Kahtaan,
Nakushukuru kwa kunipm,nimeona majibu niliyokupa pia niyalete huku kwenye thread ili kunufaisha na wengine.Nadhani sytem ya vifaa vya ufugaji ulivyonunua ni battery cages ambavyo hapa kwetu Tanzania hatuna mfumo huo.Ni mfumo ambao kila kuku anakaa kwenye cage yake,nadhani nitakuwa nimepatia kwa mujibu wa maelezo yako.
Ama kuhusu upatikanaji wa chakula cha kuku hapa Tanzania,kinapatikana tu vizuri bila shida na aina ya vyakula(ingredients) zinazotumika kwa ajili ya kutengeneza chakula cha kuku kwa mujibu wa formula za chakula nilizonazo ni kumi,mahindi yaliyobarazwa,pumba ya mahindi,mashudu ya alizeti,Soya iliyobarazwa,mifupa/dcp,Raw meal,(premix+unga laini wa soya),lysine,Methionine na Chumvi. Kwa kuchanganya mahitaji hayo utapata chakura bora cha kuku wa mayai,nyama na hata kuku wazazi.
Kuku wa mayai mmoja aliyeanza kutaga anakula kilo 52 kuanzia wiki ya 24 hadi 80.ILe miezi 2 ya mwanzo kuku mmoja anakula kilo 2,miezi minne inayofuata kuku mmoja anakula kilo 8.Bei ya chakula kilo moja layers mash tsh.660/=,chicks mash kilo moja tsh.760 na growers mash kilo moja tsh.700.
Mradi wa utotoleshaji wa vifaranga unahitaji pesa,kwa ajili ya kununulia parent stock(kuku wazazi),kununulia incubators,ujenzi wa hatchery(nyumba ya kutotoleshea vifaranga),mabanda ya kulelea vifaranga,nyumba za kutunzia kuku wazazi,Nyumba itakayotumika kwa ajili ya ofisi,nyumba ya kutengenezea chakula cha kuku,gharama za kununulia chakula cha kuku,mashine za kuchanganyia chakula cha kuku,Mishahara ya wafanyakazi ,stoo ya kuhifadhia chakula.nk.
Kwa kuanzia unaweza kuanza na kuku wazazi wa mayai 1000,na kuku wazazi wa nyama 500 wanatosha kabisa kukufanya kutengeza faida ya kutosha kabisa.Ila kama utahitaji naweza kukutengenezea business plan ya mradi mzima wa utotoleshaji wa vifaranga kwa gharama ya tsh 1000,000/=tu.Ukihitaji Business plan ya kuku wako 5000 wa mayai,pia naweza kukutengenezea kwa gharama hiyohiyo.
Mradi wa utotoleshaji wa vifaranga ukiwa na eneo la ekari mbili linatosha kabisa kwa ujenzi wa structure zote nilizoeleza hapo awali.
Umeme ni muhimu kwa mradi wa utotoleshaji wa vifaranga,hasa kwa ajili ya kuendeshea Incubators pamoja na brooding house(chumba cha kulelea vifaranga),lakini kwa kuku wazazi ambao ni wakubwa umeme si muhimu sana kwani usiku wanatakiwa wazimiwe taa ili walale na digestion iweze kufanyika vizuri.
Kuhusu kuwalisha kuku,kuku anahitaji alishwe mara moja tu share yake yote anayohitaji kula kwa siku,akishamaliza aachwe tu bila ya kuongezewa chakula kingine chochote isipokuwa maji yawepo muda wote.
Kama kuna sehemu utakuwa sijaeleka,usisite unaweza kuniuliza,kwa ufafanuzi.
Asante