Ufugaji wa Kuku wa Kisasa: Fahamu Mbinu, Faida, Changamoto na Masoko

Ufugaji wa Kuku wa Kisasa: Fahamu Mbinu, Faida, Changamoto na Masoko

Naomba msaada je nawezaje kupata hawa Rhode Ireland red(RID)
au Barred polmouth rock. Niko entebbe Uganda ( majogoo 10 kila type ) ntashukulu sana msaada wowote
Ngamba,

Majogoo aina ya Barred polmouth rock na Rhode Island red ni mpaka nikuagizie kutoka uholanzi ambako ndiko wanakopatikana.Kwa Tanzania utapata wale waliochoka baada ya kutoa service kwa muda mrefu, ambao bei yao huuzwa tsh 20,000/=kwa mmoja.

Uholanzi wanauzwa wakiwa na umri wa siku moja na bei yao hadi wakiwa wafikishwa Tanzania ni tsh 17,000/=
Kumbuka haya ni majogoo ya kuku wazazi.
 
asante mkubwa hivi kuna chombo cha kuangulia mayai ya kienyeji ikiwezeka nitumie namba yk ya simu nitakutafuta

Mannu,

Natumai chombo cha kuangalizia mayai unachokusudia ni kile cha kukuwezesha kujua kama mayai ni mazima au la,au mayai yamo kwenye incubator yameatamishwa kwa siku kadhaa na hivyo ukataka kujua kama yametengeneza vifaranga au la.Kuhusu kuangalia kama ni mazima kwa maana kuwa na sifa ya kuwekwa kwenye incubator tayari kwa kutotoleshwa,hicho kifaa sikifahamu ila ,kama unatotolesha vifaranga na mayai yako unayapata kutoka kwa wakulima,ni muhimu ukauliza historia ya mayai toka yametagwa yamekaa siku ngapi. Wastani wa mayai toka kutagwa hadi kuwekwa kwenye mashine kwa ajili ya kutotoleshwa yasizidi siku kumi,ingawa kwa hatchery nyingi mayai hutumia mayai yaliyokaa siku saba na ile siku ya nane

Kama ni kuangalia mayai yaliyo kwenye machine ili kujua kama yametengeneza vifaranga au laa,kuna kifaa cha kuangalizia kinaitwa candle.
 
Habari wanajamvi?

Mkuu Kichwa mbovu tunashukuru sana kwa elimu yako murua. Tunachukua elimu na kuifanyia kazi. Sasa kama kuna wakala wa vifaranga vya Mayai yupo humu namuomba aniPM.

Nataka kuanza kufuga Ila tatizo vifaranga wa Mayai wamekuwa adimu...foleni imekuwa ndefu sana mpaka kupata..hope nitapata majibu murua

Nakushukuru mh. Pachanya,kuhusu wakala wa vifaranga wa mayai tuwasiliane kupitia +255767989713 nitakudarect kwa agent wa vifaranga hivyo,tena utawapata bila kusubiri.Asante.
 
Mkuu kichwa, hivi inakuaje Vifaranga wanatotolewa kwa siku 5? kuna mather mmoja ana incubator ndogo ya mayai 50 aina ya JN8-48, Sasa maajabu ni kwamba baada ya siku 18 mayai yalishushwa chini na ilipo fika siku ya 21 vifaranga walianza kutotolewa cha ajabu wanatoka watano, au watatu kwa siku na wanaendelea kutotolewa hadi leo hii, it means

Ni sababau zipi zinapelekea mayai kupishana muda mrefu sana kweye kutotolewa? make nilivyo juna mara nyingi wakianza siku ya 21 siku ya 22 au 23 huw wamemalizika,
Chasha,

Hapo tatizo liko kwenye mashine,joto lake haliko sahihi.Wakati mwingine kwa nje unaweza ukaona mashine yako ina joto sahihi,lakini kwa ndani haliko sawa.Kuangalia kama kuna utofauti wa joto linalosoma nje na lile la ndani,ni muhimu ukatumia clinical themometer(themometa ya kawaida ya wanayotumia manesi na madaktari kumwangalizia mgonjwa joto hospitali) kisha ining'inize ndani ya Incubator (machine ya kutotolea vifaranga).

Kama machine iko sawa,kwa upande wa joto na unyevunyevu,vifaranga watazaliwa kwa muda muafaka yaani siku 21 na si vinginevyo.Mashine nyingi kwa kweli zina changamoto kubwa sana kwenye ufanisi wa utotoleshaji.Ni muhimu kuwa makini na kampuni unayoagiza na kununua Incubator.
 
Ngamba,
Majogoo aina ya Barred polmouth rock na Rhode Island red ni mpaka nikuagizie kutoka uholanzi ambako ndiko wanakopatikana.Kwa Tanzania utapata wale waliochoka baada ya kutoa service kwa muda mrefu,ambao bei yao huuzwa tsh 20,000/=kwa mmoja.

Uholanzi wanauzwa wakiwa na umri wa siku moja na bei yao hadi wakiwa wafikishwa Tanzania ni tsh 17,000/=
Kumbuka haya ni majogoo ya kuku wazazi.
Asante, swali ni kuwa je nawezaje kuwapata hapa nilipo maana kwa sasa naishi kwa mzee m7(Uganda-Entebbe) hio naona sio garama kubwa sana maana ninachoanfalia ni ubora wa bidhaa ninayotegemea kupata
 
Asante, swali ni kuwa je nawezaje kuwapata hapa nilipo maana kwa sasa naishi kwa mzee m7(Uganda-Entebbe) hio naona sio garama kubwa sana maana ninachoanfalia ni ubora wa bidhaa ninayotegemea kupata
Ngamba,

Kuhusu kuwapata wewe siyo shida,shida iliyopo ni kuwa kiwango cha chini kabisa kinachoruhusiwa kuagiza ni kuku wazazi 150,kwa hiyo idadi yako, mpaka nipate mtu ambaye atahitaji hivi karibuni nimwagizie hao parent stock kisha niunganishe na oda yako au kama utaweza kulipia 150 wote, it is ok, ndani ya mwezi mmoja utapata baada ya kukamilisha malipo.

Mara nyingi njia ya usafiri ninayokutumia kuingizia kuku wazazi kutoka uholanzi ni kwa njia ya ndege ya KLM.
Karibu.
 
Asante, swali ni kuwa je nawezaje kuwapata hapa nilipo maana kwa sasa naishi kwa mzee m7(Uganda-Entebbe) hio naona sio garama kubwa sana maana ninachoanfalia ni ubora wa bidhaa ninayotegemea kupata
Ngamba,

Kuhusu kuwapata wewe siyo shida,shida iliyopo ni kuwa kiwango cha chini kabisa kinachoruhusiwa kuagiza ni kuku wazazi 150,kwa hiyo idadi yako, mpaka nipate mtu ambaye atahitaji hivi karibuni nimwagizie hao parent stock kisha niunganishe na oda yako au kama utaweza kulipia 150 wote, it is ok, ndani ya mwezi mmoja utapata baada ya kukamilisha malipo.

Mara nyingi njia ya usafiri ninayokutumia kuingizia kuku wazazi kutoka uholanzi ni kwa njia ya ndege ya KLM.
Karibu.
 
Kahtaan,

Kiukweli wazo lako la ufugaji wa kuku ni zuri na linafaida sana. Kwanza kabisa kuku wa mayai wanalipa kama utafuata kanuni bora za ufugaji wa kuku. Lakini kama una mtaji wa mkubwa ni bora ukaanzisha hatchary (shamba la kuzalisha vifaranga wa kuku wa mayai na nyama) Inalipa sana.Ndani ya miaka michache utakuwa umesharudisha gharama zako zote na kuanza kutengeneza faida.

Eneo la ekari kumi ni kubwa na linaweza kutosha kufanyia shughuli zote za ufugaji unaotaka .Kwa kuku elfu nne au tano unaotaka kuanza nao,hapo utahitaji kuwa na mabanda 5 kila moja litabeba kuku 1000. Na katika kila banda utatakiwa utengeneze partition ya vyumba vitano kila kimoja utaweka kuku 250 na kimoja kitakochobaki ni kwa ajili ya kuwatengea kuku wagonjwa.Ingawa wakati mwingine unaweza ukawa na nyumba moja kubwa ikatosha kuku wote 5000, lakini ni hatari sana kama itatokea mlipuko wa magonjwa.

Nimeona huu mjadala wako niulete huku ili uwanufaishe na wengine pia .

Kuna vitu vingi nataka kukuelimisha hapa ili mpaka utakapoanza huo ufugaji wako utakuwa tayari na uelewa wa kutosha juu ya ufugaji wa kuku.

Asante.
 
Kahtaan,

Nakushukuru kwa kunipm,nimeona majibu niliyokupa pia niyalete huku kwenye thread ili kunufaisha na wengine.Nadhani sytem ya vifaa vya ufugaji ulivyonunua ni battery cages ambavyo hapa kwetu Tanzania hatuna mfumo huo.Ni mfumo ambao kila kuku anakaa kwenye cage yake,nadhani nitakuwa nimepatia kwa mujibu wa maelezo yako.

Ama kuhusu upatikanaji wa chakula cha kuku hapa Tanzania,kinapatikana tu vizuri bila shida na aina ya vyakula(ingredients) zinazotumika kwa ajili ya kutengeneza chakula cha kuku kwa mujibu wa formula za chakula nilizonazo ni kumi,mahindi yaliyobarazwa,pumba ya mahindi,mashudu ya alizeti,Soya iliyobarazwa,mifupa/dcp,Raw meal,(premix+unga laini wa soya),lysine,Methionine na Chumvi. Kwa kuchanganya mahitaji hayo utapata chakura bora cha kuku wa mayai,nyama na hata kuku wazazi.

Kuku wa mayai mmoja aliyeanza kutaga anakula kilo 52 kuanzia wiki ya 24 hadi 80.ILe miezi 2 ya mwanzo kuku mmoja anakula kilo 2,miezi minne inayofuata kuku mmoja anakula kilo 8.Bei ya chakula kilo moja layers mash tsh.660/=,chicks mash kilo moja tsh.760 na growers mash kilo moja tsh.700.

Mradi wa utotoleshaji wa vifaranga unahitaji pesa,kwa ajili ya kununulia parent stock(kuku wazazi),kununulia incubators,ujenzi wa hatchery(nyumba ya kutotoleshea vifaranga),mabanda ya kulelea vifaranga,nyumba za kutunzia kuku wazazi,Nyumba itakayotumika kwa ajili ya ofisi,nyumba ya kutengenezea chakula cha kuku,gharama za kununulia chakula cha kuku,mashine za kuchanganyia chakula cha kuku,Mishahara ya wafanyakazi ,stoo ya kuhifadhia chakula.nk.

Kwa kuanzia unaweza kuanza na kuku wazazi wa mayai 1000,na kuku wazazi wa nyama 500 wanatosha kabisa kukufanya kutengeza faida ya kutosha kabisa.Ila kama utahitaji naweza kukutengenezea business plan ya mradi mzima wa utotoleshaji wa vifaranga kwa gharama ya tsh 1000,000/=tu.Ukihitaji Business plan ya kuku wako 5000 wa mayai,pia naweza kukutengenezea kwa gharama hiyohiyo.

Mradi wa utotoleshaji wa vifaranga ukiwa na eneo la ekari mbili linatosha kabisa kwa ujenzi wa structure zote nilizoeleza hapo awali.

Umeme ni muhimu kwa mradi wa utotoleshaji wa vifaranga,hasa kwa ajili ya kuendeshea Incubators pamoja na brooding house(chumba cha kulelea vifaranga),lakini kwa kuku wazazi ambao ni wakubwa umeme si muhimu sana kwani usiku wanatakiwa wazimiwe taa ili walale na digestion iweze kufanyika vizuri.

Kuhusu kuwalisha kuku,kuku anahitaji alishwe mara moja tu share yake yote anayohitaji kula kwa siku,akishamaliza aachwe tu bila ya kuongezewa chakula kingine chochote isipokuwa maji yawepo muda wote.

Kama kuna sehemu utakuwa sijaeleka,usisite unaweza kuniuliza,kwa ufafanuzi.

Asante
cleardot.gif
 
Mkuu kichwa mbovu,

Naomba kujua utofauti wa pallet meal na hichi chakula cha kuku cha kawaida cha kuchanganya in terms of efficiency katika ubora wa ufugaji wa kuku. Naona sasa hivi kuna viwanda vikubwa vinajengwa cha Falcon Tegeta na Hill pale mapinga Bagamoyo kwa ajili ya utengenezaji wa pallet meal feed
 
Mkuu kichwa mbovu ..... naomba kujua utofauti wa pallet meal na hichi chakula cha kuku cha kawaida cha kuchanganya in terms of efficiency katika ubora wa ufugaji wa kuku ..... naona sasa hivi kuna viwanda vikubwa vinajengwa cha Falcon Tegeta na Hill pale mapinga Bagamoyo kwa ajili ya utengenezaji wa pallet meal feed

Bluetooth,

Ni pellet feeds,siyo pallet,ni chakula cha kuku ambacho kinatengenezwa kwa kutumia mvuke na kukiweka kwenye vipande vidogo vidogo vya mvilingo vilivyoungana pamoja na kuunda hicho chakula kinachoitwa pellet feeds. Pellets feeds hutengenezwa kutokana na chakula kilichotengenezwa kwa ingridients zote kikakamilika, kisha hubadilishwa na kutengenezwa pellets feeds.

Pellet feeds husaidia kuongeza ubora wa chakula,hurahisisha mmeng'enyo wa chakula kinachotokana na wanga, pia huzuia umwagikaji na upotevu wa chakula. Pellet feeds pia husaidia kushikamanisha virutubisho visipotee.
 
Huu ndiyo mwonekano wa mbele wa kitabu changu cha mwongozo wa ufugaji bora wa kuku.Bado naendelea kukiuza kwa wafugaji mbalimbali kote nchini.
 
Mkuu kichwa hongera sana,

Vipi unaweza jua njia ya kutambua mayai abayo hayana mbegu zidi ya kutumia Tochi? Kuna njia moja nilielezwa jana naRfaiki zangu za Kenya, Nataka nii tst and then nilete humu, Hii njia ni ya kuyatambua kabla hata hujayaweka kwenye mashine, na ile ya mayai yenye nyufa ngoja esho itakueleza matokeo yake make sikuwa kwenye site na yalemayai ndo yameanguliwa so nataka nikaprove kwa yale yenye nyufa
 
Mkuu kichwa habari za kazi
Mimi nataka kujua kwa mfano nataka niwe napata mayai ya kuingiza kwenye incubator yangu kama 1000 kila wiki inabidi niwe na kuku wazazi kiasi gani??
 
Ni bei gani? and kwetu sisi tulio mbali naweza kipataje (Uganda)?
 
Mkuu kichwa hongera sana,

Vipi unaweza jua njia ya kutambua mayai abayo hayana mbegu zidi ya kutumia Tochi? Kuna njia moja nilielezwa jana naRfaiki zangu za Kenya, Nataka nii tst and then nilete humu, Hii njia ni ya kuyatambua kabla hata hujayaweka kwenye mashine, na ile ya mayai yenye nyufa ngoja esho itakueleza matokeo yake make sikuwa kwenye site na yalemayai ndo yameanguliwa so nataka nikaprove kwa yale yenye nyufa
Tunasubiri utafiti wako ili uje utujuze mkuu,nadhani itakuwa faida kwetu sote.
 
Mkuu kichwa habari za kazi
Mimi nataka kujua kwa mfano nataka niwe napata mayai ya kuingiza kwenye incubator yangu kama 1000 kila wiki inabidi niwe na kuku wazazi kiasi gani??
Mh.king kingo,unatakiwa angalau uwe na kuku wazazi 200.
 
Ni bei gani? and kwetu sisi tulio mbali naweza kipataje(uganda)?

Bei yake ni tsh elfu sitini. Kwa Uganda naweza kukutumia kupitia Mabasi yanayakuja huko kama hard copy na itakulazimu pia utume gharama ya utumaji,au naweza kukutumia kama soft copy ambayo haina gharama yayote.
 
Bei yake ni tsh elfu sitini.Kwa Uganda naweza kukutumia kupitia Mabasi yanayakuja huko kama hard copy na itakulazimu pia utume gharama ya utumaji,au naweza kukutumia kama soft copy ambayo haina gharama yayote.
Habari za siku? Hivi kichwa mbovu hiyo soft copy na hiyo hard copy zina tofauti gani? Nakumbuka siku za nyuma sisi wa JF tuliwahi kukuomba hiyo soft copy lakini ukawa kimya! Sasa kama hiyo soft copy ni bure nitumie na mimi kwenye email yangu ambayo unayo. Vinginevyo ngoja nitafute hiyo elfu sitini kwani elimu ndiyo msingi wa kila kitu!
 
Back
Top Bottom