu hutumika kufugia kuku wa kisasa lakini ni mzuri pia katika ufugaji wa kuku wa asili. Sakafu ya banda la kutumia katika ufugaji shadidi ifunikwe kwa landa za mbao, makapi ya mpunga, majani makavu au maganda ya karanga.
Faida za ufugaji shadidi;
  • Usalama wa kuku ni kamili.
  • Huduma ya kuku ni nzuri na rahisi.
  • Ni mfumo mzuri kwenye maeneo yenye uhaba wa ardi kwasababu huhitaji eneo dogo la kufugia.
  • Ni rahisi kutibu maradhi ya kuku.
  • Ni rahisi kudhibiti utagaji na ukusanyaji wa mayai.
  • Japo usafi ni muhmu lakini hakuna haja ya kufagia kinyesi cha kuku kila siku.
  • Faida ni ya uhakika.
  • Ni rahisi kuweka kumbukumbu.
Hasara zake;
  • Mfumo huu huhitaji gharama katika ujenzi wa banda, ulishaji wa kuku na huduma zingine za kuku.
  • Hutumia muda mwingi kuhudumia kuku zaidi ya ufugaji huria na nusu huria.
  • Kuna uwezekano kwa kuku kuatamia mayai bila mpangilio kama usimamizi hautoshi.
  • Kuna uwezekano wa kuku kudonoana na kula mayai wasipokuwa na huduma na uangalizi mzuri.

  • Kuku watakosa mionzi ya jua ambayo ni muhimu kwa vitamin D.
Zingatia;
  • Kuku wawiane na ukubwa wa banda. Wasizidi 6 kwa kila mita moja ya mraba.
  • Bada liwe bora ambalo haliluhusu unyevunyevu na athali zingine za hari ya hewa kwa kuku.
  • Chanjo ni muhimu.
  • Usafi wa vyombo vya kulishia unahitajika.

KULEA VIFARANGA

Malezi ya vifaranga hufanywa na kuku hivyo ili kulea vifaranga vizuri inabidi kuiga mfano wa kuku anavyo lea. Vifaranga huhitaji joto, chakula, maji, uangalizi na huduma zingine ili wakue vizuri. Usalama wa vifaranga huhitajika ikiwa ni pamoja na kuhakikisha hawadhuliwi na mabadiliko ya hari ya hewa, wanyama hatari kama mwewe, kunguru, kenge, vicheche n.k

Vifaranga wa asili wanaweza kulelewa na kuku au kulelewa kisasa. Iwapo umetotolesha vifaranga wengi kwa wakati mmoja, unaweza kuwaweka walelewe na kuku mmoja kati ya walio totoa, mwenye upendo kwa vifaranga, asiye na ubaguzi au ukawalea kisasa na mama zao ukawaacha huru bila vifaranga ili wawahi kutaga tena.

Kulea vifaranga wa asili kwa kuku (mama zao);

Baada ya vifaranga kutotolewa waache na mama mahali penye usalama kwa muda wa mwezi mmoja, hakikisha wanapata maji na chakula cha kutosha kila siku. Unaweza kuandaa sehemu yenye usalama kwa ajili ya kulelea vifaranga kwa kujenga banda maalumu kwa ajili ya vifaranga au kuwafunika na tenga iwapo ni wachache kwa ajili ya usalama. Vifaranga wasipigwe jua wala kunyeshewa mvua. Kama unawafunika vifaranga kwenye tenga bila mama yao, hakikisha jioni unawarejesha kwa mama yao ili wapate kukingwa na baridi. Kwa kufanya hivi vifaranga wakifikisha umri wa mwezi mmoja watenge rasmi na mama yao.

Kulea vifaranga wa asili kwa njia ya kisasa (kwa kutumia kitalu);

Kitalu kinacho zungumziwa hapa ni sehemu maalumu ya kulelea vifaranga. Andaa kitalu cha kulelea vifaranga chenye ukubwa unao wiana na idadi ya vifaranga ulio nao. Kitalu kinaweza kuandaliwa ndani au nje ya banda ila kinatakiwa kuwa sehemu salama yenye kivuli, mwanga wa jua na hewa ya kutosha.

Kwa ufugaji mdogo hasa katika maeneo ya kijijini unaweza kuandaa kitalu kwa kutumia mifuko ya magunia; zungusha kuta mbili za magunia zinazo achiana nafasi ya nchi tatu katikati kisha hiyo nafasii iliyo wazi ijaze maranda ya mbao tayai utakuwa umepeta kitalu cha kulelea vifaranga.

Katika ufugaji mkubwa andaa kitalu/vitalu vya kudumu kwa ajili ya kulelea vifaramga. Vijengewe ukuta imara kwa kutumia tofari.

Weka taa ya chemli katikati ya kitalu ambayo itatumika kutoa joto linalo hitajika kwa ajili ya vifaranga. Pia unaweza kutumia taa ya umeme badala ya chemli. Njia nzuri na rahisi ya kulea vifaranga ni kwa kutumia taa kubwa nyekundu za umeme (wati 200 au 275) au tumia kipasha joto (Heater) Taa moja ya umeme inatosha kulea vifaranga mia moja thelathini katika sehemu za joto na vifaranga mia moja katika sehemu za baridi. Mwanzoni taa iwekwe umbali wa kati ya kitaru. Taa iendelee kushushwa karibu na vifaranga kadri bari inavyoongezeka.

Vifaranga wakisogelea sana taa jua joto halitoshi, ongeza joto kwa kupandisha utambi wa chemli au kama ni taa ya umeme, ishushe karibu na vifaranga ili wapate joto zaidi. Pia ukiona vifaranga wanasogea mbali na chemli/taa ya umeme, jua joto limezidi, punguza. Usizime chemli/taa hadi utakapoona vifaranga wametawanyika wote kwenye kitalu na kuonesha hali ya kuchangamka.

Kuku walio nyang’anywa vifaranga warudishwe kwenye kundi lenye jogoo ili wawahi kupandwa na kutaga tena. Kulea vifaranga wa asili kwa kutumia kitalu hufanya kuku waongezeke haraka.

Ili kudhibiti magongwa vifaranga wapewe chanjo dhidi ya magonjwa yafuatayo;
  • Kideri (new castle) siku ya 3 baada ya kuanguliwa, rudia baada ya wiki tatu kisha uchanje kila baada ya miezi mitatu.
  • Kuhara damu au rangi ya ugoro (Coccidiosis) : Wapewe kinga kwa dawa ya Amprolium kwa siku 3 mfululizo mara tu wanapofikisha umri wasiku 7 baada ya kuanguliwa.
  • Gumboro; Kuku wanashusha mbawa na kujikusanya pamoja kwa baridi, pia wanaharisha kinyesi chenye rangi nyeupe. Hutokea kuanzia wiki ya 2 hadi ya 18. Wapewe chanjo siku ya 10 hadi ya 14 baada ya kuanguliwa na rudia baada ya siku 28 na 42. Na zingine utakazo shauriwa na mtaalamu wa mifugo wa eneo ulilopo.
Vifaranga wapewe chakula stahiki kwa umri wao na maji safi ya kutosha wakati wote kwa muda wa miezi miwili. Baada ya hapo wanapewa chakula cha kuku wanaokua.

Kuku wakikaribia kupevuka wakiwa na miezi mitatu hadi mine, tenganisha temba na majogoo ili kudhibiti kuku wenye uhusiano wa damu wasipandane wao kwa wao. Wakipandana na mayai yao yakianguliwa hawatatoka vifaranga wenye sifa nzuri.

mfano: Ukuaji wao utakuwa hafifu kuliko wazazi wao, uwezo mdogo kuhimili magonjwa na wengine wanaweza kuwa na ulemavu. Pia zingatia matemba hao wasipandwe na baba yao. Vilevile majogoo hao wasimpande mama yao, kwa masaada zaidi wa kitaalamu kuhusu mbinu bora za ufugaji wa kuku karibu NaGA Media.
 
Mkuu Nlikua naomba unijuze vyakula bora kwa ajili ya vifaranga
 
Naombeni ushauri wenu.
Nina ishi dar, ila nataka kuanza ufugaji wa kuku na nataka kuanza na vifaranga kama 150, na mabanda nimejenga mkoan huko Kilimanjaro na. nitamweka kijana wa kusimamia ufugaji huo.
Tatizo linakuja nianze kufuga kuku gani? Kwa sababu nataka faida nzuri ya mayai na nyama. Nashidwa kujua aina gani ya kuku au vifaranga gani ninunue na wapi wanapatikana.
Kuna Sasso, Malawi, na kloiler hao sasso ni wazuri kwa kukua haraka sana Ila kwenye utagaji siyo wazuri kivile na kloiler kwenye ukuaji siyo wazur kivile Ila wanataga mayai vizuri na mazuri. Chagua hapo ila nakushauri chukua kloiler
 
Naombeni ushauri wenu.
Nina ishi dar, ila nataka kuanza ufugaji wa kuku na nataka kuanza na vifaranga kama 150, na mabanda nimejenga mkoan huko Kilimanjaro na. nitamweka kijana wa kusimamia ufugaji huo.
Tatizo linakuja nianze kufuga kuku gani? Kwa sababu nataka faida nzuri ya mayai na nyama. Nashidwa kujua aina gani ya kuku au vifaranga gani ninunue na wapi wanapatikana.
Nenda interchick kachukue chotara
 
Wakuu neema iwe juu yenu.
Naomba nielezee changamoto na faida nilizokumbana nazo katika ufugaji wa kuku.
Nanze na broilers ambao watu wengi huwaona hawana faida.
kwakweli kama unafuga hawa kuku na ukawa na soko kwa wakati nikimaanisha kuwa kuku wamefika siku za kuuzwa na soko likawa linaeleweka basi ukiuza vizuri utaona faida nzuri sana kwa mana kuku hawa ukiwa mzoefu unajua ni idadi ngapi ya mifuko ya chakula kuwalisha mpaka wafike muda wa kuuzwa.
Changamoto inakuja pale wamefika kipindi wauzwe halafu unakuta soko halieleweki kwa mfano una kuku 500 bandani basi itakubidi kuwalisha mfuko mzima wa kilo 50 kwa kila siku na kwa kufanya hivyo kwa siku hata 5 soko likichelewa basi ujue kuku ndo wamekula faida na pindi uuzapo utarudisha pesa ya mtaji tu.
Ushauri wangu kwa kuku wa aina hii mfugaji unatakiwa uwe na soko tayari ili ifikapo muda wa kuuza basi wasiendelee kukaa bandani na kutafuna faida yenyewe.
Kwa sasa nafuga hawa kuku aina ya kutoiler japo wenyewe wanaita kienyeji chotara. Kuku hawa ni wazuri sana sababu ufugaji wake hautofatiani kama wale wa asili.
Kuku hawa ununuapo vifaranga huwezi tambua majike ni wangapi na madume mangapi ila tunakuwa na imani kuwa uwiano siku zote unalingana.
Faida ya kuku wa hii ya kuroiler ni mayai yao.
kwa mana mayai huuzwa mengi kwa ajili ya utotoreshaji pamoja ya kula.
Mayai haya hayana tofauti na yale ya kienyeji pure na soko lake lipo wazi wazi. Faida nyingine ni hawa kuku wanapokua unakuwa na idadi kamili ya majogoo na kwa usahuri tunashauriwa kuweka uwiano wa mitetea 7 kwa jogoo 1 kisha unauza majogoo waliobakia.
Majogoo wa kuroiler ufika mpaka kilo 5 ya uzito na kwa haraka haraka unaweza kupata 30,000/= kwa jogoo mmoja.
Ulishaji wake si changamoto sana kama wale wa broiler, sababu unaweza kupata mchanganyiko wa chakula (formula) nzuri ukachanganya mwenyewe na kuona matokeo mazuri.
Changamoto iliyopo ni kwamba uvumilivu wa kuwalea toka vifaranga mpaka wafike miezi 5 hapo ni pesa inatoka tu.
Ushauri wangu kuku hawa pindi ufugapo wahahitaji uangalizi wa hali ya juu sana ili uje upate pesa baada ya hiyo miezi 5.
Magonjwa yanayosumbua sana ni kinyesi cha ugoro (coccidiosis)na kupelekea kuku kupata chorela. Changamoto hiyo ni kwa sababu ya kutopatikana maji salama maeneo mengi.
Mimi nilikuwa nikichemsha maji usiku na kuyahifadhi vizuri ifikapo asubuhi nawapa kuku, ilinisaidia sana kuondokana na maradhi hayo wakati bado wako wadogo mpaka miezi 2.
Changamoto ni sasa hivi kwa mana wamekua wakubwa na wanakunywa maji mengi kulingana na awali.

Ahsanteni sana japo uandishi wangu si mzuri.

Bham cihi.

Mkuu naweza kupata wapi hawa kuku aina ya kutoiler na bei zao ni kiasi gan pamoja na mazingira ya kuwafugia natakiwa niwe nimeyandaa kwa ubora gani.
 
Mkuu upo mahali gani kwanza. pili umeshajenga banda la kufugia?.
 
Nikiri Mimi nimeuza sana kuku, Ila kiukweli kwa sasa hivi soko zuri hasa LA uhakika ni kuku wa kienyeji pure. Demand yake ni kubwa sana na mara nyingi wateja wangu ambao ni mabar hupendelea kienyeji pure kwa ajili ya supu. Mimi nilikuwa nawachukulia singida na order ilifika mpk 60 per day. Kwa mwez nilikuwa na uwezo wa kuuza kuku mpaka 1000 au 1200 na zaid. Nilichojifunza kuku wa kienyeji anafaida sana kuliko hata kuroiler ukiamua kufuga kisasa na ukiwa na eneo kubwa. Ikungi singida Luna mzee alikuwa anafuga kienyeji na amefanikiwa sana. Kwangu naomba tu kuendelee kuwa na zuio LA kuingiza vifaranga ili wafugaji wetu wanyanyuke.
Mkuu naomba niku-PM. Naona una madini ninayohitaji sana
 
Wakuu neema iwe juu yenu.
Naomba nielezee changamoto na faida nilizokumbana nazo katika ufugaji wa kuku.
Nanze na broilers ambao watu wengi huwaona hawana faida.
kwakweli kama unafuga hawa kuku na ukawa na soko kwa wakati nikimaanisha kuwa kuku wamefika siku za kuuzwa na soko likawa linaeleweka basi ukiuza vizuri utaona faida nzuri sana kwa mana kuku hawa ukiwa mzoefu unajua ni idadi ngapi ya mifuko ya chakula kuwalisha mpaka wafike muda wa kuuzwa.
Changamoto inakuja pale wamefika kipindi wauzwe halafu unakuta soko halieleweki kwa mfano una kuku 500 bandani basi itakubidi kuwalisha mfuko mzima wa kilo 50 kwa kila siku na kwa kufanya hivyo kwa siku hata 5 soko likichelewa basi ujue kuku ndo wamekula faida na pindi uuzapo utarudisha pesa ya mtaji tu.
Ushauri wangu kwa kuku wa aina hii mfugaji unatakiwa uwe na soko tayari ili ifikapo muda wa kuuza basi wasiendelee kukaa bandani na kutafuna faida yenyewe.
Kwa sasa nafuga hawa kuku aina ya kutoiler japo wenyewe wanaita kienyeji chotara. Kuku hawa ni wazuri sana sababu ufugaji wake hautofatiani kama wale wa asili.
Kuku hawa ununuapo vifaranga huwezi tambua majike ni wangapi na madume mangapi ila tunakuwa na imani kuwa uwiano siku zote unalingana.
Faida ya kuku wa hii ya kuroiler ni mayai yao.
kwa mana mayai huuzwa mengi kwa ajili ya utotoreshaji pamoja ya kula.
Mayai haya hayana tofauti na yale ya kienyeji pure na soko lake lipo wazi wazi. Faida nyingine ni hawa kuku wanapokua unakuwa na idadi kamili ya majogoo na kwa usahuri tunashauriwa kuweka uwiano wa mitetea 7 kwa jogoo 1 kisha unauza majogoo waliobakia.
Majogoo wa kuroiler ufika mpaka kilo 5 ya uzito na kwa haraka haraka unaweza kupata 30,000/= kwa jogoo mmoja.
Ulishaji wake si changamoto sana kama wale wa broiler, sababu unaweza kupata mchanganyiko wa chakula (formula) nzuri ukachanganya mwenyewe na kuona matokeo mazuri.
Changamoto iliyopo ni kwamba uvumilivu wa kuwalea toka vifaranga mpaka wafike miezi 5 hapo ni pesa inatoka tu.
Ushauri wangu kuku hawa pindi ufugapo wahahitaji uangalizi wa hali ya juu sana ili uje upate pesa baada ya hiyo miezi 5.
Magonjwa yanayosumbua sana ni kinyesi cha ugoro (coccidiosis)na kupelekea kuku kupata chorela. Changamoto hiyo ni kwa sababu ya kutopatikana maji salama maeneo mengi.
Mimi nilikuwa nikichemsha maji usiku na kuyahifadhi vizuri ifikapo asubuhi nawapa kuku, ilinisaidia sana kuondokana na maradhi hayo wakati bado wako wadogo mpaka miezi 2.
Changamoto ni sasa hivi kwa mana wamekua wakubwa na wanakunywa maji mengi kulingana na awali.

Ahsanteni sana japo uandishi wangu si mzuri.

Bham cihi.
Hiyo cocordiosis ndo imenifanya nistop kuwafuga hawa walikufa sana hadi nikaogopa mkuu
 
Pole sana Toplemon, Hii ishu ni serious kuliko haya mafundisho wanayoyatoa kwa siku. mimi nilipata gharama za kuchemsha maji kila siku wakati vifaranga wangu wadogo mpaka walivyokua nikaacha so hivi sasa huwa nawapa anticox mara 3 kila mwezi ili kukabiliana nayo.
 
VYUNGU VYA KUTOA JOTO KWA VIFARANGA

Ni imala na vikubwa
Vina sehemu ya kutolea majivu (chember)
Vinatumia mkaa kidogo kwa muda mrefu
Vimetengenezwa kwa ubunifu wa hali ya juu
Vina tafauti na vyungu vingine
Vinatunza joto kuanzia masaa 12-15
Chungu kimoja kina uwezo wa kutoa joto kwa vifaranga 100
Bei zetu ni sh elfu 14@ chungu ila kwa mteja atakayenunua kuanzia vyungu 3 atauziwa sh elfu 13@ chungu na Kama mteja atakuwa mwenyeji wa dar es salaam ataletewa mpaka sehemu husika
Tupo dar es salaam temeke mkoani nako tunatuma kwa ghalama za mteja kwa uaminifu mkubwa
Weka oda yako mapama make wanaoitaji NI wengi
Tupigie kwa namba izi 0687474845 au
VYUNGU VYA KUTOA JOTO KWA VIFARANGA NI CHANZO CHA UHAKIKA CHA KUTOA JOTO
 
Back
Top Bottom